Duniani hapa kuna vitu vidogo vidogo na vya kawaida sana kiasi kwamba mtu akikuambia vinaweza vikakatisha uhai wako mara moja inakuwa vigumu sana kuamini. Ni mpaka pale janga hilo lilkukumbe au limkute mtu wako wa karibu kama vile mtoto, kaka, dada shangazi, mjomba nk.
Mimi binafsi sikuwa nalijua hili hapo kabla, mpaka pale
mteja wangu mmoja alipokuwa akinunua mswaki. Kila mara anapofika dukani kununua
mswaki, huwa nashangaa vile anavyokuwa makini na aina ya mswaki anaotaka,
anauliza ikiwa mswaki niliokuwa nao unatoa nyuzinyuzi kirahisi, maana yake ni
kwamba huwa anataka kuhakikisha kuwa mswaki anaonunua ni bora na imara
usiopukutika kirahisi.
Nilipotaka kujua ni kwa nini anakuwa makini kiasi kile
alinieleza kisa kizima, kwa kweli nikabaki “mdomo wazi” kwani sikuamini kabisa
alichokuwa akinisimulia;
“Siku
moja asubuhi Shangazi yangu alikuwa akipiga mswaki kama kawaida yake, lakini
ghafla akasikia kitu kama kiuzi kimeingia katika koo lake la hewa, kikaanza
kumpalia. Yeye alidhani kama kawaida kitatulia tu na kutoka chenyewe lakini
kumbe haikuwa hivyo, ikabidi apelekwe hospitali teule ya Tumbi ambako alilazwa
kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Hata operesheni ilikuwa ni vigumu kumfanyia hadi
mgonjwa anakata roho” Alimaliza kunisimulia mteja wangu
anayejulikana kwa jina la Sefu.
Inavyosemekana ni kwamba, kitu kidogo sana kama vile ‘unywele’
wa mswaki unapoingia kwenye koo la hewa na kwenda kuganda katika kuta
zake inakuwa vigumu sana kwa madaktari kukiondoa pale kwani hata kwa njia ya
upasuaji inaweza isiwezekane kutokana na sehemu yenyewe kuwa tete mno (delicate)
Hivyo inashauriwa watu kuwa makini siyo na miswaki tu bali hata na vitu
vingine vyovyote vile vya jamii ya manyoyanyoya au nywele.
Mwanadada
akipiga mswaki.
|
Hakikisha unaponunua miswaki kwa familia yako, basi
angalao uchague ile imara na yenye ubora unaoaminika hata ikiwa bei yake ni
kubwa. “Ni heri kujikinga kuliko kujitibu”.
Halikadhalika pia inashauriwa na wataalamu wa kinywa
kwamba mswaki ukitumiwa baada ya miezi mitatu, basi kiafya ikiwa ni pamoja na
kuzuia madhara kama hayo ya kupukuchika kwa mswaki basi ni bora utupwe na
kununuliwa mwingine mpya.
*Ndugu msomaji ikiwa unawajali ndugu na jamaa zako, basi usisite kushare nao makala hii katika mitandao ya kijamii au hata kwa kuwaambia tu kwa njia ya mdomo.
0 Response to "JE, WAJUA MSWAKI NI HATARI WAWEZA KUKUUA?"
Post a Comment