Katika zama zote, viongozi wa dini wamekuwa wakionya,
mapambano ya mwanadamu “kuwa na Imani” katika hili, lile na imani au dini
nyingine, lakini wameshindwa kuwaeleza watu namna
ya kuwa na imani. Hawajaeleza kuwa imani ni hali ya akili, na kwamba inaweza
ikaanzishwa kwa njia ya kujishauri binafsi.
Katika lugha mtu yeyote wa kawaida anayoweza akaelewa
tutaelezea kila kinachofahamika kuhusiana na kanuni ambazo kupitia hizo, imani inaweza ikakuzwa mahali ambapo
haikuwepo tayari.
Kuwa na Imani ndani yako mwenyewe; Imani katika umilele.
Kabla hatujaanza, unapaswa kukumbushwa tena yakwamba:
IMANI
ni “suluhisho la peponi” litoalo uhai, nguvu na vitendo kwa msukumo wa fikra!
Sentensi ifuatayo inastahili kusomwa kwa mara ya pili, na
ya tatu, na ya nne, inastahili kusomwa kwa sauti!
IMANI ni mwanzo wa malimbikizo yote ya utajiri!
IMANI ni msingi wa “miujiza” na maajabu yote ambayo
hayawezi yakachanganuliwa kwa kanuni za sayansi !
IMANI ni kiua-sumu pekee kinachojulikana cha MAANGUKO !
IMANI ni kiasili, “kemikali” ambayo inapochanganywa na
sala, humpa mtu mawasiliano ya moja kwa moja na nguvu kuu ya asili.
IMANI ni kiungo kinachobadilisha mtetemo wa kawaida wa
fikra, unaotengenezwa na akili ya kawaida ya mtu kwenda katika hali ya kiroho
iliyokuwa na ukubwa sawasawa nao.
IMANI ni wakala pekee
ambaye kupitia kwake nguvu kuu za kiulimwengu zisizokuwa na mwisho
zinaweza zikavunwa na kutumiwa.
KILA
MMOJA, KATIKA KAULI ZIFUATAZO ANAO UWEZO WA KUTHIBITISHA !
Uthibitisho ni rahisi na mwepesi kufafanuliwa.
Umefungashwa katika kanuni ya kujishauribinafsi. Kwa hiyo, hebu tuelekeze
umakini wetu katika somo la kujishauribinafsi, na kuona ni kitu gani
kinachoweza kufikiwa.
Ni ukweli unaofahamika vizuri kwamba mtu mwishowe huja kuamini chochote kile anachorudiarudia
mwenyewe, iwe ni kauli ya ukweli ama ya uwongo. Ikiwa mtu atarudia uwongo tena
na tena, uwongo mwishowe utakubalika kama ukweli.
Zaidi ya hapo, utasadikiwa
kuwa ukweli. Kila mmoja wetu tupo kama tulivyo kutokana na fikra zinazotawala tunazoziruhusu kuwa katika akili zetu. Fikra
ambazo zimewekwa kwa makusudi katika akili zetu wenyewe na kuchochewa na huruma,
na zikichanganywa na mhemko wowote mmoja au zaidi huwa na nguvu za kiushawishi.
Nguvu hizi huongoza na kuthibiti kila shughuli zetu, matendo tunayoyatenda kwa
kujua au kwa kutojua !
FIKRA
ZINAZOCHANGANYWA NA HISIA ZOZOTE AU MIHEMKO HUWA NA NGUVU ZA “USUMAKU” AMBAZO
HUVUTA, KUTOKA KATIKA MITETEMO YA ANGANI FIKRA ZINAZOFANANA AU ZENYE UHUSIANO
NAYO.
Hivyo Wazo “lililosumakishwa” kwa mhemko linaweza
likalinganishwa na mbegu ambayo wakati inapopandwa katika ardhi yenye rutuba,
humea, kukua na kuongezeka yenyewe tena na tena mpaka ile mbegu moja ndogo
inapogeuka kuwa mamilioni ya mbegu zisizohesabika za aina moja !
Anga(ether) ni mkusanyiko mkubwa wa kiulimwengu wa nguvu
za kimtetemo zisizokuwa na mwisho.Limeumbwa kwa vitu viwili, mitetemo hasi na
mitetemo chanya. Wakati wote, hubeba mitetemo ya woga, umasikini, magojwa,
kushindwa, mateso na mitetemo ya utajiri, afya, mafanikio na furaha. Hufanya
hivi, kiukweli tu kama inavyokuwa linavyobeba sauti za mamia ya bendi za muziki
na mamia ya sauti za binadamu, wote wakidumisha upekee wao na jinsi ya
kujitambulisha kupitia chombo cha redio.
Kutoka kwenye stoo kubwa ya anga(ether), akili ya
binadamu mara zote huvuta mitetemo ile inayoendana sawa na kile kinachotawala akilini kwa wakati huo.
Fikra yeyote, wazo, mpango au lengo ambalo mtu anakuwa nalo akilini, huvuta
kutoka kwenye mtetemo wa anga mwenyeji wa mawazo yanayofanana nayo(mawazo ndugu).
Huwaongeza hawa ‘ndugu’ katika nguvu zake yenyewe na kukua mpaka kuwa “bwana
mshawishi” anayetawala katika akili ya mtu wazo lilipohifadhiwa.
Sasa hebu turudi nyuma mwanzoni na kuangalia ni kwa namna
gani mbegu ya mwanzo ya wazo, mpango au lengo inaweza ikapandwa akilini kupitia
kurudiwarudiwa kwa fikra. Hii ndiyo sababu unashauriwa kuandika kauli ya lengo
lako kuu au kuelezea dhamira kuu, kuihifadhi akilini na kuirudiarudia-ukitamka
kwa sauti, siku baada ya siku-mpaka hii mitetemo ya sauti imefika ndani ya
akili yako ya ndani.
Sisi tupo kama tulivyo kwa sababu ya mitetemo ya fikra
ambayo tunaichukua na kuisajili kupitia vichocheo vya mazingira yetu ya kila
siku.
Nuwia kuachana na ushawishi wa mazingira yeyote yale hasi
na kujenga maisha yako mwenyewe katika mstari
mzuri. Piga hesabu ya nguvu na udhaifu wa akili, utagundua kwamba, udhaifu wako
mkubwa kabisa ni kukosa kujiamini binafsi. Kilema hiki kinaweza kikazidiwa
nguvu na kutishwa kiurahisi na kugeuzwa kuwa ujasiri kwa kupitia kanuni ya
kujishauribinafsi.
Matumizi ya kanuni hii, yanaweza yakafanywa kupitia
mpangilio rahisi wa msukumo chanya wa fikra iliyoelezwa katika maandishi,
ikatiwa akilini na kurudiwarudiwa mpaka yanakuwa sehemu ya zana za kufanyia
kazi za kitivo cha mawazo ya ndani ya akili yako.
Kanuni
Ya Kujiamini Binafsi.
1. Ninafahamu kwamba ninao uwezo wa kutimiza lengo langu
kuu katika maisha. Kwahiyo ninahitaji uvumilivu wangu mwenyewe, vitendo mfululizo
kuelekea kulikamilisha, na mimi hapa na sasa naahidi kuchukua hatua hiyo.
2. Natambua mawazo yanayotawala akili yangu, mwishowe yatajizalisha
yenyewe kuwa vitendo halisi na taratibu kujigeuza yenyewe kuwa ukweli halisi. Kwahiyo
nitayaelekeza mawazo yangu yote kwa dakika 30 kila siku kwenye zoezi la kumfikiria
mtu ninayetamani niwe, hivyo kutengeneza akilini mwangu picha halisi ya mtu huyo.
3. Najua kupitia kanuni ya kujishauribinafsi kwamba Shauku
yeyote ninayoendelea kuibeba akilini mwangu pasipo kuchoka mwisho wake itatafuta
kujibainisha kupitia baadhi ya njia za kivitendo za kutimiza lengo. Kwa hiyo nitatenga
muda wa dakika 10 kila siku kunifanya mimi mwenyewe kukuza kujiamini-binafsi
4. Nimeandika kwa ufasaha maelezo ya lengo langu kuu halisi maishani. Kamwe sitaacha kujaribu
mpaka nimekuza vya kutosha kujiamini binafsi katika kulifikia.
5. Ninatambua kabisa kwamba hakuna utajiri wala nafasi inayoweza
ikadumu muda mrefu pasipo kujengwa juu ya ukweli na haki. Kwa hiyo sitaingia katika makubaliano
ambayo hayatakuwa na faida kwa pande zote zinazohusika. Nitafanikiwa kwa kuvutia
kwangu mwenyewe nguvu ninazotamani kuzitumia na ushirikiano wa watu wengine.
Nitawashawishi
wengine kunitumikia kwasababu ya utayari wangu wa kuwatumikia wengine. Nitaondosha
chuki, husuda, wivu, ubinafsi na bezo kwa kukuza upendo kwa binadamu wote kwasababu
najua kwamba mtazamo hasi dhidi ya wengine kamwe hautaweza kuniletea mafanikio.
Nitawafanya wengine kuniamini kwa sababu pia nitawaamini na
kujiamini. Nitasaini jina langu katika kanuni hii, kuiweka akilini na kuirudiarudia
kwa sauti kila siku mara moja, kwa imani
kamili kwamba, taratibu itayaathiri mawazo
na vitendo vyangu kusudi nije kujitegemea
mwenyewe na kuwa mtu mwenye mafanikio.
0 Response to "NGUVU NA UDHAIFU WA AKILI YAKO, HUTOKANA NA KUJIAMINI BINAFSI AU KUKOSA KUJIAMINI"
Post a Comment