SURA YA NANE.
Hatua ya 7 Kuelekea utajiri wa kweli.
Fanya maamuzi mara mora, lakini ubadilishe maamuzi hayo taratibu, watu wengi
wanaoshindwa kumiliki fedha za kutosha (utajiri) kwa ajili ya mahitaji yao, ni wale ambao wanaaathiriwa
kwa kiasi kikubwa na maoni ya watu wengine. Huruhusu, magazeti na vyombo vingine
vya habari kufikiri badala yao. Ikiwa
wewe ni mtu wa aina hii basi hautaweza kuwa na shauku ya kutimiza mambo
yako na badala yake utageuka mtumwa wa mawazo ya watu wengine.
Ni tabia ya watu wanafiki, na wasio na upeo wa kutosha kujifanya kuwa
wanaelewa sana. Watu hawa hupenda kuongea sana na hawapendi
kusikiliza toka kwa mwingine.
Ushauri : Ikiwa utapenda kuwa na tabia ya
kufanya maamuzi ya haraka basi fungua
macho na masikio yako zaidi kuliko vile unavyoufungua mdomo wako. Ikiwa
utongea zaidi kuliko kusikiliza unajinyima fursa nyingi za kujilimbikizia maarifa. Na kumbuka pia kwamba kila mtu
unayekutana naye pia anatafuta fursa ya kupata pesa kama wewe, utakapokuwa unazungumza
kupitiliza, unaweza ukajikuta unampa na siri za mipango yako, na ukaja kushanga
baadaye amekupiku kwa kuiweka katika vitendo kabla yako.Wanaofanya maamuzi
mara moja na yenye uhakika, wanafahamu wanachokihitaji na mara nyingi hukipata.
0 Response to "KUCHAMBUA THINK & GROW RICH SURA YA 8, (MAAMUZI KIBOKO CHA KUSITASITA)"
Post a Comment