Ngugu msomaji wa makala hii
na mjasiriamali, hivi unayakumbuka yale mabilioni ya Kikwete aliyogawa kwa
wajasiriamali kipindi kile alipokuwa akiingia madarakani awamu yakeya kwanza?.
Ni vipi uliweza kunufaika na mabilioni hayo? Ulifanikiwa kupata japo sehemu ya
fedha hizo?. Na je ikiwa Rais mpya Dr. John Pombe Magufuli ataamua naye kutoa
fedha Mamilioni au hata Mabilioni kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake hebu
niambie, umejiandaa vipi kuyapata mapesa hayo?
Magufuli,
Kikwete na sera za kuwawezesha vijana na wanawake kwa mabilioni
|
Kama ulikuwa pengine kwa bahati mbaya hukufanikiwa kupata habari za mabilioni hayo kwani naamini kabisa kuwa, wapo watu hata hawakuwa na fununu kwamba kulikuwa na mabilioni yaliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwe kila Mkoa Tanzania Bara shilingi bilioni moja, na Tanzania visiwani shilingi milioni 6 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali hasa vijana waliokuwa katika vikundi kujikwamua na umasikini, sembuse kuambulia kuzipata pesa hizo, basi leo utapata kujua kila kitu kuhusiana na fedha hizo.
Kwa upande wangu binafsi, baada
tu ya kupata habari za ujio wa mabilioni hayo ya Kikwete kipindi hicho,
nilipata hamasa kubwa nikajua sasa mambo yangu yatanyooka na kuwa safi muda si
mrefu. Hata mkopo kutoka taasisi moja ndogo niliokuwa nafuatilia kwa ajili ya
biashara yangu ndogo, nilipunguza ‘spidi’ ya ufuatiliaji niliyokuwa nayo
nikijua sasa, naenda kupata mkopo wenye masharti nafuu. Hakukuwa na masharti
magumu kama vile, kuweka dhamana nyumba, kadi ya gari au mdhamini mwenye nyumba
nk. Ila nakumbuka sharti moja lililokuwa gumu kwa watu wengi mpaka ikafika
mahali wahusika wakaamua kuliondoa lilikuwa ni sharti la mtu kuandaa Mpango au
mchanganuo wa biashara unayotaka kwenda kuendeleza.
Sharti hili lilionekana kuwa
kikwazo kwa watu wengi baada ya karibu kila mjasiriamali aliyezihitaji pesa
zile kuanza kuzunguka huku na kule kutafuta wataalamu wanaoweza kuandika michanganuo
ya biashara. Pesa
zilikabidhiwa kwa baadhi ya mabenki ili wazigawe, ikiwemo benki ya NMB nadhani
na CRDB kama sikosei na benki zingine kadhaa. Mimi nilifunga safari mpaka benki
ya NMB pale Ilala boma nikamuuliza afisa mmoja aliyenikatisha tama kabisa.
Nilifahamishwa kuwa fedha zile
zilikuwa zimeshamalizika kitambo na walikuwa wakisubiri awamu nyingine. Cha
kushangaza mimi sikuona kama ulikuwa umepita muda mrefu tangu mchakato ule
uanze, sasa kwanini ziishe mapema kiasi kile?. Lakini jamaa mmoja niliyekutana
naye mtaani aliniambia kuwa fedha zile zilikuwa sawa na tone moja la maji
katika bahari kubwa kutokana na sababu kwamba Tanzania ni kubwa na hata kwa
mfano kikwete angesema kila raia apate mgawo basi kwa idadi yote kila mwananchi
angeliambulia wastani wa shilingi elfu moja(1000) pekee. Kwa kweli kiherehere
changu chote kiliishia pale NMB ilala, sikuja kuzifuatilia tena!
Tanzania Bara kila mkoa ulipewa
pesa kiasi cha sh. Bilioni moja wakati Tanzania visiwani wao walipewa sh.
Milioni sita(6) kwa ujumla, ukichanganya na nyingine sh.milioni 6 iliyotoa
serikali ya Mapinduzi ya Zanziba zinakuwa jula shilingi Bilioni 1.2 kwa
visiwani.
Jumla ya fedha zilizotolewa zote
ni karibu shilingi bilioni 43.7 na wajasiriamali walionufaika walikuwa
elfu 74.5 tu. Hapo ni jinsi gani unaweza kuona pesa hizi zilikuwa kidogo kiasi
ambacho ni watu wengi walihisi zilikuwa ni kiini macho kwa kutokuonekana wazi
zilikokwenda. Lakini pia kulikuwa na changamoto kubwa ya urasimu pamoja na
kutokuwajibika kwa wale waliopewa dhamana ya kuzigawa kwa wananchi.
Mfano mmoja wapo ni Rais Jakaya
mwenyewe pale alipoagiza kukutanishwa na angalao watu wawili au watatu
walionufaika na mikopo yake hiyo katika kila Wilaya ili kujiridhisha kama kweli
walikuwa wananufaika alipokuwa akifanya ziara mikoani “Nia
yangu ni kuthibitisha, “to demonstrate”, kuwa
mikopo hii inakuwa na tija” Alisema Rais Kikwete alipokuwa akiwahutubia
wananchi wa Kilombero mwaka 2008.
Kama hiyo
haikutosha, Rais Jakaya Kikwete tena hapo mwaka 2009, baada ya kuchoshwa na
malalamiko ya wananchi juu ya mabilioni yake hayo, alitaka arejeshewe fedha
zake hizo alizozitoa kwa ajili ya kuinua maendeleo ya wananchi ikiwa zilikuwa
hazijafanyiwa kazi kama ilivyokuwa imekusudiwa. Hayo aliyasema alipokuwa
akitembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara(BET) ya 33.
"Fedha
hizo ni zangu kama mmeshindwa kuzizungusha kwa wananchi naomba mzirudishe kwa
kuwa nilizitoa kwa nia ya kuwasaidia wananchi wangu ili waweze kukabiliana na
hali ngumu ya maisha," Alisema Rais
Kikwete na kuongeza kwamba madhumuni ya kutoa
fedha hizo yalikuwa ni kuwasaidia wananchi wake pamoja na kuleta tija kwa
maendeleo ya nchi na wala siyo watu wachache jambo ambalo limekwenda kinyume na
utaratibu.
Inasemekana
mpaka Kikwete anaondoka madarakani fedha hizi bado nyingine zilikuwa
hazijagawiwa kwa wananchi, hata hivyo pia wananchi wenyewe kwa upande wao,
hawakupenda kuzirejesha pesa hizo, mfano ni pale mwanzoni mwa mwaka huu Wabunge
walipohoji juu ya fedha hizo na serikali kujibu kuwa, baadhi hazijagawiwa na
waliogawiwa wengi hawajazirudisha na idara ya ukaguzi wa ndani ina mpango wa
kufanya ukaguzi kujua ni kina nani waliokopeshwa ili ichukue hatua stahiki.
Mimi binafsi
katika uchunguzi wangu mtaani, nilifanikiwa kuzungumza na kijana mmoja
aliyechukua mkopo akiwa Wilayani Kibaha, anajitapa kuwa hakuna hela aliyoifaidi
kama ile ya Mabilioni ya JK kwani hakuona umuhimu wa kuzirejesha; kwanza
kutokana na kuwa zilitolewa na serikali, pili anasema hata watu wa benki
wenyewe hawajawa na msukumo wa kuzifuatilia kama ilivyokuwa kwa fedha zingine.
Kwingineko anasema hata maafisa wenyewe wa benki huwahamasisha waliochukua
mikopo hiyo kutokurudisha kwa maslahi wanayoyajua wao wenyewe.
Ikiwa hali
yenyewe ndiyo hiyo basi, Ujio mwingine wa Mabilioni ya Dr. Magufuli,
Mjasiriamali Umejipanga vipi?
Hakuna
ajuaye ikiwa Rais mpya Dr. John Pombe Magufuli atakuja na sera gani juu ya
kuwawezesha wafanyibiashara wadogowadogo hususani vikundi vya akina mama na
vijana, lakini ni lazima atakuwa na mpango wake. Hata kama hatakuja na
utaratibu mpya lakini kama tulivyoona katika makala haya bado yale mabilioni
aliyotoa Kikwete mengine hayajagawiwa.
Usisubiri
mpaka usikie wanaanza kugawa ndipo uanze kukimbia kimbia kutafuta wataalamu wa
kukuandikia mpango wa biashara kama wengi walivyofanya kipindi cha JK.
Naandika
kama utani vile, lakini ndugu yangu baadaye haya yanaweza yakaja kuwa na maana.
Hebu tu, hata pasipo kuwa na mawazo ya mabilioni ya Magufuli kichwani, tafakari
na kujiuliza ikiwa utapata mtaji labda kuanzia milioni kadhaa( ) kutoka
mahali popote pale, mpango wako ni nini?, utafanya biashara gani?. Jaribu
kutengeneza picha ya mchanganuo kichwani mwako ni jinsi gani utakavyozitumia
fedha hizo kujikwamua na umasikini.
Hapa
namaanisha kuwa muda wote kuwa “updated” kuhusiana na maswala yahusuyo pesa,
kuwa na elimu sahihi juu ya fedha, haikuhitaji wewe kukaa darasani tena, kwani
siyo lazima.
Unaweza
ukapata ufahamu huo kwa njia mbalimbali mbadala na moja wapo ni kama hivi
unavyosoma kupitia blogu hii. Njia nyingine ni semina na makongamano mbalimbali, na
vilevile unaweza ukasoma vitabu mbalimbali na napendekeza ikiwa utahitaji
vitabu basi usikose vitabu kutoka kampuni ya "SELF HELP BOOKS TANZANIA
LIMITED", wana vitabu vizuri, mfano ni kitabu kilichobeba kila kozi ya
ujasiriamali ndani yake na kwa ubora wa hali ya juu, yaani ni kila kitu ndani
ya kitabu kimoja, “JIFUNZE UJASIRIAMALI NA MICHANGANUO YA
BIASHARA” hautajutia pesa
yako kamwe.
Wana kitabu
pia “online book” ambacho unaweza kukinunua hata dakika
hii hii unaposoma hapa, “Miferejiya Pesa”. Cha kufanya tu ni
kwambba, unatuma sh. 3,000/- kwenye namba hizi, 0712 202244 au 0765 553030
pamoja na meseji yenye anuani ya barua pepe yako(e-mail address). Na kisha
unapakua(Unadownload) kitabu chako chini ya dakika 5.
Kumbuka
ndugu msomaji wangu, dunia tunakoelekea sasa, unahitaji kila kitu kufanya
katika mtizamo wa kibiashara, na zaidi ya hapo kijasiriamali zaidi, mathalani
unafanya muziki, huwezi tena kufanya katika ule mtizamo waliokuwa nao
wanamuziki enzi zile za kina NUTA jazz na Sikinde, bali itakubidi uende
sambamba na akina AY, Ali Kiba, Diamond, Lady JD na wengineo, kwa kuwa na
mameneja(menejimenti), timu inayolipwa mishahara kukamilisha majukumu
mbalimbali ya kampuni pamoja na promosheni au kujitangaza kwa njia mbalimbali
ikiwemo mitandao ya kijamii na katika ‘level’ za kimataifa.
Tuseme pia
unafanya kilimo, siyo tena kama kile cha kutegemea jembe la mkono kwa ajili ya kujikimu chakula cha
familia tu, bali kilimo cha kisasa kinachohusisha mashine kama matrekta na
maksai, mbegu bora, umwagiliaji, kuongeza thamani katika mazao unayovuna na
hatimaye soko la uhakika.
Yoote haya
unahitaji maarifa ya kifedha, ufahamu wa maswala ya msingi kabisa kama vile,
faida na hasara, mzunguko wa fedha taslimu "cash
flow" , mipango ya biashara, hisa, mitaji, mizania katika
biashara, kutafuta masoko nk. Na utavijuaje vitu hivyo?, Ni kwa njia ya
kujifunza peke yake na wala siyo vinginevyo.
Asante sana
kwa kusoma makala hii na uendelee kubarikiwa.
0 Response to "UJIO WA MABILIONI YA MAGUFULI: MJASIRIAMALI UMEJIANDAAJE?"
Post a Comment