Kumbe hata mhalifu namba moja Duniani, Joaquin El Shapo
au Guzman, kwa jina la utani ‘Shorty’ au mtu mfupi, anafahamu dhana hii kuu
katika suala zima la ujasiriamali. Ujasiriamali unaweza ukatumika katika karibu
kila nyanja ya kimaisha hata katika shughuli haramu kama hii ya biashara za
madawa ya kulevya.
Mtu usipochukua hatari
yaani kufanya jambo ambalo mwisho wake hauna uhakika asilimia mia moja
ikiwa utaishia kupata faida ama hasara kamwe mafanikio katika ujasiriamali
hautayaona.(Simaanishi kwamba uhalifu nayo ni njia halali ya kujipatia kipato)
Kauli ya mhalifu huyo, ‘Zungu la unga’, na mtu
anayesakwa mno na Marekani aliitoa punde tu
baada ya kutoroka gereza lenye ulinzi mkali(maximum security) kushinda
yote nchini Mexico, alikokuwa ameshikiliwa kwa takribani mwaka mmoja. Guzman
hii si mara yake ya kwanza kutoroka jela, mara ya kwanza mwaka 2001 alitoroka
tena baada ya kuwahonga walinzi wa jela kiasi kikubwa cha pesa wakamtia kwenye
pipa la taka alilotumia kutorokea. Safari hii mnamo siku ya jumamosi usiku saa
2 katika bafu la kuogea alizama katika handaki lililokuwa limechimbwa chini kwa
chini na mainjinia wake, kazi waliyoifanya kwa muda unaokadiriwa kufika mwaka
mmoja.
Handaki hilo lilianzia katika jumba moja jirani na gereza
alimokuwa Guzman ambalo ujenzi unaonekana ulikuwa ukiendelea kwa nje kumbe kwa
ndani ndipo kazi ya kuchimba ilikuwa ikifanyika. Handaki hilo lililokuwa na
urefu upatao maili moja kutoka gereza lilipo kwenye bafu la kuogea mpaka
alipoibukia lina upana wa futi 2 na nchi
3, na urefu wa futi 5 na inchi6, urefu unaolingana na ‘Shorty’ mwenyewe
linakadiriwa kugharimu kiasi cha Dola milioni $50.
![]() |
Sehemu ya kuingilia kwenye handaki.
|
Ndani kulikuwa na kila kitu muhimu kuanzia taa za umeme,
mitungi ya hewa ya oxygen, toroli la kubebea mchanga na pikipiki kwa ajili ya
kusafiri haraka wakati anatoroka kutoka gerezani mpaka jumba lilipokuwa maili
1. Inakadiriwa pia udongo(kifusi) uliotokana na kazi hiyo unafika tani 3,250 na
ulihitaji magari zaidi ya 379 kuubeba lakini ajabu ni kwamba hakuna ripoti yeyote iliyoweza kuzifikia
mamlaka kutoka kwa waliohusika na ulinzi katika eneo hilo la gereza mpaka
anafanikiwa kutoroka.
‘Akitweet’ katika account inayosadikiwa kuwa ni ya mwanawe, Guzman
alimjibu kwa matusi makali mtangaza nia
wa chama cha Republican, Bilionea Donald Trump kwamba, atamfanya ayameze matamshi yake aliyoyatoa juu yake. Trump hapo kabla alikuwa amesema kwamba; Guzman anafaa kulaumiwa kwa kila jambo baya
linalotokea Mexico na kuongeza kwamba
angeweza kumpiga teke la “makalioni”.
Kufuatia tishio hilo Trump ameogopa na kwenda FBI kuomba uchunguzi ufanywe juu ya hiyo akaunti ya twiter. Hakuishia hapo, Mhalifu huyo pia alitweet kwa raisi wa nchi hiyo na kumwambia hivi; “Na wewe usiniite mhalifu, kwani nawapa watu ajira, tofauti na wewe mwanasiasa mwoga”
Kufuatia tishio hilo Trump ameogopa na kwenda FBI kuomba uchunguzi ufanywe juu ya hiyo akaunti ya twiter. Hakuishia hapo, Mhalifu huyo pia alitweet kwa raisi wa nchi hiyo na kumwambia hivi; “Na wewe usiniite mhalifu, kwani nawapa watu ajira, tofauti na wewe mwanasiasa mwoga”
Pia aliposti, “Kamwe
usiseme haitakaa itokee, hii dunia inazunguka. Katika maisha haya asiyechukua
hatari yeyote hawezi kufanikiwa” ( 'Never say never, this world keeps
turning. In this life, he who risks nothing cannot win')
Aliwataja pia watu
maadui zake aliosema ndiyo wa kwanza kuuwawa kwasababu walichekelea yeye afie
jela, mmoja wao ni El Chabelo mhalifu wa madawa ya kulevya mwenzake anayedai
alimsaliti.
Mashuhuda mtu na mkewe Lorenzo na Maria wanaoishi jirani na jumba
linalojengwa alimotorokea walisema kwamba walishangazwa kuona miezi sita
iliyopita akija mtu mgeni na eneo lile akajitambulisha kwa jina la ‘El Pastor’ (mchungaji
kondoo)na kudai alikuwa anahamia pale kufanya ujenzi wa nyumba.
Walieleza jinsi jinsi
mtu huyo alivyoingia kwenye jengo hilo la matofali mwanzoni mwa mwaka huu na kisha
baadaye kuanza msururu wa kazi za ujenzi. Mtu huyo mrefu, mnene na
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, mara kwa mara alionekana kuingiza ndani
na kutoa nje ya ‘saiti’ hiyo vifaa vya ujenzi akitumia gari yake nyekundu aina
ya 4×4 na Pick up nyeupe. Walisema; “Hakuwa mwenyeji wa eneo hili kabisa lakini
mara zote alionyesha urafiki wa hali ya juu. Alitueleza kwamba alikuwa akijenga
nyuma mpya kwenye hicho kiwanja lakini kamwe hatukuona mabadiliko yeyote ya
nje”.
Siku ya Jumamosi ambayo
ndiyo siku El Chapo alipotoroka, wanandoa hao wanaeleza kuwa waliona gari mbili
‘luxury’ sana aina ya 4×4 zikiingia kwenye kile kiwanja na siku iliyofuata
asubuhi waliziona tena zile gari zikiondoka pale zikiwa sambamba na magari
mengine mawili ya El Pastor.
![]() |
Gereza
la Altiplano linavyoonekana kwa mbali.
|
Awali Guzman
alipokamatwa mwaka jana serikali ya Marekani iliiomba sana serikali ya Mexico
impeleke akafunguliwe mashtaka Marekani kwa hofu kuwa ni lazima angetoroka
lakini Rais mpya wa Mexico Enrique
Peña Nieto aliyekuwa ameingia
madarakani akiapa kutokomeza magenge ya wauza madawa alikataa na kudai safari
hii asingeweza kutoroka tena. Serikali ya Mexico imeweka dau la dola milioni
3.8 kwa atakayefanikisha kumkamata.
Soko lake kubwa la
madawa ya kulevya lipo Marekani. Ni miongoni mwa watu matajiri zaidi Duniani
akimiliki mtandao mkubwa wa biashara ya madawa ya kulevya Duniani uitwao 'Sinaloa Cartel' , pia ana jeshi binafsi hatari
lililokuwa na uwezo wa kumuua mtu yeyote anayeingilia maslahi yake na ana uwezo
wa kuwahonga maafisa wengi katika serikali ya Mexico kufanikisha mipango yake. Mashabiki na wafuasi wake wanaokadiriwa kufikia milioni 3.2 huwa anatoa misaada mbalimbali pamoja na pesa na wengi humsaidia katika harakati zake za kujificha serikali isimkamate hasahasa eneo analotoka la Sinaloa.
Jarida la Forbes mwaka 2009 liliwahi kumweka miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kama kina Bill Gates na Warren Buffet, na lilisema alikuwa na utajiri uliofikia Dolla Bilioni 1.
Jarida la Forbes mwaka 2009 liliwahi kumweka miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kama kina Bill Gates na Warren Buffet, na lilisema alikuwa na utajiri uliofikia Dolla Bilioni 1.
Anamiliki pia ndege
binafsi pamoja na timu ya mainjinia mahiri walio na vifaa vya
kisasa kabisa wanaomwezesha kutengeneza miundombinu mbalimbali ya kujificha na
kutoroka hasa mahandaki na njia za chini kwa chini za kuingiza madawa nchini
Marekani.
![]() |
Kimwana,
mrembo aliyezaa naye mapacha.
|
Kamuoa pia mrembo mmoja
mwenye asili ya Marekani na Mexico, Emma Coronel, na amezaa naye watoto mapacha
wawili ambao mama yao alikwenda kuwazalia nchini Marekani ili wawe raia wa nchi
hiyo.
CHANZO: DAILY MAIL ONLINE
CHANZO: DAILY MAIL ONLINE
0 Response to "TAJIRI BILIONEA WA MADAWA YA KULEVYA ALIYETOROKA JELA “ASIYECHUKUA HATARI HAFANIKIWI”"
Post a Comment