Wanasayansi walisema
dawa hiyo mpya “ya kushangaza” inauwezo wa kufanya kazi vizuri dhidi ya
vimelea wa malaria ambao kwa sasa wameonyesha usugu kwa dawa nyingine
zilizokuwepo. Ina uwezo wa kufanya kazi kwa njia tofauti kabisa na dawa nyingine za malaria zilizoposokoni na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliana na tatizo la usugu wa dawa zilizopo kwa wadudu wa malaria.
Maelezo kwa kina kuhusiana na dawa hiyo yamechapishwa
katika jarida la kisayansi la “Journal Nature”
Dr. Keavin Read, kiongozi mwenza katika mradi huo alisema
kwamba dawa hiyo inahitajika haraka, kwani
usugu wa dawa zilizokuwepo sasa umekuwa tishio la kweli. Aliongeza
kuwa Malaria inaendelea kuhatarisha karibu nusu ya idadi yote ya watu Duniani na
ambayo pia ndiyo isiyokuwa na uwezo wa
kumudu gharama za kuutibu.
Chanzo cha habari hii ni BBC
Chanzo cha habari hii ni BBC
0 Response to "DAWA MPYA YA MALARIA YAGUNDULIWA NA WANASAYANSI"
Post a Comment