SURA YA SABA.
MIPANGO MATHUBUTI.
(Kubadilisha shauku kuwa vitendo.)
Hatua ya sita 6 kuelekea katika
utajiri.
Umeshajifunza kwamba kila kitu mwanadamu anachoumba au kumiliki, huanzia na shauku, na shauku hiyo huanzia safari yake pasipokuwa na kitu chochote, sifuri
mpaka kufikia kitu kinachoweza kushikika kupitia karakana ya ubunifu (imaginasion) ambapo mipango kwa ajili ya
mchakato mzima hutengenezwa na kupangwa.
Huko nyuma sura ya pili, tuliona
hatua kamili sita katika mchakato wa
kubadilisha shauku kuwa pesa, moja ya hatua hizo ilikuwa ni kutengeneza
mpango kamili unaotekelezeka. Sasa
katika sura hii utaelekezwa namna
unayoweza kutengeneza mpango huo;
(a)
Tafuta washirika wengi kadiri unavyohitaji
watakaoshirikiana na wewe katika kutekeleza mipango yako ya kuchuma pesa.
(b)
Kabla
hujawatafuta amua ni faida gani watakayopata kama malipo kwa ushirikiano wao
kwani hakuna mtu anayeweza kufanya kazi ya bure.
(c)
Panga
kukutana na watu wako mara kwa mara angalao mara 2 kwa wiki
(d)
Hakikisha
kunakuwa na utulivu na masikilizano kati yako na washirika.
Hakikisha unakuwa na mipango madhubuti na pia ni lazima ukubali
uzoefu, elimu, uwezo, na ubunifu binafsi
wa washirika wako. Mbinu hii imefuatwa na kila mtu ambaye amewahi kupata
utajiri au mafanikio. Unapoanguka katika mipango yako kubali, kwani ni ishara
kwamba mipango yako haikuwa sahihi, itengeneze tena upya na uanze tena safari
ya kutimiza lengo lako ulilojiwekea.
0 Response to "THINK AND GROW RICH UFUPISHO WA SURA YA 7, MIPANGO IMARA"
Post a Comment