Ikiwa leo ni siku ya
mama duniani, watu wengi katika nchi nyingi duniani wamekuwa wakiwakumbuka mama
zao, upendo waliokuwa wakiwaonyesha walipokuwa wadogo mpaka hata sasa hivi
ukubwani pamoja na kujitoa hata pale kulipokuwa na hatari kubwa kiasi gani.
Siyo kama kina baba
hawana upendo kiasi hicho kwa watoto wao, lakini kusema ule ukweli kina mama
ndiyo waliokuwa na dhamana kubwa zaidi pengine kutokana na kazi ya ulezi kuwa
inafanywa na wao zaidi na muda mwingi hujikuta wakiwa na watoto hasa wanapokuwa
wadogo.
Nakumbuka sana mama
yangu mzazi tukiwa wadogo alikuwa mara kwa mara akitusimulia jinsi ambavyo
kitendo cha yeye na baba kutaka kuachana kilivyokuwa kigumu kutokana na
kufikiria suala la watoto wake ambao ni sisi. Anasema kuna nyakati walifikia
hatua ya kuachana baada ya kutokuelewana lakini alipowaza juu yetu watoto na kututazama tulimtia
huruma mno kiasi cha kuahirisha uamuzi wake.
Kisa hiki cha mama
kinanifanya nizidi kuamini kwamba kweli
upendo na huruma ya mzazi hasahasa mama hupindukia kiasi kama makala nyingine hii inavyouelezea uhusiano baina ya mzazi na mwanaye.
Wazazi wote mama na
baba wana umuhimu wa kipekee kama mwanamuziki huyu hapa chini, mwanamama Doly
Parton alivyoimba katika kibao chake hiki maarufu katika mtindo wa Country, “I remember mama and Daddy most of all”
akimaanisha “Nawakumbuka mama na baba
zaidi ya vyote”.
Kwa heshima ya siku
hii ya mama nimeyatafsiri mashairi ya wimbo huo yote kuanzia mwazo hadi mwisho
katika lugha ya kiswahili, pamoja na kuweka audio na video ya wimbo huo.
Popote pale ulipo
ukihangaika na maisha, iwe unafanya ujasiriamali, au hata umeajiriwa mahali,
wazazi hasa mama ni watu wa kukumbuka sana. Inawezekana kiuchumi hali yako ni
duni unashindwa kuwapa chochote lakini walao chukua muda kuwatafakari na kuwaenzi moyoni
mwako. Na wala haijalishi kama wameshatangulia mbele za haki au bado wapo hai.
Audio ya wimbo Nawakumbuka mama na baba zaidi ya vyote
Audio ya wimbo Nawakumbuka mama na baba zaidi ya vyote
Video ya wimbo Nawakumbuka mama na baba zaidi ya vyote.
Mashairi ya wimbo, "Nawakumbuka mama na baba zaidi ya vyote" wa 'Dolly Parton'.
Nawakumbuka Nawakumbuka
Nawakumbuka mama na baba zaidi ya kitu chochote.
Nayakumbuka malisho na mashamba ya ngano ya dhahabu.
Nawakumbuka ndege waimbao
na miwa mitamu mno
Nakumbuka vitu vingi
sana ambavyo mara nyingi hujirudia akilini
Lakini namkumbuka
mama na baba zaidi ya vyote
Naukumbuka mkate wa
tangawizi, aliokuwa akioka mama yangu
Na naikumbuka midoli
ya kutengenezwa nyumbani, ambayo baba alikuwa akitengeneza.
Ndiyo nakumbuka vitu
vingi, ambavyo hujirudia akilini mara kwa mara.
Lakini nawakumbuka
mama na baba zaidi ya vyote.
Nawakumbuka mama na
baba zaidi ya vyote.
Na nyumba yetu ndogo
kijijini, walijawa na upendo.
Nawakumbuka mama na
baba zaidi ya vyote.
Na vitu vyote
walivyofanya, kufanya maisha yawe ya furaha kwetu.
Ndiyo nakumbuka vitu
vingi sana ambavyo hujirudia akilini mara kwa mara.
Lakini nawakumbuka
mama na baba zaidi ya vyote.
Nakumbuka peremende
baba alizokuwa akileta, nakumbuka nyimbo mama alizokuwa akiimba.
Oh nakumbuka vitu
vingi, ambavyo hujirudia akili mara kwa mara.
Lakini nawakumbuka
mama na baba zaidi ya vyote.
Nawakumbuka mama na
baba zaidi ya vyote.
Na jinsi walivyokuwa
wakitufunza sisi watoto, yaliyokuwa mema na mabaya.
Nawakumbuka mama na
baba zaidi ya vyote.
Jinsi walivyotumaini
na kusali, kusudi waishi watuone tukikua.
Oh nakumbuka vitu
vingi ambavyo hujirudia akilini mara kwa mara.
Lakini nawakumbuka
mama na baba zaidi ya vyote.
Nawakumbuka,
Nawakumbuka, Nawakumbuka mama na baba zaidi ya vyote, zaidi ya vyote.
.................................................................................................
0 Response to "MAMA HUBEBA WATOTO WAO KIPINDI KIFUPI LAKINI MIOYO YAO HUWABEBA MILELE"
Post a Comment