Kuna vitu kadhaa mjasiriamali yeyote yule anayetaka
kufanikiwa kimaisha anavyoweza akajifunza kutoka kwa bingwa mweusi mashuhuri
zaidi wa ngumi aliyewahi kutokea Duniani na mwanamichezo wa karne ya 20.
Roho ya kutokukata tamaa kamwe, uvumilivu, Nidhamu ya
hali ya juu na Ujasiri vilimfanya Muhammad Ali kuvishinda vikwazo nje na ndani
ya ulingo. Vikwazo vya kubaguliwa, kuchukiwa, kudharauliwa kwa sababu ya rangi
na dini hasa na watu weupe.
Muhammad
Ali wakitaniana na bondia mwenzake Nelson Mandela walipokutana mwaka 2005.
Mandela aliwahi kuwa bondia zamani.
|
Muhammad Ali alipoanza mazoezi miaka ya 50 alikuwa ni mtu
mwenye nidhamu ya hali ya juu kwenye mazoezi yenyewe, chakula alichokula, na
hata kwa waalimu waliomfundisha. Aliweza kujizuia kunywa pombe, kuvuta sigara
na vyakula vya mafuta mengi na sukari ambavyo alikuwa akivipenda. Nukuu yake
maarufu inasema hivi;
“Yeyote
yule asiyekuwa na Ujasiri wa kutosha kuchukua hatari, kamwe hataweza
kufanikisha chochote maishani.”- Muhammad Ali
Ingawa Muhammad Ali alichukiwa sana na jamii hasa ya watu
weupe, lakini mwishowe baada ya kushinda mataji ya ngumi ya Dunia mara tatu mfululizo, kila mtu alikuja kumkubali na huu ni
uthibitisho kwamba;
“Mtu yeyote yule anaweza kuwa chochote kile anachotamani kuwa, endapo tu ataweka jitihada za kutosha na wala haijalishi ana imani gani, kabila gani au ni rangi gani, kila kitu kinawezekana chini ya jua”- Peter
“Mtu yeyote yule anaweza kuwa chochote kile anachotamani kuwa, endapo tu ataweka jitihada za kutosha na wala haijalishi ana imani gani, kabila gani au ni rangi gani, kila kitu kinawezekana chini ya jua”- Peter
Raisi Barack Obama akitoa salamu zake za rambirambi baada
ya kifo cha Muhammad Ali hapo siku ya tarehe 3 june 2016 akiwa na umri wa miaka
74, Obama alitamka maneno yafuatayo;
“Muhammad
Ali alikuwa Mkuu….mtu aliyetupigania. Alisimama na akina King na Mandela
kipindi kilichokuwa kigumu, akiongea pale wengine waliposhindwa kuongea.
Mapambano yake nje ya ulingo yalimgharimu taji lake na msimamo wake hadharani.
Yaliweza hata kumjengea maadui kulia na kushoto, na hata kukaribia kumpeleka
jela. Lakini Ali alisimama kidete, na ushindi wake umetusaidia kuwa na Marekani
tunayoiona leo.”- Barack Obama.
Kama ilivyokuwa kwa binadamu mwingine yeyote yule, hakuna
kizuri kisichokuwa na kasoro na shilingi ni lazima iwe na pande zote mbili,
Muhammad Ali hakuwa mkamilifu alikuwa na mapungufu yake, kubwa likiwa ni tabia yake ya
kuwatukana maadui zake na kuwatolea maneno makali hata pale alipokuwa ulingoni.
Hata hivyo, ubaya wake wote huo ulifunikwa kabisa na mazuri aliyoyafanya huku
maadui zake wengi wakijikuta wanakuwa mashabiki wake wakubwa.
Hata miaka yake ya mwisho aligeuka na kuwa balozi mkubwa wa amani na maridhiano duniani kote baina ya pande zote zinazokinzana siyo tu katika siasa bali na katika imani, dini na matabaka mbalimbali.
Hata miaka yake ya mwisho aligeuka na kuwa balozi mkubwa wa amani na maridhiano duniani kote baina ya pande zote zinazokinzana siyo tu katika siasa bali na katika imani, dini na matabaka mbalimbali.
Pambano
la ngumi za uzito wa juu mashuhuri zaidi Duniani kati ya Muhammad Ali na George
Foreman Kinshasa nchini Zaire Congo(DRC) “Rumble
in the jungle” mwaka 1974.
Muhammad Ali akimwangusha chini Foreman. |
Pambano la ngumi kati ya mfalme wa ngumi Duniani,
Muhammad Ali na George Foreman(Ramble in the Jungle) lililofanyika
jijini Kinshasa Zaire(Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa) mwaka 1974 ndilo
pambano la ngumi la uzani wa juu mashuhuri zaidi kuwahi kufanyika Duniani.
Sababu za pambano hilo kuwa mashuhuri kiasi hicho
zinatokana na ukweli kwamba lilikuwa ni baina ya mabondia wawili mashuhuri na
ambao sifa zao zilitofautiana. Foreman akionekana kama mzalendo aliyekuwa
ametoka kuliwakilisha Taifa lake katika michuano ya Olimpiki na kurudi akiwa na
medali ya dhahabu, huku Muhammad Alli yeye akichukuliwa kama bingwa mweusi
ambaye alikuwa amegadhabishwa mno na tabia ya watu weupe ya kuwadharau na
kuwabagua watu weusi.
Sababu hizo ndizo hata zilizomfanya Muhammad Alli ambaye
hapo awali alijulikana kama Cassius Clay kubadilisha dini kutoka Ukristo kwenda
Uislamu. Hadi kufikia katikati ya mwaka 1974, Muhammad Alli alikuwa
ameshawapiga mabondia wote wa uzani wa juu na sasa pambano lake hili na Foreman
alitaka aendelee kuwa bingwa. Kwa upande wa mafanikio katika kipindi hicho basi
angeweza kuwa wa pili baada ya Floyd Patterson.
Madai ya meneja wake kutaka bondia wake Muhammad Alli
alipwe jumla ya dola million tano yalimshitua sana mdhamini wa pambano hilo Don
King ambaye hapo kabla hakuwa amewahi hata siku moja kudhamini pambano la pesa
nyingi kiasi hicho. Hata hivyo Don King aliahidi kufanya kila lililowezekana
kuzipata pesa hizo.
Kwa kutumia ujanja na mbinu mbalimbali katika mkanda wa
video alioutuma kwa aliyekuwa Raisi wa Zaire, Dikteta Mobutu Seseseko,
alifanikiwa kumshawishi mpaka akakubali kutoa dola milioni 10 ambazo zilitosha
kuwalipa mabondia wote wawili. Kiasi kingine kilichobakia kufanikisha pambano
hilo ilitoa kampuni moja ya Kiingereza.
Mobutu ni mtu aliyependa sana sifa na kwa hivyo aliliona
pambano lile kuwa lingeitangaza nchi yake na yeye mwenyewe Dunia nzima. Tabia
yake ya kuutukuza Uzungu ilimfanya aibatize Zaire “Ubelgiji ya Congo”. Kuna
wakati aliwahi kuwafungia wahalifu 300 katika uwanja mmoja wa michezo kisha
akaamuru wauwawe 50, na waliosalia waachiwe wakawasimulie raia wengine. Kwa
mtindo wake huo, Zaire ilifikia mahali ikawa na kiwango cha chini sana cha
uhalifu.
Tukirudi katika pambano, Foreman alikuwa ni bondia mwenye
uwezo mkubwa, katika raundi za pili tu za mwanzo, alikuwa ameshawatoa kwa ‘Knok
out’ wapinzani wake mara 8; na kati ya mapambano yake 40 alikuwa
ameshashinda 37.
Muhammad Alli baada ya kujiandaa vilivyo kambini kwake
huko Pennisylvania, alisafiri na kuwasili Zaire wiki mbili kabla ya mpambano
kusudi apate muda wa kutosha kuyazoea mazingira. Alichagua nyumba iliyokuwa
maeneo ya nje kidogo ya jiji la Kinshasa kama kilomita 40 hivi.
Foreman pamoja na wapambe wake, wao walichagua nyumba eneo
katikati ya jiji la Kinshasa. Kutokupendelea kwake kutembelewa na wageni wasio rasmi
kulimfanya amuweke mbwa getini wa kulinda. Muhammad Alli kwa upande wake
aliitumia kila fursa aliyoipata kuwa karibu na watu akidhihirisha mapenzi yake
kwa Uafrika.
Kila alikoenda alizungukwa na kundi kubwa la watu. Siku
nne kabla ya pambano Foreman aliumia juu ya jicho lake ikabidi pambano
liahirishwe mpaka Oktoba 30, jambo
lililosababisha kuwe na tetesi kuwa Mobutu alikuwa amewazuia kuondoka nchini
humo.
Hatimaye Foreman alipona na “miamba” hao wawili wakaingia ulingoni mwezi Mei 20 1974 majira ya
saa 10 za usiku za huko Afrika ya Kati. Ulipangwa muda huo kusudi uweze
kuendana sawasawa na muda wa jioni kule Marekani ambako watu walikuwa
wakisubiri kwa shauku kubwa kuushuhudia mpambao huo wa kukata na shoka katika
televisheni zao.
Uzito wa Foreman uliuzidi ule wa Muhammad kwa paund
kadhaa, kabla ya raundi ya kwanza kuanza watu walikuwa wakiimba kwa vifijo
nyimbo za kumshangilia Muhammad Alli,
walitamka maneno “Boma Yee……” Wakimaanisha , “Alli muue Foreman…..!”
Katika raundi ya kwanza Muhammad Alli aliachia makonde
mfululizo akitumia mikono yote miwili, staili ambayo kwa kawaida mabondia
huitumia mwishoni mwa mchezo mpinzani anapokuwa ameshachoka.
Mbinu hiyo ilizaa matunda lakini hata hivyo Foreman naye
akajibu mashambulizi kwa kurusha makonde kadhaa ya nguvu. Katika raundi ya
pili, Foreman alimkimbiza Muhammad na kumlazimisha arudi hadi kwenye kona.
Muhammad pale kwenye kona aliamua kubadili mbinu na
kuanza kubakia kwenye kamba muda wote. Aliiegemea kamba kwa nyuma jambo
lililomfanya Foreman amfuate, Muhammad alirudi mbele na kumpa kipigo tena na
tena.
Katika dakika za mwisho za raundi hiyo, Muhammad alikuja
juu kwa kasi ya ajabu na kuutikisa kwa makonde mazito mwili wa Foreman uliokuwa
umeshaanza kuchoka.
Raundi za sita na saba zilienda taratibu huku Foreman
akijaribu bila mafanikio kumtoa Muhammad kwa ‘knok out’. Karibu na
mwishoni mwa raundi ya nane Muhammad alikusanya nguvu zake zote na ujasiri,
akajitayarisha kurusha ngumi ya mkono wa kushoto! Kila mtu alifikiri lile ndilo lingekuwa
shambulio la mwisho.
Badala yake, Muhammad aliachia ngumi ya mkono wa kulia
iliyomwacha Foreman na kamba ya ulingo wakigaagaa kwa mpepesuko.
Muhammad alimpokelea kwa mikono yote miwili huku
akimimina makonde mfululizo, akiitumia ile staili aliyokuwa ameanza nayo katika
raundi ya kwanza.
Konde moja zito lilitua sawia katikati ya paji la uso wa
Foreman likamfanya aruke kwa kupepesa mikono mithili ya “parachute” linapochomoka ndani ya ndege inayotaka
kuanguka.
SOMA: Mabuti ya Nelson Mandela aliyosahau Tanzania mwaka 1962 haya hapa.
SOMA: Mabuti ya Nelson Mandela aliyosahau Tanzania mwaka 1962 haya hapa.
Washangiliaji walishikwa na uwendawazimu! Muhammad Alli
alikuwa ameshinda tena kwa mara ya pili ubingwa wa Dunia wa ngumi za uzito wa
juu kwa staili iliyowaacha watu hoi na kuwastaajabisha.
Dakika moja baadaye Mbingu zilimimina mvua kubwa
iliyoambatana na ngurumo na radi. Mvua hiyo kama ingelikuwa imenyesha kabla ya
pambano ingelilazimu liahirishwe tena.
Vyanzo: Tovuti na mitandao mbalimbali.
Vyanzo: Tovuti na mitandao mbalimbali.
0 Response to "MUHAMMAD ALI: UVUMILIVU, NIDHAMU, UJASIRI, MSIMAMO VILIMPA UBINGWA KINSHASA ZAIRE"
Post a Comment