Donald Trump, Bilionea maarufu anayemiliki majumba nchini Marekani, ameendelea kutawala mdahalo
wa kwanza katika kinyanganyiro cha kumpata mgombea urais wa Marekani kupitia
tiketi ya chama cha Republican licha ya kuzomewa na wanaompinga kutokana na
misimamo yake hasa juu ya sera zake za nje kama vile suala la wahamiaji kutokaMexico wanaoingia nchini humo nakusababisha tatizo la kuongezeka magenge ya wauzaji madawa ya kulevya.
Aliwaita wanasiasa kuwa ni “wapumbavu” na kwamba alikuwa
anajiandaa kuachana na chama cha Republicana na kwenda kuanzisha cha kwake.
Aliwalaumu wanasiasa wa marekani kuwa ni wajinga kwa kukubali kuwapokea
wahamiaji wa Kimexico wakati viongozi wa Mexico wenyewe wakionekana kuwa ni
werevu na wajanja kwani huwatuma ‘wahalifu’ na ‘wabakaji’ kwenda nchini
Marekani.
Watangaza nia walikuwa 17 katika mdahalo huo lakini
Donald Trump ndiye aliyengara zaidi akifuatiwa na wengine wachache kama vile,
gavana wa zamani wa Florida na mdogo wake Rais wa zamani George W Bush Jeb Bush, wengine ni Seneta wa Florida, Marco Rubio,
Gavana wa Wisconsin Scott Walker na wengineo.
Atakayeibuka kidedea katika kinyanganyiro hicho
atakabiliana na mgombea atakayekuwa
amesimamishwa na chama hasimu cha Democrat katika kumtafuta Raisi na kwa
kiasi kikubwa imeshatabiriwa na wengi kuwa huenda akawa Bi Hillary Clinton,
mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika Taifa hilo kubwa
Duniani.
0 Response to "MTANGAZANIA BILIONEA DONALD TRUMP WA CHAMA CHA REPUBLICAN AZOMEWA"
Post a Comment