Ndugu msomaji natumaini hapo ulipo unasonga mbele licha
ya vikwazo vya hapa na pale ambavyo vinaweza kukukatisha tamaa katika safari
yako ya kuelekea maisha mazuri yenye mafanikio. Makala hii ni maalumu kwa
kukutia moyo endapo labda utafika mahali na kudhani kwamba kila kitu
hakiwezekani, ukakata tamaa na kufikia hata hatua ya kujidhuru.
SOMA: MAMA HUBEBA MTOTO TUMBONI MIEZI 9 LAKINI HUMBEBA MOYONI MILELE.
SOMA: MAMA HUBEBA MTOTO TUMBONI MIEZI 9 LAKINI HUMBEBA MOYONI MILELE.
Kama mjasiriamali, kuna vitu 4 vinne muhimu sana ambavyo
unaweza ukavitumia na ikawa ndiyo dawa itakayokomesha kabisa hali ya kukata
tamaa inayoweza kukusababisha usiweze kuyafikia malengo yako unayojiwekea
maishani. Ipo mifano ya watu wengi waliovitumia na wakaweza kufanikiwa.
IMANI.
Chochote kile ukifanyacho ni lazima kwanza uamini kwamba
kitu hicho kitawezekana hata kabla hujatekeleza. Imani hiyo ndiyo iliyokuwa
muhimu na ndiyo nguvu itakayokuchochea wewe kutimiza hilo unalolipanga kufanya.
Mfano mzuri kabisa na uliokuwa wazi ni imani za dini na madhehebu mbalimbali.
Waumini wake pamoja na kwamba hawana ushahidi wa moja kwa moja kuwa kuna maisha
baada ya kifo, lakini IMANI huwafanya waendelee kusadiki hivyo bila kuchoka.
SOMA: UPENDO WA WAZAZI HAUNA MIPAKA, NI "UNCONDITIONAL LOVE"
SOMA: UPENDO WA WAZAZI HAUNA MIPAKA, NI "UNCONDITIONAL LOVE"
SUBIRA.
Ni mara ngapi umewahi kukata tamaa na kusita kufanya
jambo fulani, kumbe mafanikio yake, ulibakia muda kidogo sana uyapate? Katika
sura ya kwanza 1 ya kitabu “Fikiri
Utajirike(Msahafu wa mafanikio)” Kuna simulizi moja maarufu ya mchimba
madini aliyejulikana kama Darby, huyu jamaa baada ya kupata habari kuwa
yameibuka machimbo ya dhahabu eneo moja huko Magharibi mwa Marekani, (kama
ilivyokuwa hapa kwetu, machimbo ya Tunduru na kwingineko kama Samunge) basi
bwana huyu akazunguka kwa kila ndugu na jamaa kukopa mtaji aende kubahatisha
bahati yake mgodini ikiwa ni pamoja na kuuza kila kitu chake cha dhamani kusudi
tu apate mtaji.
Darby alianza kazi ya kuchimba dhahabu kwa matumaini
makubwa lakini baada ya muda kupita na kuona hamna mafanikio makubwa haraka,
alikosa subira, akakata tamaa na kuamua kumuuzia dalali mmoja wa vyuma ule
mgodi, yeye akarudi zake mjini. Madalali kama iulivyokuwa kawaida yao ni
wajanja mno kwenye pesa!, alimtafuta injinia(mhandisi wa madini) akaomba
ushauri.
Injinia baada ya kupima pima alimwambia bamba la dhahabu lilikuwa futi tatu 3 tu! kutoka pale Darby alipoachia kuchimba baada ya kukata tamaa. Kilichofuata baada ya hapo ndugu msomaji wangu nadhani unaweza kubashiri mwenyewe. Unaweza ukakisoma kisa/simulizi hiyo vizuri kwa kubonyeza maandishi yafuatayo, Futi tatu tu, kutoka dhahabu ilipo!
Injinia baada ya kupima pima alimwambia bamba la dhahabu lilikuwa futi tatu 3 tu! kutoka pale Darby alipoachia kuchimba baada ya kukata tamaa. Kilichofuata baada ya hapo ndugu msomaji wangu nadhani unaweza kubashiri mwenyewe. Unaweza ukakisoma kisa/simulizi hiyo vizuri kwa kubonyeza maandishi yafuatayo, Futi tatu tu, kutoka dhahabu ilipo!
UVUMILIVU.
Kama ilivyokuwa Subira, uvumilivu nao kwenye maisha unahitajika
sana. Mchimba dhahabu bwana Darby, hakuwa navyo vyote viwili, uvumilivu na
subira. Kuna kisa kingine cha kweli katika kitabu hichohicho. Bila shaka katika
nyumba unamoishi, kila siku usiku ni lazima uwashe taa ya umeme au balbu.
Unajua mgunduzi wa taa hiyo, Thomas Edson alijaribu mara ngapi kabla hajaigundua?.
Alijaribu mara 9,999 ya 10,000 ndipo
alipofanikiwa! Ungelikuwa ni wewe ungeliachia wapi?, Kwa upande wangu nafikiri
hata mara ya 20 nisingefikisha.
Na isitoshe Edison mwenyewe alipohojiwa alikuwa
anajisikiaje kufeli mara zaidi ya elfu 9, alijibu hivi; “Nafurahi nimegundua
njia 9,999 zisizofaa kugundua balbu”
MUDA.
Muda ndiyo kiunganishi katika hivyo vitu vingine vyote
vitatu, Imani, Uvumilivu na Subira katika safari ya mtu kupata mafanikio.
Hakuna mafanikio yanayoweza yakapatikana ndani ya kipindi kifupi kama siku
moja, mbili, au tatu labda iwe ni kamari. Yanahitaji muda wa kutosha, hata
unapopanda mazao kama vile mahindi huwezi ukategemea kuyavuna kabla ya muda
wake kutimia. Watu wengi hukatishwa tamaa wanapofikiria muda waliokwisha
upoteza kwenye miradi/shughuli fulani lakini wanashindwa kukumbuka kuwa
mafanikio yeyote yale yanahitaji muda kuyatimiza na muda wenyewe ni lazima uwe
wa kutosha.
SOMA: NI UA ZURI NA HATARI SANA!, LINA UWEZO WA KUUA MTOTO HARAKA.
SOMA: NI UA ZURI NA HATARI SANA!, LINA UWEZO WA KUUA MTOTO HARAKA.
Mafanikio ya aina yeyote yale unayojaribu “kuyapika”
katika maisha yako ya thamani hapa duniani, hakikisha viungo hivi vinne, IMANI,
SUBIRA, UVUMILIVU NA MUDA havikosekani katika “chungu unachotumia kuchemshia
mafanikio hayo.” Na hasa hasa Imani, kwani ikiwa kama hauta amini kwa thati
kabisa kuwa unalolitaka liwe litakuwa, basi sahau mafanikio kabisa.
Mwisho, usikate tamaa kamwe, jipe tena nafasi nyingine ya
kujaribu na inaweza ikawa ndiyo mara yako ya 10,000 kama ilivyokuwa kwa Thomas
Edison, mvumbuzi wa glopu ya umeme.
Nakutakia kila la heri katika safari yako ya kutimiza
malengo uliyojiwekea maishani na kama bado hujajiweka malengo ama hufahamu
jinsi ya kujiwekea malengo mazuri, basi nakushauri ujipatie kitabu hiki
kilichobadilisha maisha ya watu wengi waliobahatika kukisoma. Bonyeza maandishi
yafuatayo kupata kitabu hicho; “MIFEREJI YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA”
Mwandishi na Mhamasishaji wako;
Peter A. Tarimo.
Mwandishi na Mhamasishaji wako;
Peter A. Tarimo.
0 Response to "PUNDE KABLA HUJAKATA TAMAA YA MAISHA SOMA VITU HIVI 4 UTABADILI NIA"
Post a Comment