Diamond: Tandale akifanya vitu vyake
|
Mkurugenzi
wa Global publishers, Eric Shigongo akizungumza ktk semina hiyo
|
Eric
Shigongo pamoja na wanasemina katika picha
|
SEMINA ya Ujasiriamali iliyokuwa ikifanyika katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Tandale, jijini Dar es Salaam, kwa muda siku
nne, ilihitimishwa kwa shamra baada ya mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Nasib Abdul Diamond, kutoa burudani ya muziki na kuongea na wakazi
wa eneo hilo.
Katika semina hiyo ilianza Aprili Mosi na kuhitimishwa
Aprili 4 mwaka huu ambapo wataalam wa ujasiriamali Eric Shigongo, James
Mwang’amba, Dr. Didas Lunyungu na Hassan Ngoma, walitoa mafunzo ya ujasiriamali
na namna mtu anavyoweza kujitoa katika umaskini na kupata mafanikio maishani.
Naye Diamond, alizungumzia jinsi maisha yake yalivyoanzia
hapo Tandale na baadaye kuwa ya mafanikio kutokana na juhudi zake anazoendelea
kuzifanya katika muziki, hivyo akawataka wakazi wa Tandale kutokukata tamaa.
‘’Nashukuru sana kwa semina hiyo mliyoipata kutoka kwa Eric
Shigongo, ambapo mkiifanyia kazi mtaweza kunufaika na kuwaletea maendeleo maana
mimi mwenyewe nimetokea Tandale hivyo nitaendelea kuwatia moyo kuwa kila jambo
linawezekana endapo mtu akiamua kujishughulisha,’’ alisema Diamond.
(HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
0 Response to "DIAMOND PLUTNUMZ: KILA JAMBO LINAWEZEKANA ENDAPO MTU AKIAMUA KUJISHUGHULISHA "
Post a Comment