MLANGO FAHAMU WA SITA : MAPITIO YA KITABU THINK & GROW RICH SURA YA 14 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MLANGO FAHAMU WA SITA : MAPITIO YA KITABU THINK & GROW RICH SURA YA 14

SURA YA 14.
MLANGO FAHAMU WA SITA.
(Mlango wa kuingilia hekalu la hekima)
Hatua  ya 13 kuelekea mafanio & utajiri.

Kanuni hii ya 13 na ya mwisho inaitwa "mlango fahamu wa sita" ambao ndio unaotumika kuwasiliana na nguvu isiyokuwa ya kawaida(Infinite Intelligence). Nguvu isiyokuwa ya kawaida tunayoiita "Mungu" au Muumba wa vitu  vyote. Uwe ni muumini wa dini yeyote au usiwe  ni lazima uamini kuwepo kwa nguvu isiyokuwa ya kawaida. Ukijidanganya haipo basi unakataa pia na uwepo wa vitu kama kifo na mambo yote yaliyoko nje ya uwezo wa mwanadamu.

Nguvu hii isiyokuwa ya kawaida hufanya mawasiliano na mhusika kupitia mlango fahamu wa sita kwa hiyari kabisa pasipo juhudi zozote kutoka kwake. Kitendo hicho ndiyo hitimisho la philosofia hii na kinaweza kikaeleweka na kutumiwa endapo  tu mtu atakuwa ameshaweza kuzitumia  kanuni nyingine zote  zilizoelezwa humu kwenye kitabu cha ‘Think and Grow Rich’. 

Nguvu hii isiyokuwa ya kawaida ambayo ndiyo chanzo cha kila kitu humu ulimwenguni kwa kutumia kanuni  hii ya 13, mtu anaweza akaitumia kubadilisha shauku kuwa kitu kinachoshikika kama vile mali au fedha.



>>>Ingia sura ya 15>>>                 

<<<Rudi sura ya  13<<<                         

0 Response to "MLANGO FAHAMU WA SITA : MAPITIO YA KITABU THINK & GROW RICH SURA YA 14"

Post a Comment