ZIARA YA OBAMA NA MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI WA ALSHABAB KENYA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ZIARA YA OBAMA NA MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI WA ALSHABAB KENYA

Muda mfupi kabla Rais Barak Obama  hajapanda ndege ya Air force One kuelekea nchini Kenya nyumani kwa baba yake mzazi, aliiambia BBC kwamba, ziara yake nchini humo pamoja na Ethiopia  inampa fursa kama rais wa Marekani kushughulikia kwa undani zaidi ukanda huu na kuhutubia Bara zima la Afrika kupitia Umoja wa Afrika kwa mara ya kwanza kama raisi wa Marekani.

Alisema pia kwamba ziara yake hiyo na kongamano la Dunia la Ujasiriamali vina uhusiano mkubwa na suala zima la usalama kwa maana kwamba, “watu wanapoona fursa na wanapokuwa na hisia za kuwa na uthibiti wa maisha yao ya baadaye, hatari ya kughilibia na propaganda na itikadi kali kupitia mitandao ya kijamii hupungua”. 

Alisema pia kwamba huko nyuma wakati walipoanza kuangalia mikakati ya kuzifikia nchi za Kiislamu na zile zinazoendelea, ujumbe wa pamoja ulijitokeza nao ni watu hawavutiwi tu na kulelewa pamoja na kupewa misaada bali wanavutiwa zaidi na kujengewa uwezo. 

Aliongeza kwamba kadiri watakavyofundisha ujasiriamali hasa kwa vijana  ndivyo nao watakavyo kuwa na matumaini zaidi na hivyo  kuhimiza zaidi yale mambo wanayoyasisitiza sana kwa serikali zao kama vile, ukomeshaji wa rushwa na   kuongezeka kwa uwazi  wa jinsi serikali zinavyoendeshwa na kuhakikisha kwamba sheria na taratibu haziwekwi kwa ajili ya wasomi peke yao bali   zinamruhusu mtu yeyote aliyekuwa na mawazo mazuri ya kujenga aweze  kutekeleza kile anachokusudia kukifanya.

0 Response to "ZIARA YA OBAMA NA MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI WA ALSHABAB KENYA"

Post a Comment