“Hivi ni biashara gani yenye faida kubwa na ya
haraka ninayoweza kuanzisha?” Hili ni swali
ambalo bila shaka yeyote ile kila
anayefikiria kuanzisha biashara mpya au hata mwenye biashara lakini
angependa kujitanua zaidi hujiuliza.
Ingawa kimsingi hakuna biashara isiyokuwa na
faida, lakini faida ya biashara katika sekta tofauti hutofautiana kulingana na
tofauti pia katika mahitaji, nikiwa namaanisha gharama mbalimbali zinazohusika
katika kuanzisha na kuendesha biashra zenyewe. Kuna biashara ambazo gharama za
kuanzisha ni kubwa, hali kadhalika pia zipo biashara
ambazo gharama za uendeshaji wake ni kubwa na kuna biashara nyingine
utakuta gharama zake zote wakati wa kuanzisha na hata kwenye uendeshaji ziko
chini sana.
Hatua ya kuanza biashara ndiyo hatua ngumu
kushinda hatua zingine zote na sababu kuu inayotengeneza ugumu huo si nyingine
bali ni mtaji au rasilimali za kuanzia ambazo mara nyingi na kwa watu wengi
wanaoanza biashara huwa changamoto yao kubwa ni namna ya kuweza kupata
rasilimali za kutosha kuisimamisha biashara husika.
Kwa sababu hiyo ndiyo maana utakuta watu
wengi wakiumiza vichwa kutaka kufahamu biashara watakazofanya kwa
rasilimali(mtaji) kidogo waliokuwa nao lakini wakati huo huo wakipata faida
kubwa katika kipindi kifupi inavyowezekana.
Mtaji kidogo ni chanzo kikubwa cha ‘vifo’ vya
biashara nyingi ndogo ndogo zinazoanza na pia ndiyo chanzo kikuu cha wamiliki
wa biashara hizo kushindwa kutenganisha matumizi ya fedha za biashara na yale
ya kwao binafsi kwani kwa mfano pale mtu
anapokumbana na hali ya ugojwa wa mpendwa wake mathalani mtoto, inakuwa vigumu
mno kusita kutumia pesa ya biashara kuokoa maisha ya mtoto huyo. Ni
kipi bora, afe mtoto au ife biashara?
Ili basi kuepukana na changamoto zote hizi
ndipo sasa utakuta watu wakijiuliza “Ni biashara gani iliyokuwa na faida kubwa
inayoweza ikafanyika haraka katika kipindi kifupi na kurudisa mtaji wote
uliowekezwa?.”
Katika kutafiti ni biashara ipi nzuri
inayolipa haraka, yapo mazingira na vigezo vingi
mtu anavyotakiwa kuzingatia wakati anapotaka kuanzisha biashara
iitakayomlipa vizuri. Kwa mfano wazo la ni biashara ipi mjasiriamali afanye, atatakiwa
kutumia mbinu hizi nne kupata wazo bora la biashara itakayofaa.
1. Anaweza
akafikiria ni kitu gani anachopendelea zaidi kukifanya maishani kwake,
2. Wazo
linaweza likatokana na taaluma mtu aliyosomea,
3. Uzoefu
wa muda mrefu katika jambo fulani,
4. Matatizo
na mahitaji katika jamii nk.
Mjasiriamali hapaswi kuangalia tu faida peke yake kama
kigezo cha kuamua ni wazo lipi la biashara itakayomfaa bali pia atatakiwa
aangalie na vigezo vingine kama hivi vifuatavyo’
· Je,
biashara hiyo inaoana na ujuzi aliokuwa nao?
· Ni
aina gani ya leseni ya biashara inayohitajika katika biashara aliyochagua?
· Kama
kuna mafunzo yatakayohitajika, ni mafunzo ya aina gani?
· Ni
lazima achunguze pia jinsi biashara itakavyostahimili kipindi cha mdororo wa
uchumi endapo utatokea.
Pamoja na mbinu na vigezo hivyo lakini
mwishowe mtu huyo atapaswa kujitathmini mfukoni mwake ikiwa anazo rasilimali za
kutosha kuanzisha mradi alioamua kuanzisha na hapo ndipo huja suala la
kuangalia ni biashara ipi kati ya zile alizokuta zinaendana na mazingira
yaliyokwishatajwa hapo juu ambayo anaweza akaianzisha.
TANGAZO.
Biashara
zenye faida kubwa na zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo uliowekezwa.
Biashara
za utoaji wa huduma ndizo zinazoshikilia namba moja kwa kuwa na faida
kubwa zaidi huku zingali zikigharimu mtaji kidogo kushinda biashara za aina
nyinginezo kama za utengenezaji na
uuzaji wa bidhaa mbalimbali.
Asilimia ya faida kwa mauzo katika biashara
nyingi za huduma utakuta zinafikia mpaka asilimia 20%. Hii ina maana kwamba
katika kila mauzo ya shilingi 100 basi faida halisi ni shilingi 20, wakati jumla ya gharama zote ni shilingi 80. Wakati
kwa upande wa huduma asilimia ya faida kwa mauzo ikikadiriwa kufikia 20%, katika
upande wa bidhaa utakuta inakadiriwa kuwa ni asilimia chini ya 10%.
Sababu
kubwa 4 ni kwanini biashara za utoaji wa huduma zinakuwa na faida kubwa kiasi
hicho?
I.
Biashara hizi kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa kwa
mtaji-rasilimaliwatu. Hakuna
gharama kubwa za vifaa, malighafi wala usafirishaji.
II.
Gharama za uendeshaji kama vile mishahara, kodi,
leseni na pango vipo chini sana, na ni kidogo jambo linalosababisha faida kuwa
juu.
III.
Gharama kidogo za kuanzisha, kwa mfano,
nyingi ya biashara za huduma zinaweza zikaanzishwa majumbani- chumbani,
sebuleni, barazani au hata katika kibanda cha stoo isiyotumika.
IV.
Biashara za huduma huwa zinakuwa na wateja
wanaojirudiarudia. Utakuta mteja anayenunua huduma kwako leo anarudi tena kwa
huduma kama ileile baada ya muda fulani kupita hivyo kuendelea kukuingizia
faida.
Hebu sasa tuanze kuzitazama baadhi ya hizo
biashara za utoaji huduma zile zinazoongoza kwa kutengeneza faida nyingi zaidi.
Kumbuka lakini biashara za huduma zipo nyingi sana zaidi ya hizo zilizotajwa
hapo chini na mfano ni biashara kama hii ninayoifanya hapa(kwa kuwa mimi siyo mchoyo na kamwe nisingependa kuficha siri kama baadhi ya watu wengine wafanyavyo).
Biashara ya kwenye mtandao wa intaneti ikiwa utaweza kutoa huduma watu wakazipenda, zina faida zaidi hata ya asilimia 50% nikiwa na maana mara 2 au 3 ya mtaji utakaowekeza. Kwa undani zaidi juu ya mada hiyo, unaweza ukasoma ndani ya kitabu chetu kilichojipatia umaarufu mkubwa cha "MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA." bofya maandishi hayo kupata ufafanizi zaidi.
Biashara hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;
Biashara ya kwenye mtandao wa intaneti ikiwa utaweza kutoa huduma watu wakazipenda, zina faida zaidi hata ya asilimia 50% nikiwa na maana mara 2 au 3 ya mtaji utakaowekeza. Kwa undani zaidi juu ya mada hiyo, unaweza ukasoma ndani ya kitabu chetu kilichojipatia umaarufu mkubwa cha "MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA." bofya maandishi hayo kupata ufafanizi zaidi.
Biashara hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;
1. UHASIBU,
USIMAMIAJI WA MAKAMPUNI NA BIASHARA.
Haijalishi ikiwa hali ya kiuchumi ni mbaya
kiasi gani, lakini watu ni lazima watahitaji huduma za uhasibu. Biashara hizi
pia huhusisha shughuli zinazofanana nazo kama vile, Utunzaji wa mahesabu ya
biashara, Ushauri wa kibiashara, huduma za ajira na matayarisho ya kodi. Hizi ndiyo
biashara zinazoshikilia nafasi ya kwanza kabisa katika kutengeneza faida nono
zaidi kidunia.
2. UWAKALA
NA UDALALI WA ARDHI NA MAJENGO(Real estate agency and Brokers)
Uwekezaji halisi wenyewe katika biashara hii
ya ardhi na majengo mafanikio yake yanategemea zaidi kuboreka kwa hali ya
kiuchumi lakini siyo katika upande wa Madalali na Mawakala wake. Wao ni kinyume
kwani hawana gharama kubwa za uendeshaji biashara zao. Hata hali ya uchumi
idorore vipi madalali na mawakala wa biashara ya ardhi na majengo huendelea
kupata faida nzuri. Kuanzisha biashara hii, mtaji pekee utakaohitajika ni fedha
kwa ajili ya kupata leseni.
3. HUDUMA
ZA KISHERIA.
Kama ilivyokuwa kwa upande wa huduma za
uhasibu, pia huduma za kisheria gharama zake za ueneshaji na hata zile za
kuanzia siyo kubwa sana na huwa wanapata wateja wanaorudi tena na tena hivyo
kuifanya biashara hii nayo kuwa ni yenye faida kubwa. Biashara hii haiwahusishi
mawakili wa kujitegemea tu peke yao, bali huwahusisha pia na mawakala wa shughuli
za kisheria kama vile, madalali wa mahakama, wasuluhishi wa migogoro nk.
4. UAZIMISHAJI NA UKODISHAJI WA MITAMBO.
Katika
uchumi wa sasa usiotabirika kirahisi, watu wengi kununua mitambo kwa mfano,
matrekta, vijiko na hata magari kwa ajili ya shughuli za muda mfupi huwa vigumu
kidogo na badala yake huamua kutafuta mahali pa kuazima au kukodisha kwa muda
fulani tu, na ndipo sasa utakuta wenye biashara hizi wanapata fedha nyingi na
baada ya kipindi kifupi mitaji waliyotumia kununulia mitambo na vifaa husika
hurudi halafu kinachofuata hapo ni faida kubwa. Unaweza ukaazimisha watu
binafsi, vilevile hata makampuni.
5. HUDUMA ZA KIAFYA.
Katika Biashara hizi, kuna huduma mbalimbali
mfano; Huduma za matibabu ya meno, Matabibu wanaotumia mimea na miti shamba,
vituo vya mazoezi ya viungo kwa waliovunjika na wenye matatizo ya misuli, vituo
binafsi vya afya na zahanati, huduma za ushauri wa kiafya nk. Kama ilivyo kwa
huduma zingine zilizotangulia, linapokuja suala la afya, halina mjadala kabisa
kwani, hata ikiwa mtu hana senti tano mfukoni lakini mbele ya kupona atafanya
kila linalowezekana ili mradi tu amepata fedha kwa ajili ya matibabu.
6. BIASHARA YA UZALISHAJI NA USAMBAZAJI WA
NISHATI HUSUSANI ILE YA UMEME.
Gharama za awali zaweza kuwa kubwa kidogo
lakini ni biashara itakayozalisha faida kubwa na endelevu kwa kipindi kirefu
kitakachofuata kwani nishati hasa ya umeme ni hitaji la msingi na ambalo mtu
atahitaji kila siku, ni kama vile ilivyokuwa chakula. Nishati ya umeme yaweza
kuzalishwa kutokana na vyanzo mbalimbali kama vile; maporomoko ya maji ya mito,
upepo, gesi, mafuta, jua(solar), “geothermal-energy(maji ya moto kutoka katika
miamba ardhini)”, mawimbi ya bahari na nishati ya nyuklia(atomic energy).
7. KUBUNI, KUDIZAINI NA KUCHORA ALAMA,
NEMBO(LOGO) MBALIMBALI ZA BIASHARA NA MAKAMPUNI.
Kila biashara/kampuni huhitaji huduma hizi
kuanzia kutengenezewa matangazo, mabango, kuandaa hati za usajili wa shughuli
mbalimbali (mfano makampuni & Ngos), kutengeneza kurasa za magazeti, tovuti
na blogs(graphics design), kudizaini na kuchora ramani za majengo, kudizaini
michoro ya bidhaa mbalimbali za viwandani nk. Sehemu kubwa ya gharama katika
shughuli zote hizi ni muda wako tu endapo tayari ujuzi unao pamoja na fedha
kidogo za kununulia kompyuta ya mezani au ile ya kupakata “laptop”.
8. TAASISI NA MASHIRIKA YA KIDINI.
Dhana kuwa mashirika ya kidini hayapo kwa
ajili ya kutengeneza faida(non profit organization), haimaanishi kwamaba
hayalengi kutengeneza faida kabisa bali kinachotazamwa zaidi ni kwa namna gani
faida inayopatikana inavyotumika. Kwa mfano badala ya faida kugawiwa kwa
wamiliki(wanahisa au waanzilishi) kama ilivyokuwa kwa makampuni ya kibiashara, faida
hiyo inapaswa kuelekezwa katika kuendeleza na kukuza zaidi dhamira(mission) ya taasisi
husika. Taasisi na Mashirika hayo huhusisha siyo tu Misikiti na Makanisa bali
pia na taasisi zilizokuwa chini yake mfano, mashule, vyuo, vyuo vikuu,
mahospitali na vituo vya afya.
…………………………………………………………………..
*Mpenzi msomaji wa makala hii, kama ulikuwa hujasoma
kitabu tulichokuandalia bure bila malipo cha “KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA
NA MAFANIKIO KWA UFANISI” basi, jiunge na blogu hii kwa kuweka e-mail yako, majina na namba ya
simu katika fomu iliyopo mwanzoni mwa blogu upande wako wa kulia au mwishoni
mwa makala hii iitwayo “KWANINI VITABU NA SEMINA ZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO HAVIWASAIDII WATU WENGI?.”
Fuata
maelekezo ikiwa ni pamoja na kufungua email yako hiyo na kisha uthibitishe
kukubali kutumiwa kitabu pamoja na zawadi nyinginezo zitakazoambatanishwa nacho
halafu utaweza kukipakua(download). Ikiwa tafadhali utapata ugumu kukipakua
kitabu hicho aidha kwa kushindwa kujiunga ama kikwazo kingine chochote kile
basi naomba tujulishe kupitia meseji au email, jifunzeujasiriamali@gmail,com
Pia vitabu vyetu vingine vyote vya kulipia
vipo, ikiwa utahitaji kitabu chochote kile kimojawapo basi wasiliana na sisi
kwa namba 0712 202244 au 0765 553030 na
tutakutumia popote pale ulipo mikoani au kama upo hapa Dar es saam pia
tuwasiliane.
Vitabu vyetu vyote vipo katika mfumo wa vitabu vya
karatasi,(hardcopy) pamoja na mfumo wa kielektroniki (softcopy)“MIFEREJI 7 YA PESA”, “SIRI YA BIASHARA ZA REJAREJA” na MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa huu, > >SMARTBOOKSTANZANIA
TUPO MBEZI KWA MSUGURI KARIBU
KABISA NA KITUO CHA DALADALA, NI KITUO CHA PILI KUTOKA MBEZI MWISHO KAMA UNARUDI
KIMARA TERMINAL.
0712 202244 & 0765 553030
jifunzeujasiriamali@gmail.com
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteComment tunazikaribisha kwa mikono miwili lakini siyo tangazo la biashara kama mwenzetu huyu alivyoliweka, bora basi angeanza kiubunifu kidogo hata kwa kuzungumzia kwanza post husika.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete- shukrani sana
ReplyDeleteAsante nawewe pia!
DeleteUnapataje mkopo au hatua zakufuata ni zipi
ReplyDeleteMikopo ukienda katika taasisi nyingi za fedha ikiwemo Mabenki kila moja ina utaratibu wake lakini mambo ya msingi wanayoangalia zaidi bila kujali umeenda benki au taasisi ipi ni, kwanza uwe na biashara ambayo tayari ulishaianzisha na inafanya kaz, Pili ni lazima uwe na dhamana, dhamana inaweza kuwa ni mali au mtu/watu wengine wanaoaminika. Tatu uwe unakopesheka isijekuwa umekimbia madeni kwingine au huna makazi maalumu na eneo unakofanyia biashara na Nne uwe unatambulika rasmi na serikali ya mtaa unakoishi
Deletevizuri sana mkuu
ReplyDeleteAsante sana Elimika!
DeleteAsante sana mkuu
ReplyDeletenawewe pia ndugu
Delete