SURA
YA 3
IMANI:
Kuona
na Kuamini Katika kufikia Shauku
(Hatua
ya pili Kuelekea utajiri)
Imani ndiyo mkemia mkuu wa akili. Imani inapochanganywa
na msisimko(mtetemo) wa fikra, akili ya ndani mara moja huuchukua msisimko, na
kuutafsiri kuwa katika kipimo cha imani na kuusafirisha kwenda kwa nguvu kuu
isiyokuwa ya kawaida sawa kama ilivyo kwenye suala la sala.
Imani,
mapenzi(upendo) na ngono(kujamiiana) ndiyo vitu vyenye nguvu
zaidi kushinda mihemko yote mikubwa. Vitu hivi vitatu vinapochanganywa, vina
athari ya ‘kugeuza’ mtetemeko wa fikra kuwa katika namna ambayo huweza kufika
mara moja kwenye akili ya ndani ambapo hugeuzwa kuwa katika mfumo wa
kiimani(kiroho), mfumo ambao ndiyo pekee wenye uwezo wa kuwasiliana na Nguvu
kuu(Mungu).
Mapenzi(upendo) na Imani ni vitu vya kiakili(nafsi),
huhusika na upande wetu wa kiroho. Ngono(kujamiiana) ni tendo la kibaiolojia
zaidi, na huhusiana tu na vitu vya nje vinavyoonekana. Mchanganyiko wa mihemko
hii mitatu una athari za kufungua moja kwa moja mstari wa mawasiliano baina ya
akili ya kawaida ya kufikiria na ule uwezo usiokuwa wa kawaida(Nguvu kuu)
Jinsi
ya Kujenga Imani.
Imani ni hali ya akili ambayo inaweza ikaambukizwa au
kutengenezwa kupitia kukiri au maelekezo yanayojirudia kwenye akili ya ndani
kwa kupitia kanuni za kujishauri binafsi. Kama kielelezo angalia nia yako kwa
mfano ya kukisoma kitabu hiki. Kimsingi lengo ni kupata uwezo wa kugeuza
mawimbi ya fikra yasiyoshikika ya shauku
kuwa kitu(mwenzake) kinachoshikika kama Pesa.
Kwa kufuata maelekezo yaliyoorodheshwa kwenye sura ya 3
juu ya Kujishauri na Sura ya 11 juu ya Akili ya ndani, unaweza ukaishawishi akili ya ndani kwamba
unaamini utapokea kile ulichokiomba. Itaifanyia kazi imani hiyo na kuirudisha
tena kwako katika mfumo wa imani, ikifuatiwa na mipango kamili ya kulifikia
lengo lako.
Njia ambayo mtu huitumia kujenga Imani, ambapo haikuwepo hapo kabla ni ngumu sana kuielezea. Kwa
kweli ni ngumu karibu sawa na ambavyo huwa ngumu kumuelezea kipofu jinsi rangi
nyekundu ilivyo. Imani ni hali ya akili ambayo unaweza ukaijenga kwa hiyari
yako mwenyewe baada ya kuwa umeshazifahamu vilivyo hatua 13 kuelekea utajiri
ndani ya hiki kitabu.
Kurudiarudia kuiambia kwa dhati akili yako ya ndani ndiyo
njia pekee inayojulikana ya kujenga hisia kubwa za imani kwa hiyari. Pengine
maana yake inaweza ikawa wazi zaidi kupitia maelezo yafuatayo ya namna watu
wakati mwingine wanavyogeuka kuwa wahalifu.
Yalielezwa katika maneno ya mtaalamu mashuhuri wa mambo
ya uhalifu kwamba; “Mara ya kwamza watu wanapokuwa karibu na maswala ya uhalifu
huwa wanachukizwa nao, Ikiwa wataendelea kwa muda kuwa nao karibu, huuzowea na
kuuvumilia. Ikiwa wataendelea kuushuhudia kwa kipindi kirefu zaidi, mwishowe
huukumbatia kwa moyo na kushawishika nao.”
Hii ni sawa na kusema kwamba, msukumo wowote wa fikra unapopitishwa
kwenye akili ya ndani mara kwa mara, mwisho wake hukubalika na kufanyiwa kazi.
Akili ya ndani huendelea kutafsiri msukumo huo kwenda kwenye kitu
kinachoshikika chenye ukubwa sawa na msukumo huo kupitia njia za kivitendo
zaidi zilizokuwepo.
Sambamba na hilo zingatia tena kauli hii, MAWAZO YOTE
YALIYOPEWA HISIA KALI NA KUCHANGANYWA NA IMANI, huanza mara moja kujitafsiri
yenyewe kuwa kitu halisi kinachoshikika na kinacholingana nayo.
Mihemko au “hisia” sehemu ya fikra, ni vigezo vinavyoyapa
mawazo(fikra) uhai, maisha na vitendo.
Mihemko ya imani, mapenzi na ngono, inapochanganywa na msukumo mwingine wowote
ule wa fikra, huipa uwezo mkubwa zaidi kushinda vile ambavyo mhemko mmoja mmoja
ungeweza kuwa ukiwa peke yake. Siyo tu misukumo ya fikra iliyochanganywa na Imani, lakini pia ile ambayo
iliyochanganywa na mihemko chanya yeyote ile au mihemko hasi yeyote ile-
inaweza ikaifikia na kuiathiri akili ya ndani.
Kutokana na kauli hii, utatambua kuwa akili ya ndani
itatafsiri msukumo wa fikra wenye asili hasi au ya kubomoa kwenda katika kitu
kinachoshikika, sawasawa kama vile itakavyotenda kwa msukumo wa fikra wenye
asili chanya au ya kujenga. Hii ndiyo sababu ya hali isiyokuwa ya kawaida, ya
mamilioni ya watu kukumbwa na kile kinachotajwa kama, “Bahati mbaya” au “Mkosi”
Mamilioni ya watu huamini
wenyewe “kuangamizwa” kwenye umasikini na maanguko, kutokana na nguvu za ajabu
ambazo huamini hawawezi kuzidhibiti. Wao ndio waumbaji wa “Mikosi” yao wenyewe
kutokana na hii imani hasi, ambayo huchukuliwa
na akili ya ndani na kutafsiriwa kuwa katika kitu halisi kinacholingana nayo.
Hapa ni mahali muafaka pa kupendekeza tena kwamba,
unaweza ukanufaika kwa kuingiza katika akili yako ya ndani Shauku yeyote ambayo unatamani kuitafsiri kuwa katika kitu halisi,
au kiasi cha fedha, katika hali ya matamanio au imani kwamba badiliko kweli linatokea.
Imani
yako au Itikadi ni kiungo kinachoamua
kitendo cha akili yako ya ndani. Hamna kitu kitakachokuzuia “kuidanganya” akili
yako ya ndani wakati unapoipa maelekezo kupitia, kujishauri binafsi, kama
nilivyoidanganya akili ya ndani ya kijana wangu. Kuufanya “uwongo” kuwa kweli
zaidi, jifanye mwenyewe tu kama vile ambavyo ungekuwa ikiwa UNGELIKUWA TAYARI
UNAMILIKI KITU UNACHOKITAKA unapokuwa ukiwasiliana na akili yako ya ndani.
Akili ya ndani itageuza kuwa kitu halisi kinacholingana, kwa kutumia njia za
moja kwa moja zaidi na za kivitendo
zilizokuwepo, maelekezo yeyote itakayopewa yakiwa katika hali ya imani au itikadi ni kwamba yatatekelezwa.
Ukweli mengi yameelezwa kutoa mahali pa kuanzia ambapo
mtu anaweza, kwa kupitia mazoezi na vitendo, kupata uwezo wa kuchanganya imani pamoja na maelekezo mengine yeyote
yanayotolewa kwa akili ya ndani. Ukamilifu utakuja kwa kupitia kufanya mazoezi
ya vitendo. Hauwezi ukaja tu hivihivi kwa njia ya kusoma maelekezo.
Ikiwa ni kweli kuwa mtu anaweza akawa mhalifu kwa kuishi
miongoni mwa uhalifu (na huu ni ukweli unaofahamika), ni ukweli sawa na huo
kwamba mtu anaweza akaikuza imani kwa kuishauri kwa hiyari akili yake ya ndani kwamba
anayo imani. Akili huja mwishowe, kuendana sawa sawa na asili ya ushawishi
ambao umekuwa ukitawala. Tambua ukweli huu na utaelewa ni kwanini ni muhimu kwako
kuchochea mihemko chanya kama nguvu zinazotawala katika akili yako, na kuivunjamoyo
– na kuiondoa - mihemko hasi.
Akili iliyotawaliwa na mihemko chanya huwa makao mazuri kwa hali ya akili
ijulikanayo kama Imani. Akili
iliyotawaliwa kiasi hicho inaweza kwa hiyari yake, kuipa akili ya ndani
maelekezo ambayo itayakubali na kuyafanyia kazi mara moja.
0 Response to "IMANI MAPENZI NA NGONO NDIYO VITU VYENYE NGUVU KULIKO MIHEMKO MINGINE YOTE MIKUBWA"
Post a Comment