Akimlinganisha Lowassa na mbia wa biashara alisema kuwa
katika biashara yeyote ile hata kama ni ya ufugaji wa kuku unapomkaribisha mtu
ni lazima uhakikishe kuwa yule utakayemkaribisha ni lazima awe asseti yaani
rasilimali na si Liability au ‘mzigo’. Amesema unaweza kuwa na mtaji wako wa
kuku 200 ulioudunduliza kwa jasho kwa muda mrefu, sasa unapoamua kumkaribisha
mbia, angalao basi aje na hata na mtaji wa kakuku kamoja.
Lakini anasema baada ya kuchunguza katika hatua zile za kumkaribisha Lowassa alibaini hakuwa na majina yeyote ya wabunge aliokuwa amedai anahama nao CCM, bali alikuwa tu na namba ya watu. Kwa maana hiyo amesema Lowassa hakuwa mtaji bali hasara au mzigo kwa kuwa hakuwa na mtaji wa watu wengi kama ilivyokuwa imedhaniwa.

Alisema yeye siasa ya ulaghai haitaki ndiyo maana aliamua
kujiondoa kwenye siasa. Dhana kwamba Chadema wanataka waiondoe kwanza CCM
madarakani pasipokuwa hata na programu inayoeleweka huku wakitumia watu wale
wale ni kujidanganya, ni upuuzi. Alisema ni afadhali apotee katia ramani ya siasa Duniani kuliko kuikana dhamira yake.
Alimalizia kwa kusema kuwa kama Taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua na ukishaumwa na nyoka, usirudie tena kuumwa na nyoka akimaanisha kuwa kipindi kinachomalizika wananchi waliahidiwa maisha bora na sasa hawajayapata. Pia aliwaasa waandishi wa habari kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika habari zao. Amesema kwamba yeye amestaafu siasa, na hana chama chochote, ataendelea kuwatumikia wananchi wanyonge akisimamia misingi ya ukweli.
Awali wakati Mheshimiwa Edward Lowassa alipokuwa akihamia katika chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, kulitokea mtikisiko mkubwa baada ya Dr. Wilbroad Slaa na Profesa Ibrahimu Lipumba wa chama cha CUF kuamua kujiuzulu nafasi zao katika vyama vyao chini ya muavuli wa umoja wa vyama vya upinzani uitwao Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)

0 Response to "DR. SLAA: LOWASSA HAKUWA ASSETI ALIKUWA LIABILITY(MZIGO)"
Post a Comment