UTANGULIZI.
v Mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu
kinachoshikika kama vile mali au pesa kwa kutumia kanuni maalum.
v Chanzo kikubwa
cha kuanguka ni tabia ya kukata tamaa
baada ya kukutana na vikwazo vya muda mfupi.
v Badala ya kukata tama unapoanguka, tumia uzoefu ulioupata
kufanya vizuri zaidi.
v Utajiri unapoanza kukujia kwa wingi kiasi ambacho unaweza ukashangaa ni
kwa nini haukuja siku zote ulizosubiri, na utajiri huo huanza na wazo kichwani
pamoja na lengo mahususi pasipo hata
chembe ya kazi ngumu.
v Mafanikio humjia mtu anayewaza mafanikio, ubongo
huambukizwa mawazo tunayofikiri midhili ya sumaku, na sumaku hiyo huvuta nguvu,
watu na mazingira yeyote yale yanayohusiana na mafanikio.
v Kwa hiyo kabla hatujaanza kutengeneza utajiri ni
sharti kwanza tuziambukize akili zetu hamu kubwa ya
kutaka kutajirika baada ya hapo, kuwa na lengo na kisha kukomalia lengo
hilo bila kukata tamaa mpaka pale tutakapofanikiwa. Waambukize na watu wengine
uliokuwa nao karibu (washirika) ili wakusaidie kukamilisha lengo lako.
0 Response to "THINK AND GROW RICH, MAPITIO YA KITABU SURA YA KWANZA (1)"
Post a Comment