SURA YA 12.
(MAWAZO/AKILI YA NDANI)
(Kiunganishi)
Hatua ya 11 kuelekea utajiri.
Mawazo au akili ya ndani ni eneo
katika ubongo ambalo mawazo au fikra hufikia
baada ya kupita moja kati ya ile
milango mitano ya fahamu ambayo ni, macho,
masikio, pua, ulimi na ngozi, hapa ndipo
mawazo hayo hupangwa katika makundi na kurekodiwa na baadaye kuweza
kutolewa mithili ya mtu uanavyopiga
muziki uliorekodiwa katika tape au Cd.
Hupokea taarifa bila ya kujali
kwamba taarifa hizo ni nzuri au ni mbaya.Unaweza kwa hiyari ukaingiza mpango
wowote ndani ya mawazo yako ya ndani ambao
una nia ya kuugeuza kuwa katika kitu halisi kama fedha au mali. Akili ya ndani
inafanya kazi usiku na mchana kwa namna ambayo mpaka sasa hakuna mtu
aliyeigundua. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba akili ya ndani ni kiunganishi
baina ya mtu na muumba (uwezo usio na kikomo).
>>>Endelea sura ya 13 >>><<<Rudi sura ya 11 <<<<<<
0 Response to "SUMMARY:KITABU THINK AND GROW RICH KWA UFUPI SURA YA 12(AKILI YA NDANI) "
Post a Comment