WANASAYANSI WAGUNDUA DAWA MPYA YA KUUWA VIRUSI VYA UKIMWI VILIVYOJIFICHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WANASAYANSI WAGUNDUA DAWA MPYA YA KUUWA VIRUSI VYA UKIMWI VILIVYOJIFICHA


Tatizo la ugonjwa wa ukimwi kutokutibika kabisa na badala yake waathirika kutumia dawa za kurefusha maisha huenda sasa likawa ni historia baada ya wanasayansi huko nchini Uingereza kugundua dawa ambayo ina viasili vya aina mbili, kiasili kimoja kina uwezo wa kuviamsha virusi vinavyokuwa vimejichimbia katika seli za mwili na ambavyo hujifanya vimekufa kumbe bado vingali hai na huja kuamka baada ya mwathirika kuacha kutumia dawa za kurefusha muda(ARVs). 
Picha inayoonyesha kirusi cha ukimwi(HIV)
Baada ya kiasili hicho kuvizindua virusi vya HIV vilivyolala, kiasili cha pili chenye dawa iliyokuwa na uwezo wa kuviangamiza  hufanya kazi yake na hatimaye kuvisafisha kabisa virusi hivyo hatari zaidi kwa binadamu.

Soma: MSANII ALIYEACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA 'ARVS'

Soma: CHANJO INAYOMALIZA KABISA VIRUSI VYA UKIMWI.

0 Response to "WANASAYANSI WAGUNDUA DAWA MPYA YA KUUWA VIRUSI VYA UKIMWI VILIVYOJIFICHA"

Post a Comment