KUFANYA UTAFITI WA SOKO LA BIASHARA YAKO: UPEMBUZI YAKINIFU-2 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUFANYA UTAFITI WA SOKO LA BIASHARA YAKO: UPEMBUZI YAKINIFU-2



Upembuzi wa Bidhaa /Huduma.
Kipengele hiki  huelezea bidhaa au huduma jinsi;
·       Itakavyosafirishwa,
·       Wapi itakapozalishwa
·       Mahitaji kiasi gani
·       Utazalisha kiasi  gani kila mwezi
·       Ina upekee gani.

      Tekhnolojia /ufundi;
·       Ukubwa wa  mashine itakayotumika ukoje?
·       Kadiria mahitaji ya vifaa, malighafi katika biashara  yako. 
·       Ni kina nani, watakaokupa  teknolojia  utakayotumia
·       Je,  teknolojia utakayotumia ni ya kisasa au imepitwa na wakati?
·       Je, ni teknolojia  inayoweza ikaigwa  kirahisi?
·       Je, soko  linafikika kirahisi?
·       Malighafi zinapatikana kwa urahisi?
·       Tathmini usafiri.
·       Tathmini upatikananji wa vitendeakazi kama vile umeme, gesi maji        n./k
·       Tathimini  uchafuzi wa  mazingira.
·       Ni faida  gani  jamii itakayopata kutokana na huo mradi ?
·       Angalia  sheria na taratibu mbalimbali zinazohitajika kufuatwa.
·      Tathimini  mwitikio wa jamii inayokuzunguka juu ya kuanzisha                biashara   husika  katika mazingira yao.
·       Tafiti upatikanaji  wa malighafi  sasa na wakati ujao.
·       Tathmini ubora na bei za malighafi na njia mbadala za kupata                malighafi.
·       Chunguza upatikanaji wa nguvukazi, utawalipa mishahara kiasi gani,    uwezo wao n.k.


Utawala/management;
·       Muundo wa uongozi  wa biashara yako ukoje?
·       Ni kina nani wanaounda wanaounda  menejiment?
·       Uwezo wao ni upi?
·       Uwezo wao utasaidiaje biashara?
·       Wana uaminifu  gani ?
·       Udhaifu wao utarekebishwaje?
·       Utaajiri watu wangapi?
·       Je utawapeleka mafunzoni ( course)?

Fedha ;
·       Biashara yako itakugharimu  kiasi gani cha fedha kuianzisha?
·       Utatumia kiasi gani kuipanua?
·       Fedha  hizo  utazipata kutoka  wapi?
·       Unatarajia mauzo yako kwa mwezi, mwaka, yatakuwa kiasi gani?
·       Utaanza  kupata faida  baada ya muda gani kupita?
·       Utahitaji kukopa mahali ili uweze kutimiza malengo utakayojipangia?
·       Utahitaji mbia?

Kumbuka ya kwamba kwenye upembuzi yakinifu au utafiti maswali hayo yote unaweza ukapata majibu zaidi ya moja, yaani unatafuta njia zote zinazowezekana na kisha baadaye unazichuja ili kupata sasa zile unazodhani ni sahihi zaidi. Hizo sasa ndizo utakazozitumia katika kuandaa Mchanganuo wako wa biashara.





0 Response to "KUFANYA UTAFITI WA SOKO LA BIASHARA YAKO: UPEMBUZI YAKINIFU-2"

Post a Comment