MAAJABU YA KUFIKIRI MAMBO MAKUBWA NA KWANINI UWEKE MALENGO MAKUBWA MAISHANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAAJABU YA KUFIKIRI MAMBO MAKUBWA NA KWANINI UWEKE MALENGO MAKUBWA MAISHANI

Kumradhi msomaji wangu, nitatoka nje ya mada hii kidogo na kisha tutarudi tena hivi punde kuendelea kama kawaida.

Katika kitabu nilichoandika mwaka 2012, “Mifereji 7 ya pesa na siri Matajiri wasiyopenda kuitoa“, sikutegemea kabisa kama kitabu kile kidogo kingelifanya maajabu kiliyoyafanya. Kwanza nilishangazwa mno na jinsi mimi mwenyewe wakati nilipokuwa nakiandika kilivyonihamasisha na kunipa mzuka, na mada iliyonisisimua zaidi haikuwa nyingine bali ni hii, “jinsi ya kujiwekea malengo katika maisha”

Sina lengo la kujisifu au kujifagilia kama watoto wa mjini wasemavyo,  ila huwa napenda kusisitiza na kurudia mara kwa mara kwamba kitabu kile kilikuwa ndiyo kitabu cha kwanza hapa Tanzania katika tasnia ya elimu ya mafanikio kutoa hamasa kubwa zaidi katika suala zima la maendeleo binafsi ya mtu(The most Inspirational Book ever written in Tanzania on Self Development).

Ikiwa kuna mtu anayebisha ukweli huu, naomba aniletee ushahidi wa vitabu/kitabu kingine kilichoandikwa nyuma ya mwaka huo wa 2012 katika tasnia hii ya maendeleo binafsi ya mtu kwa hapa nchini kilichoelezea kwa ufasaha mkubwa namna mtu anavyoweza kujiendeleza binafsi. Sisemi kwamba kabla ya hapo hakukuwa na watu waliokuwa wakitoa elimu ya maendeleo binafsi hapa nchini, la hasha, walikuwepo ndiyo maana hata katika kitabu kingine nilichotunga cha “Kanuni ya kujifunza Elimu ya pesa na mafanikio kwa ufanisi” hili nimelieleza bayana kabisa.

Ninachomaanisha hapa ni kwamba, Kitabu kilichotungwa hapa Tanzania kinachogusa maeneo yote muhimu yahusuyo maendeleo ya mtu binafsi kuanzia, jinsi ya kujipatia kipato nje ya shughuli yako ya msingi, katika maana nyingine unaweza ukasema, kufungua biashara ukiwa bado umeajiriwa, kufungua biashara au mradi mwingine wa kiuchumi nje ya ule mradi uliouzoea kila siku na hata kufanya mradi wa kiuchumi ungali bado chuoni au masomoni.

Dhana hii niliielezea kama “MIFEREJI 7 YA PESA” na ndiyo hata iliyobeba jina la kitabu chenyewe. Eneo jingine lilikuwa ni jinsi ya kujiwekea vitu vya msingi kabisa mtu unapotaka kuanzisha kitu chochote kile, kwa mfano, biashara yeyote, mradi wa kiuchumi, taasisi, na hata kwa mtu binafsi pale unapotaka kuingia katika ajira. Vitu hivyo 3 niliviainisha kuwa ni DHAMIRA KUU, MALENGO na DIRA au kwa kimombo unaweza ukaviita, MISSION, OBJECTIVES and VISION.

Dhana au maneno hayo 3 maarufu katika ulimwengu wa biashara, kazi na pesa, hutumiwa karibu kila mahali, kuanzia na mtu mmoja mmoja mpaka taasisi mbalimbali ikiwemo na serikali yenyewe. Watu huwa tunavitumia hata ikiwa hatuelewi ni kitu gani kwa kuwa ndiyo mwanzo wa kila jambo linalofanywa na kiumbe chenye akili na hususani mwanadamu, wanyama hawana uwezo huo.

SOMA: Kuanzisha biashara ukiwa kazini(umeajiriwa) au masomoni(chuo) fuata hatua hizi 7

Maeneo mengine kwa ufupi tu yalikuwa ni, Siri matajiri wasiyopenda kamwe kuitoa, jinsi unavyoweza kuutumia muda wako vizuri siku ikawa na masaa 25 badala ya 24, na mwaka huu nimekiboresha zaidi kwa kuongeza zingine nzuri mojawapo ikiwa ni, “hesabu muhimu zaidi kweynye biashara yeyote ile ambayo mjasiriamali hata kama hajui kusoma wala kuandika, ni lazima ajue kuitumia. Hesabu yenyewe siyo ngumu na kwa kweli hutumiwa na kila anayefanikiwa kipesa. Ni rahisi mtu kuipuuzia na kuona haina umuhimu wowote pasipo kujua, na hii ndiyo sababu ya watu wengi kuishi maisha ya umasikini. Ukifikiria hesabu hiyo ni ile maarufu ya “MAPATO – GHARAMA = FAIDA” Utakuwa umekosea vibaya!

Nimalizie kwa kusema kwamba, hamasa kitabu hiki iliyochochea kwa jamii ya Kitanzania ni jambo ninalomshukuru Mungu kila siku kwani ndiyo moja ya malengo yangu kimaisha pamoja na mimi mwenyewe kufanikiwa lakini kuhakikisha na watu wengine wengi kadiri inavyowezekana nao wanafanikiwa hasa katika kubadili fikra na mitazamo ya jadi tuliyoizoea.

Lakini pamoja na mafanikio hayo kidogo, Tanzania bado tuko nyuma sana kwani inashangaza mno kusikia kumbe kuna watu wasiokuwa na taarifa sahihi kiasi kwamba bado wanazo akilini zile fikra za miaka 47 kiasi cha kuangamiza roho za watu kisa eti wamewahisi ni ‘mumiani’ au chinjachinja wanaonyonya damu za watu. Na lakushangaza zaidi hata mchungaji anayetegemewa kua kioo kwa waumini wa kawaida ndiyo kwanza anakuwa mhamasishaji mkuu wa mauaji hayo. Watu kama hawa wanahitaji kubadilishwa fikra!

Ni baada ya kutoka kwa kitabu hiki mwaka 2012 kikiambatana na kampeni kubwa niliyoipa jina la, “KUELEKEAUTAJIRI” ndipo vijana wengi walipopata mwamko mkubwa katika kujitafutia maendeleo binafsi  kupitia njia mbalimbali nilizopendekeza mle kwenye kitabu.


Ndugu msomaji wangu, nililazimika kutoka nje kidogo ya mada ya leo ili kwa pamoja tuweze kukumbuka ni wapi tunakotoka na tunakoelekea ni wapi. Kama unadhani mimi ni muongo au niliyoyasema hapa ni porojo basi nakuomba kitu kimoja, shilingi elfu tatu najua ni nyingi hasa usawa huu wa awamu ya Tano, lakini najua pia utakuwa haujapoteza bali umewekeza; Hebu kinunue kitabu hicho sasa hivi na kukisoma hapahapa kwenye simu yako au kompyuta unayotumia sasa hivi kwa bei ya sh. 3,000/=. Pindi tu ukituma pesa kwenye namba 0712 202244 na wewe utapokea kitabu kwenye e-mail yako au Telegramu kama unayo ndani ya muda usiopungua dk.10. Kama unatumia mitandao mingine nijulishe.

Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na ni kwanini uweke malengo makubwa maishani.
Hebu kwanza jiulize mwenyewe, huwa malengo unayojiwekea yakoje? Ni malengo madogomadogo ambayo unapoyatekeleza yanakupa burudani au ni malengo makubwamakubwa yanayokupa tabu wakati wa kuyatekeleza? Na je, wakati ukijiwekea malengo hayo huwa unafikiriaje?, Unafikiri mambo makubwa au madogo?

Baada ya hapo sasa na hebu tuanze kuziangalia njia hizo za kivitendo zinazoelezea uwezo huu wa ajabu wa kufikiri mambo makubwa  hata ikiwa ni ndoto tu ambazo bado hazijawa vitu halisi.

Ipo tabia moja, matajiri karibu wote duniani wanayo, akiwemo, Bill Gates, Warren Buffet, Said Salim Bakhresa, Mohamed Dewj,  Mzee Reginald Mengi na wengineo wengi. Tabia hiyo siyo nyingine bali ni tabia ya “KUFIKIRI MAMBO MAKUBWA” Alhaji Aliko Dangote kwa kutumia mbinu hiyo ameweza kuanzisha viwanda vikubwa zaidi barani Afrika vya kuzalisha sementi na kufanikiwa kuwa tajiri namba 1 barani humo, Jeff Bezoz aliweza kuanzisha duka kubwa zaidi duniani la vitabu mtandaoni- Amazon,

Donald Trump anayegombea kiti cha uraisi wa Marekani sasa hivi kupitia Republican ameweza kuwa mjenzi wa majumba(Real estate Agent) mkubwa kabisa na anayeheshimika siyo Marekani tu bali na Duniani nzima kwa ujumla. Katika hotuba zake siku za nyuma, Trump mwenyewe aliwahi kusema hivi na hapa namnukuu; “Watu wengi hufikiria mambo madogo kwasababu wanayaogopa mafanikio, huogopa kufanya maamuzi na huogopa kushinda. Na hivyo kuwapa watu kama mimi faida kubwa”-Donald Trump.

Unapoyatazama maneno haya ya Trump utagundua kwamba hata anachokifanya sasa kwenye kinyanganyiro cha urais kule Marekani  ni sawasawa ni hicho alichowahi kukitamka miaka zaidi ya mitano iliyopita. Trump hujiwekea malengo makubwa, Trump hufikiri mambo makubwa, Trump haogopi mtu hasa anapojua anafanya jambo ambalo havunji sheria ya nchi, Trump hana aibu linapokuja suala la maslahi yake iwe ni kisiasa au kiuchumi na Trump haogopi kabisa kufanya maamuzi hata ikiwa ni katikati ya hatari inayoweza kumgharimu kile anachokipigania.

Trump hapa anaendelea tena kusema hivi; “Napenda kufikiria mambo makubwa, ikiwa utaenda kufikiria kitu chochote, unaweza pia ukafikiria mambo makubwa”-Donald Trump

Sasa na sisi ndugu yangu tunasubiri kitu gani? Kwanini tusifikirie mambo makubwa na kujiwekea malengo makubwa maisha yetu yakabadilika? Hata kama hatutaweza kuwa kama Trump, lakini angalao tuweze kubadilisha tu mboga na watoto wetu wasome bila shida.

Baada ya utangulizi huo, hebu sasa tukayaone yale maajabu yenyewe 7 ya kufikiria mambo makubwa na sababu zinazokufanya ulazimike kujiwekea malemgo makubwa katika maisha yako ukiwa hapa Duniani.

1. Kufikiria mambo makubwa kunaisukuma akili yako, kuhoji misemo, kauli na desturi mbalimbali za jadi zilizozoeleka miongoni mwa jamii nyingi za kiafrika. Jamii nyingi pasipo hata kujua zimejijengea tamaduni mbalimbali na mitizamo ambapo jambo au kitu chochote kile kilichokuwa nje au kinyume na tamaduni hizo basi huchukuliwa kama ni jambo lisilowezekana au kitendo kiovu. Kauli hizo ni kama hizi zifuatazo;
1)  Soma sana ili baadae upate kazi nzuri yenye mshahara mnono.
2)  Ridhika na kile upatacho.
3)  Aliye juu mngoje chini.
4)  Ili utajirike ni lazima kwanza uwe fisadi au uende kwa wataalamu wa jadi wakupe dawa za kuvuta utajiri nk.
Unapofikiri mambo makubwa, ni kwamba unailazimisha kabisa akili yako kupinga kauli kama hizo mbovu na ubongo wako kuanza mara moja kutafuta njia ya kujinasua  na hali hiyo. Bill Gates angefuata kauli ya “Soma sana ili baadaye upate kazi nzuri” sidhani kama leo hii ungemsikia mtu akisema “Nipigie kompyuta yangu Window 7” au karibu katika kila ofisi duniani kukuta programu za “Microsoft office” kwenye komputa zao.

Nakuomba unielewe vyema hapa, siyo kwamba natetea kila mwanafunzi au mwanachuo aache masomo yake akaanzishe ujasiriamali, HAPANA. Ila ninachotaka kukisisitiza hapa ni kuacha kuzifanya hizo kauli na misemo ya jadi kuwa kama sheria. Kwa mfano kwamba hakuna njia nyingine kabisa ya kufanikiwa maishani zaidi ya kusoma, inamaana hata wale wanaofeli basi huo ndio uwe mwisho wao wa maisha? Fikiria kwanza nje ya kauli hizo kabla haujazipa nafasi ya kwanza.

Wagunduzi wa ndege, Wright Brothers wangeliridhika tu hivihivi na kauli kwamba “Binadamu hawezi kabisa kuruka angani kwa vile hana mabawa ya kurukia kama ndege, hebu nieleze leo hii ungelizisikia ‘Bombadier Q400’ za rais magufuli?

2. Hukupa changamoto ya kwenda hatua mbele zaidi kwa kukubali ukweli hata  ikiwa ukweli wenyewe ni mchungu kiasi gani.
Unapojiwekea lengo kubwa maishani kiasi ambacho unahisi pengine lengo hilo ni gumu na halitawezekana, huwa unajisikia vibaya, lakini hapo unashauriwa ujisukume hivyohivyo tu kulitekeleza kwa kutumia mbinu hii ya kufikiri mambo makubwa, mwishowe utashangaa unafanikisha lengo lako kama ulivyolipanga.

3. Kufikiria mambo makubwa huunganisha pamoja hisia na shauku yako. Unavyojisikia wakati unapoweka lengo kubwa maishani mwako kunategemea sana jinsi utakavyovichanganya vitu hivyo viwili, hisia na shauku. Ikiwa utajisikia vibaya kuwa unalenga lengo kubwa basi inakubidi ujichunguze upya akilini mwako, lakini ikiwa utajisikia mchangamfu na uliyehamasika basi upo katika mstari mzuri. Lengo kubwa inamaanisha kuichangamsha shauku yako bila ya kujali lengo hilo lina changamoto kiasi gani.

4. Huiweka huru silka yako ya ubunifu.
Kufikiria mambo makubwa hiweka huru silka yako ya ubunifu na kukufanya ufunue mawazo yatakayokuwezesha kufikia malengo yako. Unapoweka lengo kubwa mwanzoni hupatwa na woga lakini baada ya akili kuanza kulizoea lengo lenyewe utaanza kuona uwezekano wa kulitekeleza lengo hilo kwa akili kuleta  njia zitakazosaidia kulifanya lengo hilo kuwa kweli.

5. Hukupa changamoto ya kuongeza kipato chako, kuliko kuishi chini ya kipato unachopata.
Bila shaka umewahi kusikia kauli hii, “Ishi chini ya kipato chako”. Kauli hiyo ni mtazamo zaidi wa mtu mmoja mmoja  kulingana na unavyoichukulia. Wanaofikiria mambo makubwa kamwe hawawzi kuishi chini ya vipato vyao. Wanachokifanya ni kutanua vipato vyao vilingane na mtindo wao wa maisha wanaoutamani. Hawaridhiki na matokeo ya wastani bali hulenga makubwa zaidi. Je, na wewe ndugu yangu ungependa uishi juu ya kipato ama chini ya kipato chako? Uamuzi ni wakwako.

SOMA: Je Dhamira, Malengo na Dira yako ya maisha ni nini?

6. Hukupa sababu ya kuliishi na kulifia lengo lako.
Kufikiria mambo makubwa na kujiwekea malengo makubwa hukupa kitu cha kushughulika nacho maisha yako yote. Christopher Columbus alipojiwekea lengo la kuizunguka dunia, pamoja na hatari yote iliyotokana na imani kwamba dunia ilikuwa na umbile tambarare lakini alilifanya kuwa lengo lake la maisha la kufa na kupona. Kila mtu hapa duniani analo lengo lake, lakini unaweza ukaligundua lengo lako tu endapo utafikiri mambo makubwa.

7. Huondoa yasiyowezekana.
Ajabu la mwisho la kufikiria mambo makubwa, ni uwezo wa kuvunja yale yote “yasiyowezekana” Hugeuza mambo yasiyowezekana kuwezekana. Kauli hii huwa kweli tu pale ambapo mtu unaanza kufikiria mambo makubwa na kuyatekeleza huku ukiwa na mtizamo wa kukubaliana na changamoto kubwa.


Sehemu ya makala hii pia inapatikana katika mtandao wa Jamii forum 
................................................................................................

Ndugu msomaji, Kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali, chenye kila kitu mjasiriamali anachohitaji ili kufika hatua ya juu kabisa kimaendeleo pamoja na uhuru kipesa, sasa ile kazi ya kukirekebisha ili kiwe katika mfumo wa kisasa wa simu za mkononi(mobile friendly) imekamilika. 

Wateja sasa watakuwa na uwezo wa kukinunua kama softcopy yaani kitabu pepe moja kwa moja kupitia E-mail zao na Telegram kwa bei ya TSh. 10,000/= badala ya TSh. 20,000/= katika mfumo wa kitabu cha kawaida cha karatasi. Ili kukipata tuma fedha na anuani yako ya e-mail kwenye namba hii. 0712 202244 jina litokee, Peter Tarimo

Vitabu vya kawaida vya karatasi navyo vipo, ukiwa Dar tunakuletea mpaka ulipo na Mikoani(mkoa wowote ule) tunakutumia kwa njia ya Mabasi. Tuwasiliane ikiwa utahitaji kitabu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu vitabu vyote kutoka SELF HELP BOOKS, tembelea ukurasa huu hapa, SMART BOOKSTZ

0 Response to "MAAJABU YA KUFIKIRI MAMBO MAKUBWA NA KWANINI UWEKE MALENGO MAKUBWA MAISHANI"

Post a Comment