Michirizi ya chumvi kwenye ardhi ya Sayari nyekundu ya
Mars inasadikiwa kuchorwa kwa maji yanayotiririka juu ya Sayari hiyo na ambayo
hutiririka kwa msimu. Ushahidi huo umepatikana kutoka kwa Satelaiti za Shirika
la anga la Marekani la NASA ambapo michirizi hiyo inayoonekana kwenye miinuko
inaambatana na chumvi iliyolundikana.
Habari hizi zimeripotiwa na Luju Ojha na wenzake katika
Jarida la kisayansi la Journal Nature Geoscience.
Sasa upo uwezekano wa kuwepo uhai katika sayari hiyo,
kwani uwepo wa maji yeyote yale kunaongeza uwezekano wa viumbehai vidogo vidogo
navyo kuwepo na kwa wanaanga wa siku zijazo katika sayari hiyo, ugunduzi wa maji
karibu na uso wa sayari utawafanya iwe rahisi zaidi kwao kuishi pamoja nakupunguza gharama za kuishi humo.
Kwa muda mrefu watafiti wamekuwa wakishangaa ikiwa maji
yaliyokatika hali ya kimiminika kuna wakati fulani huwa yanatiririka katika
sayari hiyo.
Siyo jambo rahisi ktokana na sababu kwamba, kwanza hali
ya joto huko ni chini ya nyuzijoto celcius sifuri na shinikizo la
anga(atmospheric pressure) ni la chini sana kiasi kwamba maji ya aina yeyote
yale yatachemka mara moja
Lakini uchunguzi uliofanyika katika kipindi cha miaka 15
kwenye makorongo na katika michirizi juu ya ardhi iayoonekana kubadilika kulingana
na misimu imeongeza tashwishi.
Bwana Luju Ojha mwanafunzi wa PHD katika taasisi ya
teknolojia ya Georgia amewakilisha data kutoka wakala wa shirika la anga; ‘Mars
Reconnaissance Orbiter’(MRO)
zinazoashiria kutegua kitendawili hicho.
MRO ina kifaa kiitwacho
Crism chenye uwezo wa kugundua kemia ya vitu vinavyounda udongo. Kilichunguza
katika maeneo manne ambapo michirizi myeusi inaonekana kuja na kuondoka katika
kipindi cha majira ya joto.
Michirizi hiyo hapo kabla
ilikuwa ikifahamika vizuri na wanasayansi na ilikuwa ikihisiwa, lakini
pasipokuwa na ushahidi kuwa ilikuwa inahusiana na maji yanayotiririka mpaka
sasa ambapo ushahidi kamili umepatikana.
Mataifa mbali mbali yakiwamo Marekani, Urusi, India, China, Uingereza na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya yamewahi kufanya majaribio kadhaa yakiwamo kutuma vyombo mbalimbali visivyokuwa na watu kwenda katika Sayari ya Mars kutafiti iwapo upo uwezekano wa kuishi viumbe hai huko pamoja na ikiwa kumewahi kuwa na maji au hata ikiwa mpaka sasa hivi yapo maji ambayo ni ishara kubwa ya kuwepo uwezekano wa kuishi viumbe hai.
Mataifa mbali mbali yakiwamo Marekani, Urusi, India, China, Uingereza na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya yamewahi kufanya majaribio kadhaa yakiwamo kutuma vyombo mbalimbali visivyokuwa na watu kwenda katika Sayari ya Mars kutafiti iwapo upo uwezekano wa kuishi viumbe hai huko pamoja na ikiwa kumewahi kuwa na maji au hata ikiwa mpaka sasa hivi yapo maji ambayo ni ishara kubwa ya kuwepo uwezekano wa kuishi viumbe hai.
0 Response to "SAYARI YA MARS KUTIRIRISHA MAJI, USHAHIDI MPYA WAPATIKANA"
Post a Comment