KUJISHAURI BINAFSI
NJIA
YA KUSHAWISHI AKILI YA NDANI.
(Hatua
ya tatu kuelekea utajiri)
Kujiashauri binafsi ni neno linalotumika kwa
mawazo yote na vichocheo vyote vinavyosimamiwa binafsi ambavyo hufika katika
akili ya mtu kupitia milango mitano ya fahamu. Kwa lugha nyingine, kujishauribinafsi
ni kujiingizia mawazo akilini mwenyewe.
Ni wakala wa mawasiliano kati ya ile sehemu
ya akili ambapo fikra za fahamu hutokea na ambayo huhudumu kama kiti cha
vitendo kwa ajili ya akili ya ndani. Kupitia mawazo yanayotawala, mtu huruhusu
kubakia katika ufahamu(iwe mawazo hayo ni hasi au chanya haijalishi), kanuni ya
kujishauribinafsi kwa hiyari huifikia akili ya ndani na kuiathiri kwa mawazo
hayo.
Ukiacha fikra(mawazo) yanayochukuliwa kutoka
angani(ether), hakuna mawazo yawe ni chanya ama hasi, YANAYOWEZA KUINGIA AKILI
YA NDANI BILA MSAADA WA KANUNI HII YA KUJISHAURIBINAFSI. Kwa maneno mengine,
maono yote ya fahamu ambayo hutambuliwa kupitia milango mitano ya fahamu
huzuiliwa na akili ya kawaida ya
kufikiria na yanaweza, aidha kupitishwa kwenda katika akili ya ndani au
kukataliwa kwa hiyari. Kwa hiyo kitivo cha akili ya nje ya kawaida huhudumu kama mlinzi wa nje dhidi ya
kuikaribia akili ya ndani.
Hivyo asili imetujenga sisi kwamba tunao udhibiti wote juu ya kitu kinachoingia
katika akili yetu ya ndani kupitia milango 5 ya fahamu ingawa hii haina maana
kutafsiriwa kama kauli kwamba kila mara tunatekeleza udhibiti huu. Kwa upande
mwingine mara nyingi sana huwa hatuitekelezi na hiyo ndiyo sababu kwanini watu
wengi kiasi hicho hupitia maisha ya umasikini.
Kumbuka kile kilichokwisha semwa juu ya akili
ya ndani kufanana na bustani yenye rutuba ambayo magugu yataota kwa wingi ikiwa
mbegu za mazao mazuri hazitapandwa pale. Kujishauri binafsi ni wakala wa uthibiti
ambaye kupitia yeye mtu kwa hiyari
huilisha akili ya ndani fikra zenye asii ya kujenga au kwa kutokujali, kuruhusu
fikra zenye asili ya kubomoa kuingia katika bustani hii tajiri ya akili.
Ulifundishwa katika hatua ya mwisho ya hatua
sita zilizoelezwa katika sura ya 2, kusoma kwa sauti mara mbili kwa siku kauli
iliyoandikwa ya shauku yako kwa pesa, na kuona na kuhisi mwenyewe tayari ukiwa
unamiliki hizo pesa. Kwa kufuata maelekezo haya, unawasilisha nia ya shauku yako moja kwa moja kwenye akili ya ndani katika roho ya imani
kamilifu. Kupitia kurudiarudia kwa njia hii kwa hiyari unatengeneza tabia za
mawazo zinazoendana na juhudi zako kubadilisha shauku kuwa katika kiasi cha
fedha kinacholingana nayo.
Rudi katika hatua hizi sita zilizoelezwa
katika sura ya 2, na uzisome tena kwa uangalifu kabla hujaendelea zaidi. Kisha
(utakapoikuta), soma kwa makini sana hatua nne kwa ajili ya kuunganisha kundi lako la kushauriana(mastermind group)
zilizoelezwa katika sura ya 7. Kwa kulinganisha hatua hizi mbili za mafunzo na
zile zilizoelezwa kwenye kujishauri binafsi, utaona kwamba mafundisho
huhusisha matumizi ya kujishauribinafsi.
Kwahiyo kumbuka , wakati unaposoma kwa sauti
ile kauli ya shauku(ambayo kupitia hiyo unajitahidi kukuza “ufahamu wa pesa”),
kwamba kusoma tu peke yake hakuleti matunda yeyote ikiwa hautachanganya mhemko
wa hisia na maneno yako. Ikiwa utarudia mara elfu kanuni maarufu ya Emil Coue
isemayo, “Siku baada ya siku, katika kila
hali, naendelea kuwa bora zaidi”, pasipo kuchanganya mhemko wa imani na maneno hayo, hautapata matokeo
mazuri.
Akili yako ya ndani hutambua na kufanyia kazi
tu yale mawazo yanayochanganywa na
mhemko wa hisia. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa kuhalalisha kitendo cha
kurudiarudia katika kila sura. Ukosefu wa uelewa wa hili ndiyo sababu kubwa ya
watu wengi wanaojaribu kutumia kanuni ya kujishauribinafsi kutopata matokeo
mazuri.
Maneno matupu yasiyokuwa na hisia hayawezi
kushawishi akilli ya ndani. Hutapata matokeo makubwa, mpaka utakapojifunza
kuifikia akili yako ya ndani na mawazo au maneno yaliyotamkwa vizuri kwa hisia
na imani. Usikatishwe tamaa kama
huwezi kudhibiti na kuongoza hisia zako mara ya kwanza unapojaribu kufanya hivyo. Kumbuka hakuna uwezekano kama huo wa kupata
kitu pasipo kutoa kitu chochote, uwezo wa kuifikia na kuishawishi akili
yako ya ndani una gharama yake na ni lazima
ulipe gharama hiyo. Hauwezi ukadanganya , hata kama unatamani kufanya
hivyo.
Gharama ya uwezo wa kuishawishi akili yako ya ndani ni msimamo usiokuwa na kikomo katika kuzitumia kanuni zilizoelezwa hapa. Huwezi ukatengeneza uwezo unaotarajiwa kwa gharama ya chini. Wewe na ni wewe mwenyewe unayepaswa kuamua ikiwa malipo kwa kile unachohangaikia(utambuzi wa pesa) yanalingana au hayalingani na gharama ya nguvu unayolazimika kulipa katika jitihada.
Gharama ya uwezo wa kuishawishi akili yako ya ndani ni msimamo usiokuwa na kikomo katika kuzitumia kanuni zilizoelezwa hapa. Huwezi ukatengeneza uwezo unaotarajiwa kwa gharama ya chini. Wewe na ni wewe mwenyewe unayepaswa kuamua ikiwa malipo kwa kile unachohangaikia(utambuzi wa pesa) yanalingana au hayalingani na gharama ya nguvu unayolazimika kulipa katika jitihada.
Busara na ujanja peke yake havitavuta na
kutunza pesa isipokuwa katika nyakati chache sana ambapo kanuni ya
wastani(kadiri) huegemea upande wa kuvuta pesa kupitia vyanzo hivi. Njia ya
kuvuta pesa iliyoelezwa hapa haitegemei sheria ya kadiri. Zaidi njia hiyo huwa
haina upendeleo. Itafanya kazi vizuri kwa mtu mmoja kama itakavyofanya kazi kwa mtu mwingine.
Pale kushindwa kunapotokea, ni mtu mwenyewe, na siyo njia iliyomuangusha. Kama
utajaribu na kushindwa, fanya jitihada nyingine na nyingine tena, mpaka
umeshinda.
Uwezo wako wa kuitumia kanuni ya kujishauri
binafsi utategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wako wa kuelekeza nguvu zote pamoja(concentration)
kwenye shauku mpaka pale shauku hiyo inapogeuka kuwa jukumu muhimu zaidi.
Unapoanza kuchukua mafunzo kuhusiana na hatua sita zilizoelezwa katika sura ya
pili, itakuwa ni muhimu kwako kufanya matumizi ya sheria ya kuweka nguvu zote
pamoja.
Ngoja hapa tutoe ushauri wa matumizi bora ya kukusanya
nguvu zote pamoja(concentration). ‘Unapoanza kufanya hatua ya kwanza ya
zile hatua sita ambazo zinakuelekeza wewe’ “kukazia” katika akili yako mwenyewe
kiasi kamili cha pesa unazotamani,’
endelea kushika mawazo yako juu ya kiasi hicho cha pesa kwa kuelekezea
nguvu zote pamoja, au mkazo wa usikivu ukiwa umefumba macho yako, mpaka kweli utakapoona umbo halisi la pesa. Fanya hivyo angalao mara moja kila
siku. Kadri utakavyokuwa ukipitia zoezi hili, fuata maelekezo yaliyotolewa
katika sura ya Imani na kuona wewe mwenyewe kweli ukiwa unamiliki hizo pesa.
Huu ni ukweli dhahiri zaidi-akili ya ndani huchukua
maelekezo yeyote inayopewa katia roho ya
imani kamili na kufanyia kazi maelekezo hayo ingawa maelekezo mara nyingi
yanapaswa kupewa tena na tena, kupitia kurudiwarudiwa, kabla hayajatafsiriwa na
akili ya ndani. Zingatia uwezekano wa kucheza “mbinu” halali kamilifu kwenye
akili yako ya ndani kwa kuifanya iamini- kwa kuwa unaiamini - kwamba ni lazima
uwe na kiasi cha fedha unachokiona
akilini, kwamba fedha hizi tayari zinakusubiri uzichukue, kwamba akili ya ndani
ni lazima
ikupe mipango ya kivitendo kwa ajili ya
kupata pesa ambazo ni za kwako. Kabidhi wazo hili kwa akili yako ya ubunifu, na kuona ni nini ubunifu wako
unachoweza au utakaofanya kutengeneza
mipango ya kivitendo kwa ajili ya kupata fedha kupitia mageuzi ya shauku yako.
Usisubirie
mpango
kamili ambao kupitia huo ndio unaokusudia kubadilisha huduma ama bidhaa kwa
malipo ya fedha unazozifikiria akilini. Anza mara moja kujiona mwenyewe
ukimiliki hizo pesa, ukihitaji na kutegemea wakati huohuo kuwa akili yako
ya ndani itakabidhi mpango au mipango unayohitaji, kaa macho kwa hii mipango,
na wakati itakapotokea, itie katika vitendo mara moja. Yamkini itamulika ghafla
katika akili yako kupitia mlango fahamu wa sita, katika umbile la
“wahyi”(ufunuo), ufunuo huu unaweza ukachukuliwa kama ujumbe wa moja kwa moja
kutoka nguvu isiyokuwa na mipaka(Mungu). Itendee kwa heshima, na ifanyie kazi
haraka mara unapoipokea. Kukosa kufanya hivi, mafanikio yako yatakuwa kazi bure.
Katika hatua ya nne kati ya sita ulifundishwa
“kutengeneza mpango kamili kwa ajili ya kutekeleza shauku yako, na anza mara
moja kuuweka mpango katika vitendo, unapaswa kufuata haya maelekezo katika
mtindo ulioelezwa kwenye aya zilizotangulia. Usije ukaziamini fikra zako
unapotengeneza mpango wako. Fikra zako zina makosa. Na zaidi kitivo chako cha
kufikiri kinaweza kuwa kivivu, na ikiwa utakitegemea moja kwa moja kukuhudumia,
kinaweza kikakukatisha tamaa.
Unapowaza akilini fedha unayokusudia kuipata(ukiwa
umefumba macho), jione mwenyewe ukitoa huduma, au ukiuza bidhaa unazokusudia
kutoa kama malipo ya hizo feha. Hii ni muhimu!.
Muhtasari
wa mafundisho(maelekezo)
Ukweli kwamba unasoma kitabu hiki ni ishara kuwa
unatafuta maarifa kwa moyo wako wote. Pia ni ishara kwamba wewe ni mwanafunzi
wa somo hili. Ikiwa wewe ni mwanafunzi tu, kuna uwezekano unaweza ukajifunza
mengi, lakini utajifunza tu kwa kujijengea tabia ya unyenyekevu. Ikiwa
unachagua kufuata baadhi ya mafundisho lakini ukadharau ama kukataa kufuata
mengine, utafeli. Ili kupata matokeo ya kuridhisha ni lazima ufuate mafundisho yote katika roho ya imani
Mafundisho yanayotolewa yakihusishwa na hatua sita kwenye
sura ya 2 sasa yatafupishwa na kuchanganywa na kanuni zilizoelezwa katika sura
hii.
1. Nenda katika eneo lililokuwa kimya(inapendekezwa
kitandani wakati wa usiku) ambapo hautabugudhiwa au kukatishwa. Fumba macho
yako na rudia wa sauti (kiasi unachoweza kusikia maneno yako mwenyewe) kauli
iliyoandikwa ya kiasi cha pesa unachokusudia kukipata na maelezo ya huduma au
bidhaa unazokusudia kutoa kubadilishana na pesa.
Utakapokuwa ukitekeleza haya mafunzo, jione mwenyewe ukiwa tayari unamiliki
hizo pesa. Kwa mfano labda unakusudia
kupata $100,000 ifikapo tarehe 1 Januari, miaka mitano ijayo na kwamba
unakusudia kutoa huduma binafsi kama malipo kwa pesa hizo katika nafasi ya
mwakilishi wa mauzo. Kauli yako ya maandishi ya lengo lako inatakiwa ifanane na
hii ifuatayo;
“Ifikapo tarehe 1 January 20… nitakuwa namiliki $100,000
ambazo nitazipata katika viwango tofauti kutoka muda hadi muda ndani ya kipindi
hicho. Kama malipo kwa fedha hizi nitatoa huduma bora zaidi ambazo naweza
kuzitoa katika ukubwa na ubora wa kiwango cha juu kabisa kwa kadri
inavyowezekana kama mwakilishi wa mauzo wa(taja huduma au bidhaa unazokusudia
kuuza)
‘Ninaamini nitazimiliki hizi pesa . Imani yangu ni
thabiti kiasi kwamba sasa naweza kuziona hizi pesa mbele ya macho yangu. Naweza
kuzishika kwa mikono yangu. Sasa zinasubiri kuhamishiwa kwangu katika uwiano
ninaotoa huduma ninazokusudia kubadilishana nazo. Ninasubiri mpango
nitakaotumia kupata pesa hizi, na nitafuata mpango huo nitakapoupokea.
2. Rudia programu
hii usiku na asubuhi mpaka utakapoweza kuona(katika akili yako) pesa
unazokusudia kuzipata.
3. Weka nakala ya kauli ya maandishi mahali unapoweza
kuiona usiku na asubuhi. Isome mara kabla hujalala na wakati unapoamka mpaka
inakaa akilini.
Utakapokuwa ukitekeleza mafunzo haya, kumbuka kuwa
unatumia kanuni ya kujishauribinafsi kwa lengo la kutoa maelekezo kwa akili yako ya ndani, kumbuka pia kwamba
akili yako ya ndani itafanyia kazi tu
maelekezo yale yenye mhemko na yaliyokabidhiwa
kwake kwa “hisia”. Imani ndiyo mhemko
wenye nguvu kushinda yote na uliokuwa na faida zaidi. Fuata mafundisho
yaliyotolewa katika sura ya 3.
Mafunzo haya yanaweza, mwanzoni yakaonekana ni nadharia.
Usiliruhusu hili likusumbue. Yafuate vyovyote vile . Muda utafika haraka. Ikiwa
utafanya kama ulivyoagizwa katika roho na pia katika vitendo, ni wakati
Ulimwengu wote mpya wa nguvu utakapojifunua kwako. Kushuku kunakoambatana na
mawazo yote mapya, ni tabia ya
wanadamu wote. Lakini ikiwa utafuata maelekezo yaliyoorodheshwa haraka kushuku
kwako kutatawaliwa na imani, na hii
matokeo yake yatadhihirika haraka kama imani
kamili. Kisha utafika mahali
ambapo unaweza ukasema kweli, “Mimi ni
Bwana wa Majaaliwa yangu, mimi ni Kapteni wa Roho yangu”
Wanafilosofia wengi wametoa kauli kwamba watu wana udhibiti
juu ya maisha yao wenyewe ya hapa duniani, lakini wengi wao wanashindwa
kusema ni kwa nini huwa inakuwa hivyo.
Sababu ni kwanini mtu anaweza akadhibiti hali yake mwenyewe ya maisha ya hapa duniani
na sanasana hali ya mtu ya kifedha
imeelezwa kwa ufasaha katika sura hii. Watu wanaweza wakaongeza udhibiti
wa wao wenyewe na mazingira yao kwa sababu wana uwezo wa kushawishi
akili
zao za ndani, na kupitia hizo huongeza ushirikiano wa Nguvu kuu
isiyokuwa na mipaka(Mungu).
Sasa unasoma sura inayowakilisha msingi wa tao la hii
filosofia . Mafunzo yaliyomo ndani ya sura hii ni lazima yaeleweke na kufanyiwa kazi kwa uvumilivu ikiwa unataka kufanikiwa katika kugeuza
shauku kuwa pesa. Kitendo halisi cha kugeuza shauku kuwa pesa huhusisha matumizi ya kujishauribinafsi. Tunza
wazo hili akilini, na wakati wote utakuwa na ufahamu wa sehemu muhuhimu ya
kanuni ya kujishauribinafsi, ni kufanya jitihada zako kupata pesa kupitia njia
zilizoelezwa katika kitabu hiki. Tekeleza maelekezo haya kama vile wewe ni
mtoto mdogo. Ingiza katika jitihada zako kitu kinachofanana na imani ya mtoto mdogo. Mwandishi amekuwa
makini sana kuona kwamba hamna mafunzo yasiyotekelezeka yaliyowekwa kwasababu
ya shauku yenye nia njema ya kusaidia.
Baada ya kusoma kitabu kizima, rudi katika sura hii na
kufuata kwa moyo na kwa vitendo hili fundisho:
SOMA SURA NZIMA KWA SAUTI MARA MOJA KILA USIKU MPAKA
UNASHAWISHIKA KABISA KWAMBA KANUNI YA KUJISHAURIBINAFSI NI DHABITI, KWAMBA
ITAKUKAMILISHIA YALE YOTE YALIYODAIWA KWAKE. UTAKAPOKUWA UKISOMA, PIGIA MSTARI
KWA PENSELI KILA SENTENSI INAYOKUVUTIA ZAIDI.
Fuata maelekezo haya na yatafungua njia kwa uelewa kamili
na umahiri katika kanuni za mafanikio.
…………………………………………………………………………
Na huo ndio mwisho wa sura hii ya 4, tukutane tena Sura inayofuata
ya 5 ya kitabu hiki cha pesa na mafanikio mashuhuri kupita vitabu vingine vyote
vilivyowahi kuandikwa Duniani na mwandishi yeyote yule.
Ukihitaji pia vitabu vya kiswahili vya biashara na ujasiriamali,
namna ya kuandaa mpango
wa biashara yako, jinsi ya kufanikia katika biashara yeyote ile ya rejareja
na njia ya uhakika ya kujipatia kipato cha ziada
nje ya shughuli zako za msingi, wasiliana na sisi kwa
simu 0712
202244
au bonyeza>>>
hapa kwa maelezo zaidi.
Asante mwalimu
ReplyDelete