Edson, mwanasayansi na mgunduzi mkubwa zaidi duniani, alikuwa akifanya kazi kama opereta wa simu wa muda(part time). Alifeli mara zisizohesabika kabla mwishowe hajafikishwa kwenye ugunduzi wa kipaji kilichokuwa kimelala ndani ya ubongo wake. Charles Dickens alianza kubandika lebo katika vyungu vyeusi. Mkasa wa penzi lake la kwanza ulipenya ndani ya roho yake na kumbadilisha kuwa mmoja kati ya waandishi vitabu wakubwa kabisa wa Dunia.
Kukatishwa tamaa kunakotokana masuala ya mapenzi kwa
ujumla kuna athari za kuwasukuma watu kwenye ulevi na uharibifu. Hii ni kwa
sababu watu wengi hawajifunzi kamwe stadi za kugeuza hisia zao kali kuwa ndoto
zenye kujenga.
Helen Keller alikuwa kiziwi, bubu, na kipofu mara tu
baada ya kuzaliwa. Licha ya taabu kubwa yote iliyomkuta, jina lake limeandikwa
kwa wino usiofutika katika karatasi za historia ya watu mashuhuri. Maisha yake
yote yalitumika kama ushahidi kwamba kamwe mtu hashindwi, hushindwa tu pale
atakapokubali kushindwa.
Robert Burns alikuwa kijana wa kijijini asiyekuwa na
elimu. Alilaaniwa kwa umasikini na kukua akiwa mlevi. Dunia ilifanywa bora kwa
yeye kuwa ameishi kwani alikuwa amejivika mawazo mazuri katika ushairi, hivyo
kung’oa mwiba na kuotesha waridi mahala pake.
Booker T. Washington alizaliwa katika utumwa akalemazwa
kwa ukabila na rangi. Kwa kuwa alikuwa mvumilivu, mwenye akili iliyofunguka
muda wote, katika masuala yote, na alikuwa muotajindoto, aliacha chapa yake kwa
mema katika jamii nzima.Beethoven alikuwa kiziwi, Milton alikuwa kipofu, lakini
majina yao yatadumu kwa kadiri muda nao utakavyopita kwa sababu waliota ndoto
na kuzibadilisha ndoto zao kuwa mawazo yaliyopangilika.
Kabla ya kuhamia kwenye sura inayofuata, amsha upya
akilini mwako moto wa matumaini, imani, ujasiri na uvumilivu. Ikiwa utakuwa na
hali hizi za akili, pamoja na maarifa ya kazi ya kanuni zilizoelezwa, vingine
vyote utakavyohitaji vitakuja kwako utakapokuwa tayari kuvipata. Let Emerson
analielezea wazo hili katika maneno yafuatayo “Kila mithali, kila kitabu, kila
jambo mashuhuri lililokuwa lakwako kwa msaada na faraja kweli litakuja
nyumbani kupitia njia iliyokuwa wazi au
njia iliyopindapinda. Kila rafiki, ambaye roho yako inamtamani mwishowe
atakukumbatia.
Kuna tofauti kati ya kutamani kitu na kuwa tayari
kukipokea. Hakuna aliyekuwa tayari kwa kitu mpaka pale atakapoamini kuwa
atakipata. Hali ya akili ni lazima iwe na imani na siyo matumaini matupu ama
matamanio. Utayari wa akili ni muhimu kwa imani. Akili iliyofungwa haihamasishi
imani, ujasiri wala kuamini.
Kumbuka, nguvu inayohitajika kuweka malengo makubwa
maishani katika kupata mali na utajiri ni sawasawa na ile inayohitajika kuleta
mateso na umasikini. Mshairi mashuhuri kwa usahihi kabisa ameeleza ukweli
huu unaokubalika na kila mtu kupitia mistari
ifuatayo;
Nilijadiliana bei na maisha,
Na maisha hayakutaka kuongeza pesa zaidi.
Hata hivyo niliomba tena jioni,
Nlipokuwa nafunga hesabu za duka langu dogo
Kwa kuwa maisha ni mwajiri tu,
Hukupa tu kile unachokiomba.
Lakini mara unapokuwa umepanga mshahara,
Kwanini, ni lazima utimize wajibu
Nilifanya kazi ya hali ya chini,
Kujifunza tu, mvunjiko wa moyo,
Kwamba mshahara wowote niliokuwa nimeomba,
Maisha yangelikuwa tayari kulipa.
Shauku
Hushinda Asili
Kama kilele muafaka cha sura hii, natamani kumtambulisha
mmoja kati ya watu wasiokuwa wa kawaida zaidi niliopata kuwajua. Nilimuona kwa
mara yangu ya kwanza dakika chache baada ya kuzaliwa. Alikuja duniani
pasipokuwa na dalili zozote za masikio ya kawaida na daktari alikiri hilo alipoulizwa atoe maoni yake kuhusu kama
mtoto angeweza kuwa kiziwi na bubu kwa maisha yake yote.
Niliyapinga maoni ya daktari. Nilikuwa na haki ya kufanya
hivyo; nilikuwa baba wa mtoto. Na mimi pia nilifikia uamuzi na kutoa pendekezo,
lakini nililisema pendekezo hilo kimya kimya, sirini ndani ya moyo wangu.
Niliamua kwamba kijana wangu angeweza kusikia na kusema.
Asili ingeweza kunitumia mtoto asiyekuwa na masikio,
lakini asili isingeweza kunishawishi kukubali ukweli wa mateso. Ndani ya akili
yangu nilijua kwamba kijana wangu angeweza kusikia na kusema. Kwa jinsi gani?
Nilikuwa na uhakika ni lazima kuna njia, na hili nilifahamu ningeweza kuipata.
Niliyafikiria maneno ya Bwana Emerson yasiyokufa “ Mlolongo mzima wa mambo
unaenda kutufunza imani. Tunahitaji tu kutii. Kuna mwongozo kwa kila mmoja
wetu, na kwa kusikiliza kwa unyenyekevu, tutaweza kusikia neno sahihi”
Neno sahihi? SHAUKU! Zaidi ya kitu kingine chochote,
Nilikuwa na shauku kwamba kijana
wangu asiwe kiziwi bubu. Kutoka shauku hiyo sikurudi nyuma hata sekunde moja.
Miaka mingi kabla niliandika hivi; “Mipaka yetu pekee ni ile tunayojiwekea
ndani ya akili zetu”. Kwa mara ya kwanza, nilishangaa ikiwa usemi huo ulikuwa
kweli.
Akiwa amelala kitandani mbele yangu alikuwa mtoto mchanga aliyezaliwa,
pasipokuwa na vyombo vya asili vya kusikia. Hata kama angeliweza kusikia na
kusema, alikuwa dhahiri mwenye ulemavu maisha yake yote. Ukweli, hiki kilikuwa
kikwazo ambacho mtoto yule hakuwa amejiwekea katika akili yake mwenyewe. Ni
kitu gani ambacho ningeliweza kufanya juu ya hilo?
0 Response to "NGUVU INAYOHITAJIKA KUWEKA MALENGO YA KUPATA MALI NA UTAJIRI NI SAWA NA ILE INAYOHITAJIKA KULETA MATESO NA UMASIKINI"
Post a Comment