Mteja wetu mmoja wa Tabora mjini kwa kifupi
anaitwa Bwana Abdalla D. jana alinipigia simu akihitaji kutumiwa vitabu viwili
yaani, kitabu cha “Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali” na
kitabu cha “Siri ya Mafanikio biashara ya Rejareja”. Nilimpa njia mbili, ya kwanza ni, ikiwa anaye mtu
yeyote anayefanya safari za Tabora Dar amuagize amchukulie, au njia ya pili na
ambayo ndiyo huwa wateja wetu wengi wa Mikoani tunawatumia ya kutuma kwa Mabasi
yanayokwenda mikoani
Yeye alichagua njia ya pili ya mabasi, nikamwambia mara nyingi kwa mikoa ya mbali mabasi huchaji mpaka shilingi elfu kumi, 10,000/= kwa hiyo pamoja na gharama za vitabu ambazo ni shilingi elfu 20 na shilingi elfu 10 jumla atume shilingi elfu 40.
Abdala leo mchana alituma pesa na mhudumu wetu akapanda
basi mara moja kuelekea Magomeni Mapipa ziliko ofisi za mabasi ya N.B.S Company
ltd, wamiliki wa mabasi yanayokwenda
Tabora. Alipouliza bei ya kutuma ile bahasha yenye vitabu aliambiwa ni
shilingi elfu tano tu!.
Kumbe haya makampuni ya mabasi huwa na bei tofauti za
utumaji wa vifurushi, vile vile gharama hutofautiana kulingana na umbali wa
mahali, ukubwa wa kifurushi na aina ya mzigo wenyewe.
Soma pia: kitendawili cha mteja wetu wa Manzese.
Basi tulichokifanya, ni kumpigia simu mteja na kumjulisha
kwamba gharama ya kutuma vile vitabu ni shilingi elfu tano, kwahiyo
tukamrudishia shilingi zake elfu tano kupitia simu yake ya mkononi.
Tunapenda pia kuchukua fursa hii kuwajulisha wateja wetu
popote pale walipo wanapohitaji vitabu vyetu, wasisite kuagiza wakihofia
kupoteza pesa zao, vitabu vitawafikia salama wasalimini na endapo itatokea
hitilafu yeyote ile kwa bahati mbaya(na haijawahikutokea bado) ni sisi SELF HELP BOOKS CO. LTD wenyewe tutakaowajibika,
unarudishiwa fedha yako yote au kutumiwa kitabu kingine haraka.
0 Response to "GHARAMA ZA KUTUMA VITABU VYA UJASIRIAMALI MIKOANI (SELF HELP BOOKS)"
Post a Comment