Akifunga ziara yake ya kihistoria Rais Barack Obama wa Marekani leo siku ya jumanne amewataka viongozi wa Bara la Afrika kuweka kipaumbele katika kutengeneza ajira mpya na fursa kwa vijana vinginevyo wahatarishe fursa nzuri za kiuchumi za baadae kwa mizozo na kutokufuata sheria.
Amesema “jukumu la
haraka” la kutengeneza ajira kwa idadi ya watu inayotegemewa kuongezeka kufikia
watu bilioni 2 katika miongo ijayo, “litakuwa ni jukumu gumu”. Lakini alisema
linaweza likafikiwa kwa msaada wa Marekani.
“Afrika itahitaji kutengeneza mamilioni ya ajira zaidi kushinda inavyofanya
sasa” Obama alisema alipokuwa akilihutubiaBara zima la Afrika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa Ethiopia.
Amesema “jukumu la
haraka” la kutengeneza ajira kwa idadi ya watu inayotegemewa kuongezeka kufikia
watu bilioni 2 katika miongo ijayo, “litakuwa ni jukumu gumu”. Lakini alisema
linaweza likafikiwa kwa msaada wa Marekani.
Rais Barack Obama akihutumia umoja wa Afrika AU mjini Addis Ababa Ethiopia |
“Afrika itahitaji kutengeneza mamilioni ya ajira zaidi kushinda inavyofanya
sasa” Obama alisema alipokuwa akilihutubia
Bara zima la Afrika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika.
“Uchaguzi utakaofanywa leo ndio utakaoamua ni njia ipi
Afrika ipite na hatimae Dunia katika miongo mingi ijayo” Alisema Obama ambaye
anaonekana na Waafrika wengi kama mtu wao. Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa
Raisi wa Marekani aliyekuwa madarakani kuhutubia Umoja wa Afrika. Hotuba hiyo pia
inahitimisha ziara yake ya siku 5 Barani Afrika ambayo hapo awali aliitembelea
Kenya, nchi ya baba yake alikozaliwa.
Obama pia aliwataka viongozi wa Afrika kuzifanya nchi zao
ziwe kivutio zaidi kwa wawekezaji kutoka nje kwa kusafisha rushwa, kuruhusu
uhuru wa kidemokrasia, kuunga mkono haki za kibinadamu na kuondoka madarakani
kwa amani na kwa hiyari pindi muda wao wa kukaa madarakani unapomalizika.
Obama ambaye muda wake uliobakia wa kukaa madarakani unaelekea
ukingoni, amewaambia; “Sielewi mantiki ya viongozi wanaokataa kuondoka
madarakani pale muda wao unapomalizika” Alitoa mfano kwa kiongozi wa Burundi
aliyerudi madarakani katika uchaguzi uliozua gumzo kutokana na muda wake kuwa
ulikuwa umemalizika.
“Kuna mambo mengi ambayo ningependa kuyafanya kuifanya
Marekani kusonga mbele. Lakini sheria ni sheria na hakuna aliyekuwa juu
yake, hata ikiwa ni Raisi” Obama amesema.
Ameahidi pia kuendelea kutoa usaidizi wa mafunzo na
misaada mingine katika mapambano dhidi ya ugaidi unaoendelea barani Afrika, na
makundi kama, Al-qaeda, Islamic State, Al-shabab na Boko haram.
Alisema Dunia ni lazima ifanye zaidi katika kupambana na makundi hayo na ataandaa mkutano hapo September Umoja wa mataifa kutafuta uungwaji mkono zaidi kimataifa na vikosi vya kulinda amani.
Alisema Dunia ni lazima ifanye zaidi katika kupambana na makundi hayo na ataandaa mkutano hapo September Umoja wa mataifa kutafuta uungwaji mkono zaidi kimataifa na vikosi vya kulinda amani.
Katika mkutano huo Obama alikaribishwa na mwenyekiti wa
Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye akimkaribisha, alimwambia
ingawa wanamkaribisha kama Rais wa Marekani lakini wanamuona kama wakwao.
Awali Rais Barack Obama alikuwa Mjini
Nairobi Kenya alipohudhuria Kongamano linalodhaminiwa na Marekani kuhusu maendeleo ya biashara na ujairiamali lakini pia alitumia fursa hiyo kukutana na ndugu zake
upande wa baba akiwemo dada yake Auma
Obama na Bibi yake wa kambo Sara.
Obama baada ya kumaliza ziara hiyo ya
kihistoria anatarajiwa kurudi jijini Washington mapema siku ya Jumatano.
0 Response to "HOTUBA YA RAIS OBAMA KWA WAAFRIKA ALIPOKUWA (AU) ETHIOPIA "
Post a Comment