KUPANGA MIPANGO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NCHI TAJIRI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUPANGA MIPANGO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NCHI TAJIRI

Unajua ni kwa nini Mataifa makubwa kama Marekani na China hufanikiwa sana kiuchumi na katika suala zima la maendeleo ya nchi na watu wao? Ni jambo gani hulifanya tofauti na nchi zingine linalowafanya waweze kupata maendeleo hayo kwa kiasi hicho? Nimezitaja nchi hizo mbili kwa makusudi kutokana na habari zilizoshika chati hivi leo katika vyombo mbalimbali vya habari Duniani.



Habari hizo zote mbili zinahusiana na upangaji wa mipango na kuweka mikakati na malengo ya kufikia jambo fulani. Tukianza na Marekani, kuna habari inayohusiana na mgogoro wa nchi ya Libya ambapo Rais Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba yeye na serikali yake walishindwa kupanga mpango mahsusi wa namna Taifa la Libya litakavyoendeshwa baada ya kumalizika kwa vita ya kumng’oa Kanal Muammar Gaddafi.

Obama aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na TV ya Fox kuhusiana na kufanikiwa na kutofanikiwa katika utawala wake. Kumbe ilikuwa ni MIPANGO tu ndiyo sababu ya Libya mpaka leo hii mambo yanakwenda kama yalivyo.

Wakati hayo yakijiri kwa upande wa Taifa hilo kubwa na tajiri zaidi Duniani, pia katika Taifa jingine linalochipukia kimaendeleo kwa kasi ya ajabu kutaka kuipiku Marekani kwa utajiri na hata ikiwezekana katika kila Nyanja, Uchina nayo tofauti na Marekani, imeamua kuanza kuweka MIPANGO mapema ili baadaye hapo mwaka 2050 isijekujutia azma yake ya kutaka kuwa Taifa kubwa kimichezo na hususani katika Soka au maarufu kama Kandanda. Wachina hawataki kuja kujilaumu kwamba ni nini kilichowazuia kufikia ndoto yao hiyo kwa kuanza mapema kufanya kitu kinachoitwa “MIPANGO”

Mpango China inaouandaa umebeba mkakati kabambe wa kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2050, China inakuwa Taifa linaloongoza Duniani katika Soka, na mwaka 2020 watoto milioni 50 pamoja na watu wazima wanacheza mchezo huo mashuhuri Duniani. Malengo mengine ndani ya Mpango huo ni kuwa na angalao vituo vya kufundishia mpira wa miguu vipatavyo 20,000 pamoja na viwanja “pitches” vipatavyo 70,000 ifikapo mwaka huo wa 2020.

Mpango huo unatiwa nguvu na Rais wao Xi Jinping ambaye ni mpenzi mkubwa wa soka na ambaye aliwahi kutamka wazi kwamba anataka China kushinda kombe la Dunia miaka 15 kuanzia sasa. Imeweka malengo ya muda mfupi na mrefu yakiwamo kuhakikisha kunakuwa na kiwanja kimoja cha mpira katika kila watu 10,000 ifikapo mwaka 2030, mpango huo umeeleza.

HITIMISHO
Mipango na malengo ni kama watoto mapacha, huwezi ukawa na mpango pasipokuwa na malengo. Sasa Je,  na wewe Mjasiriamali umeandaa mpango wa Biashara yako?, umeweka malengo na mikakati  itakayokuwezesha kuifikia ndoto yako? 
Libya baada ya vita.
Angalia usije ukawa kama Marekani kule Libya ukaja kujuta kama alivyofanya Obama leo, Na wewe anza kuweka mpango wa biashara yako, siyo biashara tu, jambo lolote lile hata ikiwa ni masomo, ajira au hata kipaji kama uanamuziki na filamu, Panga mipango, weka malengo, yatekeleze na mwisho wa siku fikia ndoto zako.



Kama utahitaji muongozo ni kwa namna gani unaweza  ukaandaa mpango wa biashara yako mpya au hata  uliyokwisha kuianza kitambo kwa ajili ya kuihuisha upya, basi Self Help Books ltd ndiyo suluhisho lako, Tuna kitabu kizuri ambacho baada ya kujifunza kila hatua ya uandaaji mpango, unapata na mipango ya biashara yenyewe halisi ambayo unaweza pia ukaifanya kama kielelezo wakati ukiandaa mpango wako mwenyewe, au hata unaweza tu ukaipitia michanganuo hiyo kwa ajili ya kukufanya uweze kuelewa vipengele mbalimbali katika uanzishaji, na uendelezaji wa biashara kwa mapana na marefu.

0 Response to "KUPANGA MIPANGO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NCHI TAJIRI"

Post a Comment