Amini usiamini kitabu hiki “Think and Grow Rich” ni moja kati ya vitabu ambavyo vimewafanya watu wengi sana duniani hususani Wamarekani kutajirika, siyo kutajirika kifedha tu bali na hata katika nyanja nyinginezo za kimaisha, kwa mfano inasemekana mtu kama raisi wa marekana ni lazima asome kitabu hiki na kukielewa ndipo anaweza kushinda kinyanganyiro hicho. Ni miongoni mwa vitabu vilivyouza nakala nyingi sana duniani kote, zaidi ya nakala milioni 15. Pamoja na kwamba kimeandikwa miaka mingi iliyopita kabla hata ya kuja kwa kompyuta za kisasa lakini maudhui yake hayajachuja na pengine hayatachuja mamia ya miaka ijayo.
Maelezo mafupi.
Think and Grow Rich kama jina
linavyojieleza ni kitabu kinachohusisha fikra (mawazo) na kupata
utajiri. Maudhui yake hasa ni jinsi binadamu
anavyoweza kubadilisha fikra au maono yake kuwa kitu halisi
kinachoweza kushikika kama mali au fedha.
Mtunzi wake Napoleon Hill
hakubaliani kabisa na dhana kuwa mafanikio
/utajiri ni bahati, urithi, au kutumia nguvu fulani za giza kama wengi
miongoni mwetu tunavyofikiria leo, bali
ni matokeo ya mipangilio madhubuti ambayo imewekwa na binadamu mwenyewe kwa kutumia akili yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Wazo la kukitunga kitabu hiki halikuwa la Napoleon Hill mwenyewe, bali
lilitoka kwa mtu mwingine tajiri aliyejulikana kama Andrew Garnegie. Napoleon hapo kabla alikuwa mwandishi wa habari na katika pitapita yake mitaani ndipo alipokutana na huyu bwana, Andrew
Carnegie ambaye alimwalika Napoleon katika makazi yake ya kifahari. Andrew Carnegie
alikuwa na wazo kichwani mwake siku nyingi kwamba, Mafanikio ni lazima yana kanuni
zake na kanuni hizo zingeweza kuandikwa na hata zikasomwa na kila mtu
anayependa kufanikiwa/kutajirika.
Carnegie alihitaji mtu ambaye
angeweza kufanya utafiti wa kina kuthibitisha kanuni hizo ikiwa kama kweli zipo
na zingeweza kuandikwa, ndipo akamwita Napoleon Hill na kumuuliza kama angeweza
kuifanya kazi hiyo. Alimuuliza Napoleon endapo alikuwa tayari kupoteza miaka 20
akitafiti swala hilo naye bila ya kipingamizi alikubali “ndiyo” na kazi
ikaanza.
Kazi yenyewe ilikuwa ni kuhakikisha anawafanyia usaili matajiri na watu mashuhuri wakubwa nchini Marekani miaka hiyo ya 1930 zaidi ya
mia tano ili kufahamu siri za
mafanikio yao. Andew Carnegie kwa kuwa
alikuwa naye ni mtu tajiri na mashuhuri
alimuandikia Napoleon Hill barua za utambulisho kwa watu mashuhuri wenzake wakati
huo kama Kina Henry Ford, Thomas Edison, F.w. Woolworth na wengineo. Napoleo
Hill aliifanya kazi ile kwa miaka ipatayo 20 na kufanikiwa kupata kanuni
maalumu ambazo matajiri wote na watu wenye mafanikio huzifuata pasipo hata ya
wengi wao kujua.Mwaka 1928 aliweza kukamilisha kazi hiyo iliyochukua vitabu
vikubwa vinane.
Kitabu cha Think and Grow Rich ni
ufupisho wa vitabu hivyo 8 vilivyotokana na utafiti huo.Napoleon Hill mwenyewe
katika kitabu hiki hazitaji siri hizo moja kwa moja bali amesisitiza mtu
kukisoma kitabu kizima na ndipo ndani yake atakapokutana na siri hizo moja
baada ya nyingine, anasema “utakapokutana na siri zenyewe utajua tu,
simama kwa muda kidogo, unapokutana nayo, chukua glasi ya maji kwanza
ujipongeze kwani wakati huo ni muhimu
sana katika maisha yako”.
Pesa na Roho.
Ndani ya kitabu mwishoni, Napoleon anaelezea sababu iliyomfanya aandae
kitabu hiki, kwamba ni kutokana na
mamilioni ya watu kote marekeani miaka hiyo ya 1930 kuwa katika lindi kubwa la woga wa umasikini. Kumbuka
miaka hiyo marekani na dunia kwa ujula ilikumbwa na mdororo
mkubwa wa uchumi (Greet Depression) baada
ya vita ya II ya dunia, mithili ya ule uliotokea hivi karibuni.
Uhusiano uliopo kati ya maswala
ya kiroho na kupata utajiri kwa Wamarekani ni jamba la kawaida tofauti na
sehemu nyingine kama huku Africa. Kwa Wamarekani ni maadili yao, kwamba utajiri ni
matokeo ya akili/fikra, ubunifu pamoja na uvumilivu. Hivyo Napoleon anahitimisha
kwamba, utajiri na mafanikiko huja kutokana na akili/fikra na wala siyo vinginevyo:-
Ukweli huo uligundulika miaka zaidi ya 70 iliyopita na bado mpaka hivi sasa
zama za mawasiliano ukweli huo unabeba mana ile ile.
Hamu (Shauku)
Kiungo kingine katika kupata utajiri Napoleon anasema ni hamu kubwa ya
kufanikisha jambo. Anaelezea habari ya mtu mmoja aitwae Edwin E. Barnes ambaye
hakuwa na chochote zaidi ya shauku kubwa ya kutaka kuwa Mbia (Partner) na tajiri
mvumbuzi maarufu Thomas Edson, mwishowe
huyo bwana alitimiza ndoto yake hiyo na
akafanikiwa pia kuwa tajiri mkubwa,
hakuanza na kitu zaidi ya hamu kubwa ya kutaka kuwa mbia wa
Edson.
Kwa ufupi hivyo ndivyo Napoleo
Hill alivyotunga kitabu chake, Think and Grow Rich Chenye sura 15 ambazo kila
moja imebeba hatua moja kuelekea utajiri
isipokuwa sura ya kwanza na ya 15 kwa maana hiyo kitabu kizima kina hatua 13 za
kuelekea utajiri kwa mujibu wa Napoleon
Hill mwenyewe. Sasa tuangalie kila sura pamoja na hizo hatua 13 kwa ufupi
zinasema kitu gani, Ili kuendelea kusoma
kinachofuata, bonyeza maandishi yafuatayo;
0 Response to "MAPITIO YA KITABU, THINK AND GROW RICH KWA UFUPI(UCHAMBUZI SANIFU)"
Post a Comment