SURA YA 2.
(MWANZO WA MAFANIKIO YOTE.)
Hatua ya kwanza kuelekea utajiri.
Kuwa na shauku (hamu kubwa ya kupata mafanikio)
Edwin C. Barnes alipopanda treni kwenda kumfuata mvumbuzi mashuhuri Bwana Thomas Edison, ungeweza kumfananisha na
omba omba au mzururaji asiye na kazi ya kufanya, lakini ndani ya akili yake alibeba wazo lenye thamani
ya mamilioni ya dola. Yeye mwenyewe kabla hajafika kwa Edison akilini alijijengea picha kama kwamba
tayari ameshakuwa mbia, ingawa bado hata hakuwa ameonana naye. Alipofika aliomba kibarua kama mtumishi wa
ndani.Miaka mitano baadaye ndoto yake
ikaja kugeuka kuwa kweli.
Ili kugeuza hamu au shauku yako kubwa kuwa kitu halisi yapo mambo sita
unayopaswa kuyafanya;
1) Tengeneza picha akilini mwako ya kiasi hasa cha kile
kitu unachotaka, kama ni fedha jiwekee kiasi kamili kwa mfano "nataka niwe na
Shilingi milioni 50."
2) Fahamu kwa uhakika ni ni kipi utakachotoa ili
kufanikiwa.
3) Panga au weka tarehe/muda maalumu utakapofanikisha
jambo hilo.
4) Tengeneza mpango mahsusi wa kuigeuza hiyo ndoto yako
na uanze mara moja pasipo kujali kama upo tayari au bado.
5) Andika katika karatasi kile kitu ulichopanga kukipata
mathalani kiasi cha fedha, muda utakaochukua pamoja na kile utakachokitoa kama
malipo.
6) Soma kile ulichoandika kwa sauti kila siku mara mbili,
asubuhi mara unapoamka na usiku kabla haujaenda kulala.Wakati unapokuwa ukisoma
jione na kujihisi mwenyewe kama vile tayari unakimiliki kile ulichokiwekea
malengo.Hakuna mtu yeyote awezaye kumiliki kitu pasipo kwanza kuamini kuwa anao
uwezo wa kukimiliki.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLB9ILbAulqS36ED5TjtTvphIPrrNXH_0afUTN_6vrGHvzhhrYJg3nxepAyJhUx1e46OyPu29gpTuu_6usqfuVFnbcuqqza_5ScM3GWyNKKKW38XHMZNRB7mbfOk_PrLQBDUmo9zerYIXx/s200/soma.jpg)
0 Response to "MUHTASARI WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA PILI 2 (UCHAMBUZI YAKINIFU)"
Post a Comment