Kwa upendo jaribu kumpa
taarifa ya ua hili jirani, rafiki na ndugu zako ili wawe makini kwa ua
hili. Basi ngoja mimi Kapulya niwatakieni siku njema na tutaonana tena
panapo majaliwa. Jumatano njema!!
Ujumbe huu nimeuona katika
blogu ya Maisha na mafanikio na kwa kuwa mwenye blogu ameruhusu ujumbe
usambazwe kwa jirani nami nikaamua niitikie wito kwa kuuweka moja kwa moja hapa
katika blogu ya jifunzeujasiriamali kwani ni jambo jema kuwalinda hasa watoto
wetu na vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha na afya zao.
Binafsi nimeshtushwa sana na ua hili, sijui kama nalifananisha au ni vipi kwani kipindi nikiwa mdogo kijijini nilikuwa nikiona ua linalofanana na hilo na lilikuwa likipandwa katika bustani ya maua na mama zangu wadogo, sijui ikiwa walikuwa wanafahamu kama lilikuwa hatari kiasi hicho au la. Nitajaribu kufanya utafiti zaidi kuulizia ikiwa ndilo na kama watu wanafahamu hatari yake.
0 Response to "LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO"
Post a Comment