HOTUBA
NZURI BAADA YA MLO WA JIONI KWA AJILI YA DOLA BILIONI MOJA
‘Mnamo jioni ya Desemba 12, 1900 baadhi ya
vigogo wa fedha wa Taifa wapatao themanini walikusanyika katika ukumbi wa klabu
ya Chuo Kikuu Barabara ya Tano kumpa heshima kijana mdogo kutoka Magharibi, ni wageni wachache waliogundua kuwa walikuwa wanakwenda
kushuhudia tukio muhimu zaidi Marekani
katika historia ya viwanda.
‘J. Edward Simmons na Charless Stewart Smith,
mioyo yao ikiwa imejawa na shukrani kwa
ukarimu kupita kiasi walioonyeshwa na Charles M. Schwab katika ziara yao hivi
karibuni walipotembelea Pittsburgh, walikuwa wametayarisha chakula cha jioni
kumtambulisha mtu wa chuma cha pua mwenye umri wa miaka 38 kwa Jumuiya ya
mabenki ya Mashariki.
‘Lakini hawakutazamia yeye kuingia kwa
kukurupuka katika ule mkutano. Walimpa angalizo, kwa kweli kwamba hisia za
ndani za watu wenye maringo wa New York zisingeliweza kusikiliza
atakachokisema, na hivyo ikiwa asingependa kuwaudhi Stilimans na Harrimans na
Vanderbbilts, ni bora angejiwekea ukomo mwenyewe kwenye dakika kumi na tano au
ishirini za maongezi mepesimepesi na kuacha mambo yaende kama yalivyo.
‘Hata John Pierpont Morgan aliyekuwa ameketi
mkono wa kulia kwa Schwab kama alivyokuwa mgeni wa heshima kwake,
alitarajia kuzungumza kidogo tu kwa
madaha kuikoga meza ya hafla ile kuwa alikuwepo. Na kwa kadri vyombo vya habari
na umma walivyokuwa wanahusika, tukio zima lilikuwa la muda mchache kiasi kwamba
halikutajwa popote katika magazeti siku iliyofuata.
‘Hivyo waandaaji wawili na wageni wao
waalikwa walikula kivyao kupitia mizunguko ya kawaida saba au nane. Kulikuwa na
mazungumzo machache na hata yale kidogo yaliyokuwepo yalizuiliwa. Ni watu wa
benki na mdalali wachache waliokuwa wamewahi kukutana na Schwab ambaye ajira
yake ilikuwa imechipua katika mabenki ya Monongahela na hakuna aliyemfahamu
vizuri.
‘Lakini kabla jioni haijamalizika, yeye - wao
pamoja na Mkuu wa pesa Morgan waligeuka marafiki ghafla, na mtoto wa Dola billioni
moja, Shirika la chuma cha pua la Marekani(United States Steel Corporation) alikuwa anakwenda kutungwa.
‘Labda ni kwa bahati mbaya kwa ajili ya
historia, kwamba hamna kumbukumbu kamwe ya hotuba ya Charles Schwab kwenye
chakula hicho cha jioni iliyowahi kutunzwa. Alirudia baadhi ya sehemu za hotuba
hiyo katika siku ya baadaye iliyofanana na ya mkutano wa Chicago wa watu wa
benki. Na bado tena baadaye wakati serikali ilipoleta madai ya kuivunja kampuni
ya chuma cha pua(steel trust), alitoa tafsiri yake mwenyewe, kutoka upane wa
ushahid, wa maoni yaliyomchochea Morgan wazimu wa kuingia katika shughuli ya
kiuchumi.
‘Pengine hata kama ile ilikuwa ni hotuba
“nyepesi” kwa namna fulani isiyofuata sarufi(kwa mambo madogomadogo ya lugha
kamwe hayakumsumbua Schwab), ilijaa semi za kuchekesha na mafumbo, lakini mbali
na hayo ilikuwa na nguvu ya kiumeme na athari kwenye bilioni tano za makadirio
ya mtaji uliowasilishwa na wanahafla ya chakula cha jioni.
‘Baada ya kumalizika na mkusanyiko ukiwa bado
kwenye mapumziko, ingawa Schwab alikuwa amezungumza kwa dakika tisini, Morgan
aliongozana naye kwenye dirisha la mapumziko ambapo walininginiza miguu yao
hewani kutoka juu kwenye viti visivyoburudisha. Walizungumza kwa saa moja
zaidi. Maajabu ya haiba ya schwab yalikuwa yamefunguliwa kwa nguvu zote, lakini
kilichokuwa muhimu zaidi na cha kudumu ilikuwa ni programu yenye kueleweka
aliyoieleza kwa ajili ya uendelezaji wa chuma cha pua.
‘Watu wengine wengi walikuwa wamejaribu
kumshawishi Morgan kuunda kampuni ya chuma cha pua kwa kuunganisha pamoja
makampuni ya biskuti, waya na magurudumu, sukari, raba, whiski, mafuta au na
mchanganyiko wa bazoka. Mcheza kamari John W. Gates, alimshawishi lakini Morgan
hakumuamini. Moore boys, Bill na Jim, madalali wa Chicago ambao walikuwa
wameunganisha kampuni ya viberiti(match trust) na kampuni ya uokaji(cracker
corporaton) walimshawishi lakini walishindwa.
‘Elbert H. Garry, wakili anayeheshimika
nchini, alitaka kumshawishi lakini hakuwa na uwezo wa kutosha kumvutia. Mpaka
pale ushawishi wa Schwab ulipomchukua J. P Morgan hadi kwenye kilele ambacho
kutoka hapo aliweza kupiga taswira ya matokeo thabiti ya mradi wa kiuchumi wa
uhakika zaidi kuwahi kuanzishwa, mradi uliochukuliwa kama ndoto ya
kiuendawazimu ya mpumbavu anayetaka pesa za haraka haraka.
‘Mvutano wa pesa uliokuwa umeanza kizazi
kimoja nyuma, kuvutia mamilioni ya makampuni madogo na wakati mwingine
yaliyoendeshwa bila ufanisi katika
muunganiko wa kampuni kubwa zenye ushindani, ulikuwa ukijiendesha katika sekta
ya chuma cha pua kupitia haramia
mchangamfu wa biashara John W. Gates.
‘Gates tayari alikuwa ameanzisha kampuni ya
chuma na waya ya Kimarekani(The Americana Steel and wire Company) kutokana na
msuruu wa kampuni ndogondogo, na pamoja na Morgan walikuwa wameanzisha Kampuni
ya Shirikisho ya chuma cha pua(The Federal Steel Company). The National Tube na
American Bridge ni makampuni mengine mawili zaidi Morgan aliyojihusisha nayo,
na Moore Brothers walikuwa wametelekeza biashara za viberiti na pipi kuunda
“American Group-Tin Plate, Steel Hoop,
Sheet Steel na The National Steel
Company.
‘Lakini kwa upande wa Kampuni kubwa la Andrew
Carnegie, kampuni iliyomilikiwa na kuendeshwa na wabia hamsini na tatu, hiyo
miunganiko mingine ilikuwa midogomidogo. Wangeweza kuungana kwa thati ya mioyo
yao lakini wengi wao hawakuweza kupenya kushindana na kampuni ya Carnegie, na
Morgan hili alilifahamu.
‘Mzee wa Kiskoti, Andrew Carnegie, mtu
asiyetabirika alilifahamu hili pia. Kutoka kilele kitukufu cha “Skibo Castle”(makazi yake ya kifahari)
alikuwa ameona kwanza kwa mshangao na halafu kwa uchungu majaribio ya kampuni
ndogondogo za Morgan kuingilia biashara zake. Majaribio yalipozidi kuongezeka,
tabia ya Carnegie iligeuka kuwa hasira na ulipizaji kisasi. Aliamua kuiga kila
kiwanda kilichomilikiwa na washindani wake.
‘Mpaka sasa hakuwa amevutiwa na waya,
mabomba, magurudumu wala mabati. Badala yake aliridhika kuwauzia kampuni hizo
chuma cha pua ghafi na kuwaacha watengeneze maumbo yeyote wayatakayo.Sasa
alikuwa na Schwab kama msaidizi wake mkuu na luteni mwenye uwezo, alipanga
kuwafilisi maadui zake.
‘Hivyo ilikuwa ni hiyo hotuba ya Charles
Schwab, Morgan alipoona jibu la tatizo lake la muunganiko. Kampuni bila ya Carnegie-mkubwa wa wote -
isingeliweza kuwa kampuni hata kidogo, kama mwandishi mmoja alivyosema, “ ni sawa na mkate wa zabibu usiokuwa na
zabibu”.
‘Hotuba ya Schwab usiku wa tarehe 12 Desemba,
1900, bila shaka ilibeba hitimisho, ingawa haikuwa ahadi, kwamba kampuni kubwa
ya Carnegie ingeliweza kuletwa chini ya hema ya Morgan. Alizungumza juu ya hali
ya baadaye ya dunia kwa chuma cha pua, juu ya kujipanga kwa ufanisi, juu ya
ubobezi katika nyanja mbalimbali, juu ya kuzifunga kampuni na viwanda
vinavyofanya vibaya na kuelekezea nguvu zaidi katika rasilimali zenye tija, juu
ya uchumi katika usafirishaji wa mawe yenye madini, juu ya uchumi katika idara
za nguvukazi na utawala, juu ya masoko ya kigeni.
‘Zaidi ya hapo aliwaeleza maharamia wa
biashara miongoni mwao, kasoro za tabia yao ya uharamia. Aliwaeleza kwamba,
malengo yao, yalikuwa ni kujenga ukiritimba, kupandisha bei na kujilipa wenyewe
faida nono nje ya stahili zao. Aliulaumu kwa nguvu zake zote mfumo huo.
‘Aliwaambia wasikilizaji wake, kutokuona
mbali kwa sera kama hiyo kunasimama kwenye ukweli kwamba kulikuwa kunazuia soko
katika zama ambazo kila kitu kilikuwa kikililia kutanuka. Kwa kurahisisha bei
ya chuma cha pua, alisema, soko linalotanuka daima lingeweza kutengenezwa;
matumizi zaidi ya chuma cha pua yangeliweza kubuniwa na sehemu kubwa ya
biashara ya dunia ingeliweza kushikwa. Ukweli ingawa hakufahamu, Schwab alikuwa
nabii wa uzalishaji wa kisasa wa bidhaa kwa wingi(mass production)
‘Kwa hiyo hafla ya chakula cha jioni katika
klabu ya Chuo Kikuu ilifikia tamati. Morgan alikwenda nyumbani kufikiria juu ya
utabiri wa kutia matumaini wa Schwab. Schwab alirudi Pittsburgh kuendesha
biashara ya chuma cha pua ya Andrew Carnegie, wakati Gary na wengine waliobakia
walirudi kwenye soko la hisa kupoteza muda na mambo madogomadogo kwa matumaini
ya kile ambacho kingelifuata.
‘Haukupita muda mrefu. Ilimchukua Morgan
kiasi cha muda wa wiki moja kutafakari wazo Schwab alilokuwa ameliweka mbele
yake. Baada ya kujihakikishia mwenyewe kuwa hakukuwa na matatizo ya kifedha
ambayo yangeliweza kuja kutokea, alituma ujumbe kumuita Schwab - na kumkuta
kijana akiwa na aibu kiasi. Schwab alidokeza ya kuwa Bwna Carnegie
asingefurahishwa ikiwa angekuta Rais wake wa kampuni anayemuamini amerubuniwa
na kukubali kuonyesha mapenzi kwa mfalme mkuu wa Wall Street, mtaa ambao
Carnegie alishaapa kutokujihusisha nao. Hatimaye mjumbe aliyetumwa W. Gates,
alipendekeza kwamba ikiwa Schwab angelikwenda katika hoteli ya Bellevue
Philadelphia, J.P Morgan naye pia angeliweza kutokea pale wakutane.
‘Hata hivyo Schwab alipowasili, Morgan kwa
bahati mbaya alikuwa mgonjwa nyumbani kwake New York, na hivyo kutokana na
shinikizo la mwaliko wa mzee huyu, Schwab ilimbidi aende New York na
kujiwasilisha mwenyewe katika mlango wa maktaba ya bwana fedha.
‘Siku hizi wanahistoria fulani wa uchumi
hueneza imani kwamba tangu mwanzo mpaka mwisho wa ‘sinema’, jukwaa liliandaliwa
na Andrew Carnegie - kwamba chakula cha jioni, hotuba maarufu, mkutano wa
Jumapili usiku kati ya Schwab na Mfalme wa pesa, yalikuwa ni matukio
yaliyopangwa na Canny Scot(Andrew Carnegie). Ukweli ni ikinyume kabisa. Wakati
Schwab alipoitwa kuja kukamilisha mapatano, hakufahamu hata ikiwa “bosi mdogo”
(kama Andrew Carnegie alivyokuwa akiitwa kwa utani), angeliweza hata kidogo
kusikiliza ofa ya kuuza, hasa kwa kundi la watu ambao Andrwew aliwachukulia
kama watu waovu.
‘Lakini Schwab alikwenda kwenye mkutano akiwa
na karatasi sita zilizoandikwa vizuri kwa mkono wake mwenyewe, aliwakilisha
akilini mwake thamani halisi na uwezo tarajiwa wa faida wa kila kampuni ya
chuma cha pua aliyofikiria kama ni nyota muhimu katika dunia mpya ya chuma.
‘Wanaume wanne walitafakari juu ya tarakimu
hizo usiku kucha . Kiongozi Mkuu, bila shaka alikuwa ni Morgan, akishikilia msimamo katika imani yake kwenye
haki ya utukufu wa pesa. Pamoja naye alikuwa rafiki yake Kabaila, Robert Bacon,
msomi na mtu muungwana. Wa tatu alikuwa John W. Gates ambaye Morgan alimbeza
kama mcheza kamari na alimtumia kama zana. Wanne alikuwa Schwab ambaye
alifahamu zaidi kuhusu mchakato wa kutengeneza na kuuza chuma cha pua kuliko
mtu mwingine yeyote yule aliyekuwepo katika kundi. Kupitia mkutano ule tarakimu
za Pittsburgh kamwe hazikuhojiwa. Kama angesema kampuni ilikuwa na thamani
kiasi fulani, basi ingelikuwa na thamani kiasi hichi hicho na siyo zaidi.
‘Alikuwa na msimamo pia juu ya kujumuishwa
katika muunganiko zile kampuni alizozitaja tu. Alikuwa ameanzisha Shirika
ambalo kusingelikuwa na kuigizwa, wala hata kuwaridhisha marafiki walafi
waliotaka kutua makampuni yao juu ya mabega mapana ya Morgan. Hivyo aliibwaga
nje kiufundi idadi ya makampuni makubwa
ambayo ‘matapeli’ wa Wall Street walikuwa wakiyatupia macho yao yenye
njaa.
‘Kulipopambazuka, Morgan aiamka na kuunyoosha
mgongo wake. Swali moja tu lilibakia…
“Unafikiri unaweza ukamshawishi Andrew
Carnegie kuuza?” Aliuliza.
“Naweza kujaribu” Alisema Schwab.
“Ikiwa utaweza kumfanya auze, nitatimiza
ahadi” Alisema Morgan.
‘Lakini mpaka kufikia hapo. Carnegie angeweza
kuuza? Ni kiasi gani cha pesa angeweza kuhitaji? (Schwab aliwaza juu ya
$320,000,000) Angechukua malipo katika mfumo gani? Katika mfumo wa hisa za
kawaida au hisa za upendeleo? Dhamana? Pesa taslimu? Hakuna mtu ambaye angeweza
kuchukua kiasi cha Dolla bilioni tatu katika pesa taslimu.
‘Kulikuwa na mchezo wa golfu mwezi Januari
katika mbuga ya barafu ya St. Andrews links huko Westchester. Andrew akiwa
amejivika lundo la sweta kujikinga na
baridi, na Charles Schwab akizungumza kwa uhodari kama kawaida ili kujitia
moyo. Lakini hakukuwa na neno lolote kuhusiana na biashara walilozungumza mpaka
pale wawili hao walipoketi chini sehemu nzuri tulivu kwenye kibanda cha
Carnegie kilichokuwa jirani.
‘Kisha kwa ushawishi uleule aliowapumbaza
mamilionea themanini kwenye klabu ya Chuo Kikuu, Schwab alimwaga ahadi zenye
kuvutia za kustaafu kwa faraja, ahadi za mamilioni ya kumtosheleza Mzee mafao
yake uzeeni. Carnegie alisalimu amri, akaandika tarakimu juu ya karatasi na
kumpa Schwab akisema, “Vizuri, hiyo ndiyo bei tutakayouza”
‘Tarakimu zilikuwa zinakadiriwa kufikia Dola $400,000,000 na ilifikiwa kwa kuchukua
$320,000,000 kiasi cha msingi na kuongeza hapo $80,000,000 ili kuwakilisha
mtaji ulioongezeka thamani kwa kipindi cha miaka miwili ya nyuma.
‘Baadaye wakiwa ndani ya meli(Trans Atlantic
Liner) Carnegie alimwambia Morgan kwa masikitiko “Natamani ningekutajia
$100,000,000 zaidi”
“Kama ungetaja, ungeliweza kuipata” Morgan
alimjibu kwa uchangamfu.
‘Schwab mwenye umri wa miaka 39 alipata
dhawabu yake. Alifanywa kuwa Rais wa Shirika jipya na kubakia katika uthibiti
wake mpaka mwaka 1930’
Simulizi hii ya kusisimua ya biashara kubwa
ilijumuishwa humu ndani ya kitabu kwa sababu ni mfano halisi wa njia ambayo
kupitia hiyo Shauku inaweza ikabadilishwa kuwa katika kitu halisi kinacholingana
nayo Ninafikiria baadhi ya wasomaji watahoji kauli hiyo kwmba ni kwa
vipi Shauku
tupu isiyoweza kushikika inaweza kugeuzwa kuwa kitu halisi. Bila shaka wengine
watasema, ‘Huwezi ukaigeuza hali ya kutokuwepo
kitu chochote kuwa kitu chochote!’
Jibu lipo ndani ya simulizi hii ya Shirika la Chuma cha Pua la Marekani(United
States Steel)
Shirika hilo kubwa liliundwa katika akili ya
mtu mmoja. Na mpango ambao Shirika liliutumia kwa viwanda vya chuma cha pua
uliolipa shirika uthabiti kipesa ulibuniwa katika akili ya mtu huyohuyo mmoja. Imani yake. Shauku yake, Ubunifu
wake, Uvumilivu wake vilikuwa ni viungo vya kweli vilivyounda Shirika
la Chuma Cha Pua la Marekani, viwanda vya chuma cha pua na mashine
zilizochukuliwa na Shirika baada ya
kusajiliwa kisheria ilikuwa ni jambo dogo, lakini tathmini ya kina
itabainisha ukweli kwamba thamani iliyokadiriwa ya mali zilizochukuliwa na
Shirika iliongezeka kwa kadirio la dola milioni
mia sita kwa hesabu tu ile iliyowaunganisha chini ya usimamizi mmoja.
Kwa maneno mengine, wazo la Charles M. Schwab ukijumlisha
na Imani ambayo aliipandikiza
kwenye akili ya J.P. Morgan na wengineo, liliuzwa kwa faida ya karibu
$600,000,000. Siyo kiasi kidogo cha pesa kwa wazo moja!
Ni nini kilichotokea kwa baadhi ya watu
waliochukua hisa zao za mamilioni ya dola ya faida iliyotokana na uuzwaji huu
ni suala ambalo hatuhusiki nalo kwa sasa. Jambo muhimu katika mafanikio haya ya
kushangaza ni kwamba yanatoa ushahidi usiopingika wa ukamilifu wa filosofia
iliyoelezwa katika kitabu hiki.
Zaidi ya hapo, utendaji kazi wa filosofia
umedhihirishwa kutokana na ukweli kwamba Shirika la Chuma Cha Pua la Marekani
lilipata mafanikio. Lilikuwa moja kati ya Mashirika tajiri zaidi na lenye nguvu
Marekani, likiajiri maelfu ya watu, kubuni matumizi mapya ya chuma cha pua na
kufungua masoko mapya, hivyo kuonyesha kwamba, $600,000,000 za faida ambazo
wazo la Schwab lilizalisha, zilikuwa halali.
Utajiri huanzia
katika hali ya fikra. Ukomo wa utajiri hupangwa tu na mtu ambaye ndani ya akili
yake fikra hutiwa katika vitendo. Imani huondoa ukomo. Kumbuka hili wakati unapokuwa
tayari kujadiliana na Maisha kwa chochote kile kiwacho unachokihitaji kama bei kwa kuwa umepitia njia hii. Kumbuka
pia kwamba, mtu aliyeunda Shirika la chuma cha pua la Marekani kiuhalisia
hakuwa anajulikana kabisa wakati huo. Alikuwa tu “Msaidizi” wa Andrew Carnegie, mpaka pale alipozaa wazo lake maarufu. Baada ya hapo, alipanda haraka kwenye nafasi
ya Madaraka, Umaarufu na Utajiri.
.......................................................................................................
Inafuata >>>>Sura ya NNE>>>>>> Usikose.
Pia kwa vitabu mbalimbali, vya Biashara, Ujasiriamali, Michanganuo na Mafanikio kwa ujumla tembelea ukurasa huu hapa >> SMART BOOKS TANZANIA.
0 Response to "UTAJIRI HUANZA NA WAZO, UKOMO WA UTAJIRI MTU HUPANGA MWENYEWE AKILINI"
Post a Comment