MWANDISHI WA HADITHI MASHUHURI ZAIDI MAREKANI AFA NA MIAKA 89 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MWANDISHI WA HADITHI MASHUHURI ZAIDI MAREKANI AFA NA MIAKA 89


Harper Lee, aliyeandika kitabu maarufu juu ya Ubaguzi wa rangi nchini Marekani  cha “How To Kill a Mockingbirdamefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 89. Kitabu kilikuwa kinamsimulia wakili mweupe aliyekuwa akimtetea mahakamani mwanamume mweusi aliyekuwa akituhumiwa kwa kesi ya ubakaji katika jimbo la “Deep South”.
Mwandishi maarufu nchini Marekani,Harper Lee. 
Aliuza nakala za kitabu hicho zipatazo milioni 40, duniani kote na kufanikiwa kupewa tuzo ya Pultzer katika riwaya mwaka 1961. Mmiaka 55 baadaye yaani mwaka jana 2015 alitoa kitabu kingine kama matokeo ya hicho cha kwanza, “Go set Watchman”.

Mwandishi huyo mzaliwa wa Alabama anasifika sana kwa tabia yake ya kipekee ya kutopenda kabisa kuhojiwa na vyombo vya habari wala kupenda umaarufu ingawa alikuwa mtu maarufu sana na aliyeheshimika katika jamii yake Marekani na Dunia kwa ujumla. 

Aliwahi kupewa tuzo na Rais wa zamani wa Marekani, George W.Bush iitwayo “Presidential Medal of Freedom” mwka 2007 na baada ya kifo hiki Bush ametoa salamu za rambirambi akisema mama huyo alikuwa ni mwenye upendo na  mwanafasihi wa kukumbukwa.


"How to kill Mocking bird" kimewahi kuigizwa kama sinema na kutumiwa mashuleni kujibia mitihani ya fasihi jambo linalofanyika mpaka sasa hivi. Ni moja ya vitabu ambavyo watu wengi hawatavisahau maisha yao yote vizazi kwa vizazi.

CHANZO: BBC

0 Response to "MWANDISHI WA HADITHI MASHUHURI ZAIDI MAREKANI AFA NA MIAKA 89"

Post a Comment