Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa vipindi wa
kampuni ya Clouds Media inayomiliki vituo cha redio na Televisheni vya Clouds fm
na Clouds Tv, Bwana Ruge Mutahaba alitangaza kuzitaja fursa kumi (10) za
kibiashara na kiuchumi zinazopatikana hapa Tanzania. Alizitaja fursa hizo 10
ndani ya kipindi maarufu cha Power Breakfast na pia kupitia TV, Kwenye kipindi
cha Clouds360.
Akizitaja fursa hizo muhimu za kibiashara
alisema kwamba, mtu anachopaswa kufanya kwanza ni kuzisikiliza fursa kumi, na
pili ni sharti ajitambue yeye binafsi. Akitolea mfano, alimtaja Nyota Ndogo,
msanii wa muziki wa kizazi kipya kwamba kama asingelitambua kipaji chake kwanza
kuwa yeye ni mwanamuziki, kamwe asingeliweza kufikia hatua aliyofikia sasa.
Aliongeza kuwa wengi tunashindwa kujitambua,
kushindwa kufahamu nguvu tulizokuwa nazo, “Ninaamini kila mtu anacho
kipaji(talanta) ambayo amezaliwa nayo”. Alisema Ruge Mutahaba, “Mwingine
anaweza kuwa mchoraji mzuri lakini hajawahi kufikiria kuwa ni ‘designer’ mzuri
kwani hakuna mtu aliyemsaidia kumuonyesha anafanyaje vitu, hivi vitu ni
kujaribu, kujifunza, kujitathmini na kujifahamu” aliongeza Ruge Mutahaba.
Akitolea mfano mwingine wa madalali, Ruge
aliuliza kuwa ni madalali wangapi wanaotumia mtandao wa ‘Instagram’ katika
biashara zao, zaidi tu ya kuwa na ‘contact’ za kawaida za simu?.
Mwisho alianza sasa kuzitaja fursa zenyewe 10
nazo ni kama ifuatavyo:-
1. FURSA
KATIKA SEKTA YA KILIMO.
Alisema
kuwa kilimo ndio msingi wa shughuli nyingine zote lakini Watanzania hulima si
kwa lengo la kufanya kilimo cha kibiashara, bali kujikimu na njaa. Hivyo
alisema hali hiyo inatoa mwanya kwa mtu yeyote anayependa kufanya kilimo cha
kibiashara kuwa na fursa kubwa ya kutoka kiuchumi. Aidha alisema
kilimohuchochea viwanda na mwishowe ongezeko la ajira katika nchi.
2.
BIASHARA YA CHAKULA (FOOD PROCESSING)
Ruge
Mutahaba fursa hii katika tasnia ya chakula anaitazama kwa jicho la kuongeza
thamani “value added”, matangazo na ubunifu. Alihimiza watu wasiishie
tu kupika kwa mazoea bali pia waongeze ubunifu kwa kwa kuibuka na vitu(njia)
mpya tofauti tofauti kusudi waweze kuongeza tija zaidi.
3. BIASHARAYA REJAREJA MITANDAONI “RETAIL E-COMMERCE”
Alisema
biashara hii mtu anaweza kuifanya, aidha anaponunua ama kuuza bidhaa/huduma
kupitia mtandao wa intaneti, “Huna haja ya kuonana na wateja ana kwa ana, na
unaweza ukauza bidhaa za kila aina kuanzia, nguo, viatu nk.
4. SEKTA YA HABARI NA BURUDANI.
“Tukiweza
kutengeneza filamu nzuri tunaweza
kufika mbali” Alitolea mfano wa Wanaigeria ambao alisema waliweza kutengeneza
filamu moja nchini Marekani na ikaweza kufikisha mauzo ya nakala laki tano(500,000)
katika kipindi cha mwezi mmoja pekee.
5. BIASHARA KATIKA TASNIA YA HUDUMA ZA KIJAMII.
Alitoa
mifano ya Mahospitali na mashule mengi ya watu binafsi, jinsi zinavyofanya
vyema na kusema, hiyo ni fursa nzuri ya watu wengi zaidi kuanza kuwekeza huko.
6.
SEKTA ZA MITINDO NA UREMBO.
Alisema
hapo zamani ili mtu aonekane kuwa ni mrembo na mwenye mvuto alihitaji kuzaliwa
nao lakini kwa sasa hivi, urembo wa mtu ni “featuring” ya mambo mbalimbalikuanzia, nywele, kucha mek up nk. Kuna fursa nyingi, mfano mmoja tu, kufanya ‘Pedicure
na Manicure’ ni shilingi elfu arobaini (40,000) na hicho ni kitu kimoja tu
katika urembo” alisisitiza Ruge Mutahaba.
SEKTA
YA VIWANJA, MASHAMBA NA MAJENGO “REAL ESTATE”
Alitaja
pia ongezeko la mashule na vyuo kama fursa ya Watanzania kuwekeza katika ujenzi
wa hosteli na majengo yatakayotoa huduma
kwa wanafunzi, biashara ambayo ni ya kudumu.
8.
TASNIA YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI.
Fursa
nyingine aliyotaja kuwa ni miongoni mwa fursa za kibiashara na uchumi
zinazokuwa kwa kasi na ambazo Watanzania wanaweza kunufaika nazo ni hii ya
usafirishaji wa abiria, mizigo na usambazaji wa bidhaa na huduma za aina
mbalimbali.
Akitoa
mfano wa ununuzi na uuzaji wa Hisa, alisema kwa sasa masuala ya hisa, uelewa
umekuwa ni mkubwa miongoni mwa Watanzania na ni fursa nzuri sasa kwa vijana
kuwekeza katika hilo.
Alisema
karibia kila jambo siku hizi huhusisha matumizi ya mtandao wa intaneti kama
kufanya biashara na hivyo alisema ni
fursa nzuri kwetu kuanza kuwekeza na kujiajiri.
0 Response to "UTOKE VIPI KIMAISHA? RUGE ANAKUPA FURSA MUHIMU 10 HIZI HAPA"
Post a Comment