Wakenya wakiwa wanasubiri ujio wa ndugu yao
Barack Obama na ambaye pia nia Rais wa Taifa kubwa Duniani Marekani, tayari shamra shamra hizo
zimekwishaanza jijini Nairobi kwa
Kongamano la Ujasiriamali la Dunia (GES), ambapo wajasiriamali na
wafanyabiashara mbalimbali wamekwisha anza kuziweka bidhaa zao tayari kwa ajili
ya kuonyeshwa kwa wageni mbalimbali watakaoambatana na ugeni huo mkubwa ikiwa
ni pamoja na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali Duniani.
![]() |
Maandalizi ya kongamano la ujasiriamali la Dunia(GES) na ujio wa Rais Barack Obama Kenya sasa yameiva. |
Lengo kuu la kongamano hilo lililoasisiwa na
Marekani chini ya utawala wa Obama hapo mwaka 2010 ni kuendeleza na kuchochea
zaidi ujasiriamali kote Duniani. Nchini Kenya litafanyika Julai 25 mpaka 26
likiwa ni la sita likikusanya wajasiriamali wa ngazi zote kutoka kote duniani,
wakiwamo, viongozi wa makampuni, wawekezaji, mamilionea, watoamisaada, na maafisa
wakuu wa serikali.
UMUHIMU
WAKE.
Kongamano hili ni fursa kubwa kwa
wajasiriamali wa Kenya, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kuweza kukutana
ana kwa ana na wawekezaji na wajasiriamali wakubwa wa Dunia waliokuwa na uzoefu
mkubwa katika maswala mbalimbali ya ujasiriamali na uwekezaji kwa ujumla.
Ni kama linavyofanyika kombe la Dunia vile,
kongamano hili pia litachochea biashara, uwekezaji kwa mabilioni ya dola,
kukuza utalii pamoja na utamaduni. “Tunataka kuwekeza na kuzisaidia kampuni ndogo
za kiafrika ziweze kuwa kubwa katika
sekta ya nishati” anasema Larry Page
mwanzilishi wa mtandao wa Google. Katika kongamano hilo Rais Obama mwenyewe
atahutubia pamoja na wageni wengine.
0 Response to "KONGAMANO LA UJASIRIAMALI KENYA NA UJIO WA BARACK OBAMA"
Post a Comment