Nimewahi kusoma mitandaoni na hata kusikia baadhi ya watu wakilalamika kwamba watoaji wa elimu ya pesa na mafanikio wengi wakiwamo waandishi wa vitabu, washauri, makocha, wanablogu na hata watoaji semina, kwamba ni matapeli, huwarubuni wasomaji kwa lengo la kuwauzia bidhaa zao vikiwemo vitabu, DVD pamoja na semina.
Kwenye tovuti(forum) moja maarufu nchini katika
mada iliyokuwa ikijadili elimu ya pesa na mafanikio, mchangiajimada mmoja
aliandika maoni yake hivi chini ya makala ile;-
“…Wanajifanya
wanazo kanuni za mafanikio katika vitabu, DVD na semina zao, lakini mwishoni
baada ya kununua na kusoma unakutana na taarifa za kawaida kabisa tena ambazo
mtu ungeliweza ukazipata kiurahisi tu mahali pengine popote pale mitandaoni na
kwenye vitabu mbalimbali…..”
Mimi mwenyewe binafsi kama mtu ninayejishughulisha na
utoaji wa elimu hiyo kupitia vitabu na
blogu, niliguswa sana na maneno hayo hasi juu ya tasnia hii ya elimu ya pesa na
mafanikio, ndipo nikaamua kufanya utafiti kupata majibu ni kwa nini kweli watu
wengi hushindwa kunufaika moja kwa moja na elimu hii kama watoaji wake
wanavyohubiri.
Lakini baada ya kuchunguza sana nilibaini kwamba mtu
kutokunufaika na elimu itolewayo kunachangiwa na sababu kadhaa kutoka pande
zote mbili, kwanza ni kutoka kwa watoaji elimu wenyewe kutokusema ukweli wote,
na sababu zingine huchangiwa moja kwa moja na yule anayepokea elimu yenyewe
kushindwa kuwajibika kwa kudhani ukishapata elimu ni basi mafanikio hutiririka
yenyewe mithili ya maji ya mto.
Mimi hapa leo nitajikita zaidi na sababu kutoka upande
wetu sisi wenyewe watoaji wa elimu ya pesa na mafanikio kwa kutokutoboa siri
zote anazopaswa mtu kuzifahamu kusudi aweze kupata mafanikio inavyostahili.
Simaanishi kwamba ni watoaji elimu ya pesa na mafanikio wote waliokuwa na
tatizo hili, la hasha, lakini ukitazama duniani kote wapo wengi wenye tabia hii
ya kutokuutoa ule ukweli wote kwa wateja wao.
Ni ukweli kabisa na tena usiopingika kwamba watoaji elimu
hii ya pesa na mafanikio duniani wako wengi. Ukiangalia kuna watu wa mwanzo
kabisa kama akina Wallace D. Wattles aliyeandika kitabu cha “Science
of Getting Rich” mwaka 1910,
Charles F.Haanel alliyeandika; “The
Master Key System” hapo mwaka 1912, Napoleon Hill
aliyeandika kitabu cha “Think and Grow Rich” mwaka 1938 na Dale Carnegie aliyeandika “How to Win Friends and Influence People” mwaka
1936
Kwanini nawaita watu wa mwanzo?, haimaanishi kuwa kabla
ya miaka hiyo basi kulikuwa hakuna wana-elimu ya pesa na mafanikio wengine hapana, walikuwepo wengi tu, watu kama akina Sun
Tzu wa china miaka
kabla hata ya Yesu Kristo na kitabu chake “The Art of War” ,
kulikuwa pia na Marcus Aurelius aliyeandika “Marcus
Aurelius’ Meditations”
mwaka 161 BC na Samuel Smiles kutoka
Uscotishi aliyeandika “Self Help” mnamo mwaka 1859, “As A Man Thinketh” cha James Allen
mwaka 1902 na wengineo wengi.
Na tena ndiyo maana hata ukawaona hao niliowataja
kuwa “watu wa mwanzo” wakiweza kutunga kazi nzuri, bila shaka kazi zao zilikuwa
ni matunda ya tafiti kutoka kwa kazi za wale waliokuwa wamewatangulia. Lakini
maana yangu ya kuwataja kuwa ni watu wa mwanzo inatokana na mantiki kwamba kazi
zao ndizo zilizoanza rasmi kupata umaarufu mkubwa dunia nzima na kusomwa zaidi
na watu wengi.
Halafu baada ya hao wakaja waandishi na wana-elimu ya
pesa na mafanikio(self improvement books) wa kizazi cha kati
mfano ni kina, OG Mandino na kitabu chake, The Greatest Salesman in The World”
mwaka 1968, “Sex and The Single Girl” cha Hellen Gurley mwaka 1962 “When
Bad Things Happen To Good People” cha Harold Kushner mwaka 1978, “To Have or To Be” cha Erich
Fromm mwaka 1976, “Feeling Good” cha David Burns mwaka 1980 na listi ni ndefu.
Na katika zama hizi za mtandao wa Intaneti nazo wapo wana-elimu ya pesa na mafanikio wengi
waliochipukia kote duniani na kutokana na usambazaji wa elimu kurahisishwa na
mitandao ya kijamii pamoja na tovuti mbalimbali imekuwa rahisi mno hata hapa
kwetu Tanzania napo kuibuka wana-elimu hiyo ya pesa na mafanikio.
Miongoni mwa hao ni akina Robert Kiyosaki na kitabu chake
“Poor
Dad Rich Dad”, Brian Tracy na “Self Made Millionaires” Malcolm Gladwell na “Outliers”, Randy Gage na
“Why
you are Dumb Sick and Broke” Donald Trump na “Think Like A Champion”
mwaka 2009 na Julia Cameroon aliyeandika “It’s Never Too Late to Begin Again” cha
mwaka 2016.
Kwa upande wa hapa nyumbani miaka ya nyuma kidogo
kulikuwa na akina Mama Terry miaka
ya 90 kuelekea 2000 aliyekuwa mhamasishaji Redioni, Marehemu Munga Tehenan aliyekuwa mhamasishaji na
mwanasaikolojia katika TV miaka ya 2000, pia aliwahi kutunga vitabu kadhaa vya
mafanikio kama vile, kitabu kiitwacho “Maisha na Mafanikio” , na alimiliki
gazeti maarufu wakati huo lililokuwa likichapisha makala za utambuzi binafsi
lililojulikana kama “JITAMBUE” chini
ya kampuni yake ya Jitambue Media.
Na sasa hivi wameibuka Wana-elimu ya pesa na mafanikio,
ikiwa ni pamoja na wale wanaotoa elimu ya biashara na ujasiriamali , wengi wao wakijikita hasahasa katika kutoa
elimu hiyo kupitia mtandao wa kisasa wa Intaneti, blogu, tovuti na mitandao ya
kijamii kama vile, facebook, wattsap, na baruapepe (e-mail).
Kuna Waandishi vitabu na blogs, waalimu wa elimu ya
biashara & ujasiriamali, Wahamasishaji,
Wanasaikolojia, Makocha na Washauri kama
vile akina; Marwa Shirati, Lemburis Kivuyo, James
Mwang’amba, Paul Mashauri, Chris Mauki, Eric Shigongo, Charles P. Nazi, Amani
Makirita, Felix Maganjila, Didas Lunyungu, Peter Augustino, Mch.Peter Mitimingi,
Dismass Lyassa na wengineo wengi.
Miaka tuseme 10 iliyopita, mtu wa kawaida tu ungeanzisha
blogu au website ungelianzia wapi ukiachilia mbali gharama ya kudizaini website
yenyewe iliyokuwa zaidi ya Sh. Milioni moja za Kitanzania?.
Mtu anaweza akajiuliza hivi;
“Mbona nimeshasoma vitabu vingi tu na
kuhudhuria semina kibao za nje kama vile vitabu vya akina Napoleon Hill, Brian
Tracy, Robert Kiyosaki, Donald Trump, na hata vitabu na semina za ujasiriamali
za waandishi na washauri wa hapa nyumbani Tanzania lakini bado sijaona
mabadiliko yeyote, wala sijaweza kuondokana na umasikini wa kipato niliokuwa
nao, Tatizo liko wapi?”
Jibu la swali hilo tutakwenda kulijua leo hii hii.
Baada ya kufanya utafiti huo mimi nikishirikiana na timu
yangu ya Self Help Books Publishers Limited, tuliibuka na jibu. Kwanza kabisa
ieleweke kwamba, siyo kila mtu anayefuatilia mafunzo hayo ya hawa watoa-elimu
ya pesa na mafanikio anashindwa kupata matokeo mazuri ya kuridhisha hapana, ila
kwa kweli ni namba kubwa ya watu wanaolalamikia kushindwa kubadilisha maisha
yao baada ya kufuatilia programu za wana-elimu ya mafanikio hao.
Kuna baadhi ya watu sijui niseme ni werevu au labda ni
wepesi wa kubaini siri, basi hujikuta“automatically”
(moja kwa moja) kwa kuzifuatilia programu zitolewazo na wana-elimu ya pesa na
mafanikio hawa, wanabadilisha maisha yao kwa spidi ya ‘rocketi’, miezi
miwili….. mitatu…mwaka…. wanajikuta wapo ‘levo’ zingine kabisa. Ila cha kusikitisha ni
watu wachache mno!
Na hii si mara ya kwanza, Self Help Books kuweka
wazi siri ambazo wale wanaozifahamu inawawia vigumu kuziweka hadharani.Tangu
tuanze kampeni yetu ya kwanza kabisa tuliyoipa jina mwanzaoni kama kampeni ya “KUELEKEAUTAJIRI”hapo mwaka 2012 na baadaye kulazimika kuibadilisha na kuiita kampeni ya “jifunzeujasiriamali Kutokomeza
Umasikini”, Tuliwahi kuziweka wazi siri kama tano hivi, angalao kila
moja katika kila kitabu, tovuti na blogu
tulizoanzisha.
Matokeo ya kampeni hiyo na utoboaji wa siri hizo ulileta
matokeo mazuri yakushangaza. Kumekuwa na ongezeko kubwa la mwamko wa watu hasa
vijana katika kujihusisha na shughuli za ujasiriamali sambamba na watu
kupunguza kwa kiasi kikubwa kuficha siri za mafanikio yao.
Kabla ya mwaka 2012 ilikuwa ni mwiko mtu hata kuelezea
namna utajiri wake alivyoupata. Ungeweza kukuta labda hata mtu anao ujuzi wa
kutengeneza kitu kama keki, lakini alikuwa tayari afe na kuzikwa na ujuzi wake
kuliko kumfundisha jirani yake, hata ikiwa ni kwa kumlipa pesa.
Kampeni zile na hata programu zingine zinazoendeshwa na wana-elimu ya pesa na mafanikio wengine
nchini zimeleta mapinduzi makubwa, leo hii karibu kila jambo huwekwa wazi, hata
matajiri na waliofanikiwa kimaisha waliokuwa hawapendi kuweka wazi walao baadhi
tu ya njia za mafanikio walizopitia, sasa wanasema waziwazi bila ya kificho.
Wenye mbinu na utaalamu wa aina mbalimbali nao huwafundisha watu wengine
kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile, redio, tv, majarida, vitabu,
semina na makongamano.
Katika hili la Elimu ya pesa na mafanikio kushindwa
kuwasaidia waliokuwa wengi, hapo bado kuna siri iliyojificha na kama
ningelikuwa “serikali” basi ningelisema
pana “jipu linalotakiwa kutumbuliwa” Na siri hiyo iliyojificha ama ‘JIPU’, hata sisi watoaji wa elimu ya
pesa na mafanikio wenyewe huwa hatupendi kuitoa kwa wateja wetu kwa hofu moja
tu ya; KUKOSA WATEJA WA BIDHAA ZETU,
VITABU, DVD, SEMINA NA VIPINDI VYA REDIO NA TELEVISHENI.
Waandishi wa vitabu, Wanablogu, Waandaaji wa semina, na
Waelimishaji wengineo wa elimu ya pesa na mafanikio(maendeleo binafsi), hudhani
kwamba kwa kuwafunulia wateja wao siri hiyo kubwa, basi na huo ndio utakaokuwa
mwisho wa wao kufuatilia mafundisho yao zikiwamo pia na bidhaa wanazowauzia. Ni
watoa-elimu ya mafanikio wachache mno duniani niliogundua kwamba walijaribu
kuiweka siri hiyo wazi lakini kwa kuibanabana kiasi kwamba mtu wa kawaida
inakuwa vigumu mno kuishitukia.
Mathalani ni waandishi wa vitabu wawili tu wa Kimataifa
akiwemo, Brian Tracy niliowaona katika kazi zao wameliweka suala hilo wazi. Kwa
upande wa watoa-elimu ya pesa na mafanikio wa hapa Tanzania aliwahi kuwepo
mwandishi-mwanasaikolojia mmoja na ambaye kwa sasa ni Marehemu, Munga Tehenan(Mungu
amrehemu), alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa elimu hiyo hapa nchini.
Mwingine ni mwanablogu mmoja mtunzi wa vitabu vya
kielectronic, e-books, niliona alijaribu
kuidokeza siri hiyo japo naye kwa kuhofia kuhatarisha mauzo ya kazi zake
akaitoa nusunusu pasipo kueleweka vyema na msomaji wa kawaida.
Kama kawaida yangu mimi na jopo langu, nimeamua kujitoa
muhanga tena, Nitaitoboa siri hiyo! Siri
ambayo baada ya utafiti wa karibu mwaka mmoja, nimeibuka pia na kanuni maalumu(Nadharia) niliyoipa jina langu
mwenyewe; “Peter’s Theory Of Studying Succes Books”(Nadharia ya Peter ya
kujifunza Vitabu vya Pesa na Mafanikio kwa ufanisi)
Ama kweli kimya kingi kina mshindo mkuu!, kanuni hii
kuivumbua ilinigharimu muda mwingi na pesa, hata ilinibidi kusitisha mambo
yangu mengi ya msingi ikiwemo kazi ya kuposti makala na insha zangu katika
blobu na tovuti za “jifunzeujasiriamali”, wasomaji wangu wengi walikuwa wakishangaa
kuona sitoi vitu vipya kila siku na nawaomba radhi sana kwa hilo.
Kazi za utafiti bwana, kama huna moyo unaweza kuachia
njiani, zinakufilisi mpaka senti tano ya mwisho mfukoni, huwezi kuamini hata
watu wako wa karibu mno utawasikia wakisema, “Kafulia huyo, anafanya nini
mjini, si arudi tu kijijini akalime kama
maisha yamemshinda?”
Kwa kauli kama hizo Unahisi kukata tamaa, lakini kwa kuwa
umedhamiria kuelimisha umma unapiga moyo konde na kusonga mbele, “You
never give up”. Kwa kuwa sasa nimeshamaliza, kazi imebakia kwako tu
ndugu msomaji wetu kuichukua na kuiweka katika VITENDO kanuni hiyo.
Unaweza ukadhani ni blaablaa tu za kawaida, nikitaka
kukughilibu ili niuze, lakini nakuhakikishia, Self Help Books hatupo hivyo,
kwanza wala hautadaiwa senti tano ili kupata kitabu chenye kanuni hiyo, utakipata Bure kabisa!. Pili, kukuhakikishia hatuna hila zozote, unaweza
ukapata ushahidi kutoka katika ahadi na kazi zetu zilizopita tangu mwaka 2012
tulipoanzisha kampeni ya kupambana na umasikini, soma makala hii hapa.
Moja ya malengo yetu siku zote imekuwa ni ‘kuvunja
miiko’, kutoboa siri ambazo
wengi hawapendi kuziweka wazi kwa hofu ya watu wengi zaidi kuzijua na kunufaika
kama wao, kumbe ni imani potofu. Hawajui kwamba jamii pana zaidi inapopata
maendeleo, majanga na majuto hupungua
huku kila mtu akifurahia maisha.
Unajisikia raha gani wewe ambaye maisha yako umepiga
hatua huku mtoto wa jirani yako hana hata malapa ya kuendea shuleni? Kesho na
keshokutwa mtoto huyu akikosa kabisa ada akaacha shule na kugeuka jambazi sugu
kisha akaja kuwakaba wanao akiwashikia mapanga na bunduki, utaendelea kufurahia?
Basi masikini huyu hana hata haja na pesa zako, mpe tu moyo na ikiwezekana
maarifa yatakayomkomboa kutoka katika lindi hilo la umasikini, atajikwamua
mwenyewe na wote kwa pamoja mtaendelea kufurahia maisha "forever"
Nisingelipenda kukuchosha sana mpenzi msomaji, nakuomba
sasa ukaisome Siri yenyewe na Kanuni maalumu ya kujifunza elimu ya pesa na mafanikio
kwa ufanisi kupitia barua-pepe yako, ‘e-mail’. Sikutaka kuiweka moja kwa
moja hapa katika blogu hii kwani siyo kila mtu yupo tayari kuisoma. Ikiwa upo
tayari, ni bure kabisa hakuna malipo yeyote, ila cha kufanya tafadhali ni kuweka email yako hapo chini kwenye box,
majina yako mawili, na namba ya simu, kisha bonyeza kitufe chenye
maandishi, “subscribe”
Ukishamaliza nenda katika email yako ifungue utakuta
tumekutumia ujumbe unaosema dhibitisha, bonyeza hapo na ukubali
kudhibitisha.Baada ya hapo, utatumiwa e-mail nyingine yenye zawadi ya kitabu
hicho kilichobeba Siri na Kanuni maalumu ya kujifunza vitabu vya Pesa na Mafanikio kwa
Ufanisi wa hali ya Juu.
Ukumbuke ndugu msomaji wangu taarifa zako hizi zitakuwa
salama, hatuna nia ya kuzitumia kwa lengo jingine lolote lile tofauti na hilo
la kukutumia taarifa muhimu kwako na ambazo siyo za kuweka kwenye blogu kila mtu azisome. Wewe unayetupatia email
yako ni maalumu(spesho) kwetu. Wala
hatuwezi kamwe kumshirikisha mtu mwingine yeyote taarifa zako.
Kwa upande wako pia kuna faida nyingi utakazozipata. Mbali na kitabu hicho kipya cha Siri na kanuni ya kusoma vitabu vya pesa na mafanikio bila malipo, pia chini yake tumeambatanisha zawadi nyingine ya vitabu 25 bora kabisa, vya waandishi mbalimbali mashuhuri wa kimataifa, navyo hakuna malipo yeyote utakayochajiwa ni “free of charge”.
Siku za usoni pia tutakutumia vitu vingine vizuri kama vile; Michanganuo ya biashara zile zilizokuwa na fursa kubwa ya kutengeneza faida, ‘Updates’ mbalimbali kila mara zitakapotokea wewe ndiye utakayekuwa wa kwanza kuzipata, makala zile zilizokuwa na umuhimu wa kipekee pamoja na Vitabu vinginevyo vya bure bila malipo tutakavyoendelea kutunga.
Siku za usoni pia tutakutumia vitu vingine vizuri kama vile; Michanganuo ya biashara zile zilizokuwa na fursa kubwa ya kutengeneza faida, ‘Updates’ mbalimbali kila mara zitakapotokea wewe ndiye utakayekuwa wa kwanza kuzipata, makala zile zilizokuwa na umuhimu wa kipekee pamoja na Vitabu vinginevyo vya bure bila malipo tutakavyoendelea kutunga.
naomba kutumiwa icho kitabu apo tayari nimeshajiunga
ReplyDeleteBila shaka mr. JAULA tulishasolve hilo, Asante
DeleteNishajiunga tayari
ReplyDeleteNaomben kitabu hicho tayar nmejiunga
ReplyDeleteNaomben sasa hivy vitabu
ReplyDeleteNishajiunga naomba vitabu sasa
ReplyDelete