Shirika la Dawa barani Ulaya, limetoa matumaini hayo baada ya
kutathimini usalama wake na uwezo wake wa kufanya kazi
Shirika la Afya duniani,WHO linatazamia kuidhinisha chanjo hii
kutumika kwa watoto, ambao miongoni mwao chanjo hiyoilileta majibu ya
mchanganyiko.
Ugonjwa wa Malaria huua watu takriban 584,000 kwa mwaka dunia
nzima, wengi wao watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kusini mwa jangwa la
Sahara.
Ndoto yawa kweli
chanjo iitwayo Mosquirix, au RTS,S ni ya kwanza dhidi ya
vijidudu vinavyosababisha malaria kwa binadamu.
Daktari Ripley Ballou, ni mtafiti toka Kampuni ya Glaxo Smith
Kline vaccines anasema huu ni wakati mzuri, amekuwa akifanyia kazi Chanjo hii
kwa miaka 30, anasema ndoto imetimia.
Kampuni hiyo haijaweka wazi gharama ya chanjo, lakini imeahidi
kutopata faida kutokana na chanjo hiyo.
Chanjo hii imetengenezwa mahususi kupambana na malaria kwa
watoto barani Afrika na haitaruhusiwa kutumika kwa wasafiri.
Watoto kati ya miaka mitano mpaka 17 wamekusudiwa kwenye chanjo
hii, ambapo walipatiwa chanjo tofauti aina tatu katika kipindi cha mwezi mmoja
kisha dawa ya chanjo nyingine katika kipindi cha miezi 20.
Katika kundi hili, watafiti walifanikiwa kupunguza athari za
ugonjwa huu kwa theluthi moja kwa kipindi cha miaka minne.
Bila dawa ya kuongezea nguvu chanjo isingeweza kupambana na
malaria kwa kipindi hicho cha majaribio.
changamoto iliyoonekana ni kuwa chanjo hiyo haikuonyesha uwezo
wake wa kuwakinga watoto wachanga dhidi ya malaria.
Hali hii inaiweka WHO katika njia panda, shirika hilo litaamua
mwezi Oktoba kuwa chanjo hiyo itumike au la, kwa sababu haikuwa na mafanikio
makubwa kama ambavyo wanasayansi walitegemea.
CHANZO CHA HABARI HII NI BBC SWAHILI
CHANZO CHA HABARI HII NI BBC SWAHILI
0 Response to "ILE CHANJO YA KWANZA YA MALARIA SASA IMEKAMILIKA"
Post a Comment