Ni ubunifu wa
vijana wawili ndugu, Innocent Junior na Innocent senior walioamua kuanzisha
Ujasiriamali wa kijamii baada ya kuhitimu Elimu yao ya chuo kikuu katika chuo
kikuu cha Mt. Augustine. Hutumia matoroli kama maktaba ya vitabu kwa watoto wa
shule za awali na msingi Mkoani Mwanza.
Soma pia: Teknolojia itakayowakomboa wasanii wa video na muziki Tanzania.
Soma pia: Teknolojia itakayowakomboa wasanii wa video na muziki Tanzania.
Vijana hawa baada ya kubaini matatizo mbalimbali yanayowakabili watoto wadogo wanafunzi wa
shule za msingi katika kupata vitabu vya kujisomea, tatizo la lugha hasa kutoifahamu
vyema lugha ya kiingereza, kutokuwa na ari ya kujisomea vitabu, ukosefu wa
mazingira mazuri ya kujisomea, shida ya umeme hasa nyakati za usiku, ukosefu wa
mikoba mizuri ya kuhifadhia na kubebea vifaa vya shule kama madaftari, kalamu
nk. waliamua kuanzisha shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama, “My Little
Traveling Library” au Maktaba inayotembea.
Vijana hawa huenda mashuleni wakiwa na matoroli yao
yaliyobeba vitabu, na baada ya kuomba ruksa kutoka mamlaka husika, hugawa
vitabu hivyo bure kwa watoto wanafunzi ili kuwajengea utamaduni mzuri wa
kujisomea maishani mwao. Wanafunzi hao baada ya kusoma vitabu hivyo hatimaye
huvirudisha na kuazima tena vitabu vingine.
Watoto
wakifurahia vitabu.
|
Wanawatofautisha watoto katika makundi ‘grades’ kuanzia
grade 1 mpkaka grade 8 ambapo grade 8 wanakuwa wameshaweza kusoma na kuelezea
kile walichokisoma mbele ya darasa(representations). Hali hii imeongeza
mahudhurio na ufanisi wa watoto katika mashule wanakohudumia.
Katika kuinua ufahamu na ari ya wanafunzi kupenda
kujifunza, My little travelling library pia wameanzisha mashindano ya kusoma baina
ya shule na shule na hata madarasa kwa madarasa. Mbali na hayo pia wameanzisha
timu ya mpira, picnics, klabu za midahalo(debates) pamoja na kuonyesha video
mbalimbali za masomo muhimu kama ya sayansi kwa kutumia projekta.
My Little Travelling Library inadhaminiwa na mradi wa
Kampuni ya simu ya Tigo ujulikanao kama “Tigo Digital Change Makers” ambapo wao
ni washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2014.
Soma na: David Adjae, mbunifu majengo wa kimataifa aliyezaliwa Tanzania.
Soma na: David Adjae, mbunifu majengo wa kimataifa aliyezaliwa Tanzania.
Ili Taasisi hii iweze kujitegemeza yenyewe, wameanzisha
mradi mwingine wa kutengeneza na kuuza mabegi mazuri kwa ajili ya kubebea vifaa
vya shule vikiwamo vitabu na zana zingine za darasani. Mikoba hii au mabegi
yametengenezwa kwa vitambaa, maarufu kama “Mashuka ya Kimaasai.”
Mabegi
hayo yakitengenezwa.
|
Kitu kingine kizuri cha ubunifu katika mabegi hayo ni
kwamba yameunganishwa na mfumo maalumu wa umeme-jua ‘solar’ ambao humuwezesha
mtoto nyakati za usiku kuunganisha balbu ambayo huwaka na kumuwezesha kusoma
bila shida.
Kwa habari zaidi kuhusiana na Asasi hii ya My Little
Traveling Library unaweza ukatembelea website yao hii hapa.
Sikiliza makala hiyo katika sauti kama ilivyotolewa na
Redio Deutsche welle Ujerumani siku ya Jumatano tarehe 25 may 2016.
CHANZO
cha
makala haya ni Tovuti ya My Little
Travelling Library pamoja na Redio DW
Ujerumani idhaa ya kiswahili.
0 Response to "MAKTABA YA VITABU INAYOTEMBEA MASHULENI MWANZA(LITTLE TRAVELLING LIBRARY)"
Post a Comment