Ni tofauti
gani ubunifu wa majengo unaweza kuleta? Mbunifu wa majengo anaweza
akawashawishi watu kufikiria tofauti? Na pengine kuwa na tabia tofauti?
Maswali hayo
na mengineyo yanajibiwa na Mhandisi/Mbunifu wa Majengo anayehitajiwa sana
sehemu nyingi duniani, David Adjaye raia wa Uingereza mwenye asili ya Ghana
lakini aliyezaliwa jijini Dar es salaam.
David Adjaye
alikuwa akifanya mahojiano na kipindi cha “Hard
Talk” kinachorushwa hewani na redio ya BBC, akielezea miradi “project”
mbalimbali alizowahi na anazoendelea kuzifanya ukiwemo mradi maarufu zaidi na
utakamuacha akikumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo, mradi wa jengo la Utamaduni
la Kihistoria kati ya Afrika na Amerika lijulikanalo kama; “Smithsonia Natioal Museum of
Africa America History and Culture” na ambalo linatarajiwa kufunguliwa
rasmi hapo Septemba mwaka huu.
Moja ya majengo makubwa aliyobuni David
Adjaye.
|
Adjaye pia
amewahi kudizaini majengo maarufu maeneo mbalimbali kote duniani yakiwamo, jengo
la kituo cha Amani cha Nobel huko Oslo Norway-“Nobel Peace Centre”, jengo la
Maktaba la ‘White Chapel’ huko London Uingereza, jengo lenye dhamani ya Paundi
milioni £160 huko Moscow Urusi lijulikanalo kama; Moscow School of Management
Skolkovo(2010), Vituo vya biashara shopping centres Beirut na Lagos, Jengo la
hospitali ya watoto nchini Rwanda na Mradi wa nyumba za kuishi watu jijini New
York.
Na sasa
kampuni yake ya Adjaye Associates ni
miongoni mwa makampuni mengine 6 yaliyochaguliwa kushindania nafasi ya kupewa
tenda ya kudizaini jengo la maktaba itakayokuwa kumbukumbu ya Urais wa Barack
Obama na mkewe Michelle. Jengo hilo linatarajiwa kujengwa huko ‘Chicago, South
Side’, eneo lenye historia kubwa kwa Wamarekani weusi.
Adjaye anapewa
nafasi kubwa ya kushinda tenda hiyo, siyo kwa sababu ya weusi wake au uasili
wake wa Afrika, la hasha bali ni kutokana na kazi yake inayokubalika kimataifa.
Yeye binafsi katika mahojiano yake na Shirika la utangazaji la BBC, alisema
hivi’
“Nina bahati sana kuchaguliwa miongoni mwa hao
saba, huhitaji kuwa Mmarekani ili kuweza kubuni jengo hilo, ubunifu wa majengo
ni lugha ya kimataifa ya ustaarabu na ubinadamu wetu, tupo wageni watatu kwenye
hilo, mtu yeyote aliye na kipaji anaweza akalidizaini”
Alliulizwa pia
kuhusiana na wakosoaji wake aliokuwa wakikosoa jengo la London la whitechapel
na wengine jengo la makaazi ya watu jijini New York wakidai rangi haikuwa
nzuri. Alijibu hivi;
“Wakosoaji wanaruhusiwa kusema chochote na
sheria ya soko haisemi eti kila wakati umfurahishe kila mtu na hasa wakosoaji.
Ninaowasikiliza ni wakaazi wa pale na ndio waliochagua rangi ya jengo”
Zifuatazo hapa
chini ni nukuu “quotes” mbalimbali maarufu alizowahi kuzitoa David Adjaye;
“Buildings can transform. They can change
places. They can change the perception of places.” -David Adjaye.
For me at the beginning of a project, the best
is to have an opportunity to just listen”-David Adjaye.
“The best buildings emerge from a deep
collaboration with the client”-David Adjaye.
David Adjaye ni
mbunifu wa majengo anayeheshimika sana duniani katia kizazi chake, amewahi
kupewa moja ya heshima ya juu kabisa anayopewa raia nchni Uingereza iitwayo OBE “Officer of the Most Excellent Order of the
British Empire”
Alifunga pingu
za maisha na mshauri wa biashara ya mitindo, Ashley
Shaw-Scott hapo mwaka 2014
David Adjaye akiwa na mkewe Ashley Shaw-Scott
siku ya harusi yao.
|
Vyanzo vya
habari hii ni kutoka katika mitandao ya;
0 Response to "DAVID ADJAYE MBUNIFU MAJENGO MZALIWA WA TANZANIA ANAYEHITAJIWA ZAIDI DUNIANI "
Post a Comment