Vimelea wanaosababisha ugonjwa wa Malaria waitwao
Plasmodium waligunduliwa kwa mara ya kwanza hapo mwaka 1888, na kujulikana
kwamba mbu ndiyo wahusika wakuu katika kueneza vimelea hao ilikuja kugunduliwa
hapo mwaka 1898. Tangu kipindi hicho magonjwa mengi mfano wa surua na polio yaliyokuja
kugunduliwa nyuma yake yamepatiwa chanjo lakini Malaria bado haijaweza kupatiwa
chanjo mpaka hivi karibuni kabisa ambapo kumekuwa na matumaini kidogo ya kupatikana kwa chanjo hiyo.
Kwanini?
Malaria husababishwa na vimelea jamii ya Protozoa,
ni wakubwa na tata kuliko virusi. Wawapo
katika mwili wa binadamu kabla hawajachukuliwa na mbu jike aina ya Anofeles,
mfumo wake wa maisha ni tata na usiotabirika kama ilivyokuwa kwa bacteria na
virusi.
Ni wajanja sana kwani wanao uwezo wa kukwepa mfumo
wa asili wa kinga ya mwili(Natural immune system) ambao pamoja
na kuwa na nguvu sana lakini hauwezi kufua dafu kwa vimelea hawa.
Wanachokifanya ili kujikinga wasiuwawe ni kujificha ndani ya seli za mwili,
hupenyeza humo haraka na kujikinga na mfumo wa kinga ya mwili.
Wana mbinu nyingine tena ambapo wakiwa ndani ya seli hujijengea kitu
mfano wa ‘koti’ la protini linalowazuguka , na ingawa chanjo inaweza
ikatengenezwa kubaini hili koti, wadudu hawa wa malaria mara moja hujibadilisha
na kutengeneza koti lingine lisilotambuliwa na chanjo husika. Kwa hiyo hali
hiyo imefanya chanjo ya malaria kuwa kitu kigumu na ghali sana kutengeneza.
0 Response to "KWANINI CHANJO YA MALARIA IMEKUWA NGUMU HIVYO KUPATIKANA?"
Post a Comment