DAVID ADJAYE MBUNIFU MAJENGO MZALIWA WA TANZANIA ANAYEHITAJIWA ZAIDI DUNIANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DAVID ADJAYE MBUNIFU MAJENGO MZALIWA WA TANZANIA ANAYEHITAJIWA ZAIDI DUNIANI

Ni tofauti gani ubunifu wa majengo unaweza kuleta? Mbunifu wa majengo anaweza akawashawishi watu kufikiria tofauti? Na pengine kuwa na tabia tofauti?


Maswali hayo na mengineyo yanajibiwa na Mhandisi/Mbunifu wa Majengo anayehitajiwa sana sehemu nyingi duniani, David Adjaye raia wa Uingereza mwenye asili ya Ghana lakini aliyezaliwa jijini Dar es salaam.


David Adjaye alikuwa akifanya mahojiano na kipindi cha “Hard Talk” kinachorushwa hewani na redio ya BBC, akielezea miradi “project” mbalimbali alizowahi na anazoendelea kuzifanya ukiwemo mradi maarufu zaidi na utakamuacha akikumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo, mradi wa jengo la Utamaduni la Kihistoria kati ya Afrika na Amerika lijulikanalo kama; “Smithsonia Natioal Museum of Africa America History and Culture” na ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi hapo Septemba mwaka huu.
Moja ya majengo makubwa aliyobuni David Adjaye.
Adjaye pia amewahi kudizaini majengo maarufu maeneo mbalimbali kote duniani yakiwamo, jengo la kituo cha Amani cha Nobel huko Oslo Norway-“Nobel Peace Centre”, jengo la Maktaba la ‘White Chapel’ huko London Uingereza, jengo lenye dhamani ya Paundi milioni £160 huko Moscow Urusi lijulikanalo kama; Moscow School of Management Skolkovo(2010), Vituo vya biashara shopping centres Beirut na Lagos, Jengo la hospitali ya watoto nchini Rwanda na Mradi wa nyumba za kuishi watu jijini New York.


Na sasa kampuni yake ya Adjaye Associates ni miongoni mwa makampuni mengine 6 yaliyochaguliwa kushindania nafasi ya kupewa tenda ya kudizaini jengo la maktaba itakayokuwa kumbukumbu ya Urais wa Barack Obama na mkewe Michelle. Jengo hilo linatarajiwa kujengwa huko ‘Chicago, South Side’, eneo lenye historia kubwa kwa Wamarekani weusi.

Adjaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda tenda hiyo, siyo kwa sababu ya weusi wake au uasili wake wa Afrika, la hasha bali ni kutokana na kazi yake inayokubalika kimataifa. Yeye binafsi katika mahojiano yake na Shirika la utangazaji la BBC, alisema hivi’

“Nina bahati sana kuchaguliwa miongoni mwa hao saba, huhitaji kuwa Mmarekani ili kuweza kubuni jengo hilo, ubunifu wa majengo ni lugha ya kimataifa ya ustaarabu na ubinadamu wetu, tupo wageni watatu kwenye hilo, mtu yeyote aliye na kipaji anaweza akalidizaini”

Alliulizwa pia kuhusiana na wakosoaji wake aliokuwa wakikosoa jengo la London la whitechapel na wengine jengo la makaazi ya watu jijini New York wakidai rangi haikuwa nzuri. Alijibu hivi;

“Wakosoaji wanaruhusiwa kusema chochote na sheria ya soko haisemi eti kila wakati umfurahishe kila mtu na hasa wakosoaji. Ninaowasikiliza ni wakaazi wa pale na ndio waliochagua rangi ya jengo”

Zifuatazo hapa chini ni nukuu “quotes” mbalimbali maarufu alizowahi kuzitoa David Adjaye;

“Buildings can transform. They can change places. They can change the perception of places.”-David Adjaye.

For me at the beginning of a project, the best is to have an opportunity to just listen”-David Adjaye.

“The best buildings emerge from a deep collaboration with the client”-David Adjaye.

David Adjaye ni mbunifu wa majengo anayeheshimika sana duniani katia kizazi chake, amewahi kupewa moja ya heshima ya juu kabisa anayopewa raia nchni Uingereza iitwayo OBE Officer of the Most Excellent Order of the British Empire

Alifunga pingu za maisha na mshauri wa biashara ya mitindoAshley Shaw-Scott hapo mwaka 2014

David Adjaye akiwa na mkewe Ashley Shaw-Scott siku ya harusi yao.


Vyanzo vya habari hii ni kutoka katika mitandao ya;

0 Response to "DAVID ADJAYE MBUNIFU MAJENGO MZALIWA WA TANZANIA ANAYEHITAJIWA ZAIDI DUNIANI "

Post a Comment