Kuku wa mayai, hakuna shaka yeyote kuwa wanaweza katika
kipindi kifupi sana wakabadilisha maisha ya mtu yeyote yule kiuchumi licha ya
woga wa watu wengi ya kwamba kuku wa kisasa na hususani wale wanaofugwa kwa
ajili ya uzalishaji wa mayai wana hatari na changamoto nyingi.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hawakifahamu
na pindi tu mfugaji yeyote yule wa kuku anapokijua basi huo ndio utakaokuwa mwanzo wa neema kwake na
akiwa mchoyo hawezi kabisa kumdokeza mtu mwingine kwa dhana ileile potofu kuwa
akimjulisha na mwingine soko litapungua kumbe kitaalamu wala siyo kweli.
Siri kubwa katika shughuli hii ya ufugaji wa kuku na hasa
wale wa mayai si nyingine bali ni, kufahamu kwa undani taratibu na miiko ya
ufugaji wa kuku wenyewe wa mayai likiwamo pia na suala zima la mahitataji na
gharama za ufugaji wa kuku hao wa mayai kwa njia ya kisasa kabisa. Huwezi
kufuga kuku tuseme labda kuku 20 wakati fedha za kuwahudumia mpaka wiki
watakayoanza kutaga huna, matokeo yake utawalisha ‘kinjaanjaa’ jambo
litakalosababisha wakupe hasara badala ya faida
Kote katika jamii kumejaa elimu hii ya ufugaji wa kuku,
kuna majukwaa mbalimbali kuanzia kwenye mitandao ya kijamii, vitabu, majarida
na hata semina mbalimbali inakotolewa elimu ya ufugaji bora wa kuku wa aina zote, iwe ni wale wa mayai,
kuku wa nyama, kuku wa kienyeji na aina zingine zote za ndege wafugwao. Kwa
kifupi leo hii siyo vigumu hata kidogo kwa mtu kupata elimu ya ufugaji wa kuku
kitaalamu.
Katika makala haya nilipenda ufahamu, ni kwa jinsi gani unavyoweza
kuwa milionea kwa kazi ya kufuga kuku wa mayai tu, tena wala pasipo kupoteza
miaka mingi. Tena mamilioni hayo ya fedha unaweza ukayakisia wewe mwenyewe ni
shilingi ngapi kabla hata haujaanza
mradi wenyewe na huo ndio uzuri wa kufuga kuku wa mayai.
Hakuna biashara iliyokuwa nzuri kama ile ambayo unakuwa
na uwezo wa kutabiri kwa dhati kabisa baada ya muda tuseme miezi 22 na nusu
kama ilivyokuwa kwa kuku wa mayai unaweza ukashika kiasi gani cha pesa
kulingana na idadi ya kuku wako ulioanza nao.
Ikiwa utafuata taratibu zote kama inavyopendekezwa na wataalamu
ikiwa ni pamoja na kanuni zote za msingi, makisio au utabiri wako unakuwa na
uhakika wa asilimia zaidi ya 85%. Ina maana kuwa ikiwa utafuga kuku wa mayai
wapatao 1000 basi una uhakika wa kuwa na
kuku zaidi ya 850 watakaokuwa wakitaga utakapofika muda muafaka wa kutaga ambao
ni wiki kuanzia ya 18 tangia siku ya kwanzauingize vifaranga wa kuku wa mayai
bandani kwako.
Haya maneno si kama nayatunga kama hadidhi hapana, ni
matokeo ya tafiti za kweli ukiwemo utafiti nilioufanya mimi mwenyewe binafsi kama
mfugaji wa kuku wa mayai. Ikiwa utapenda kusoma Mchanganuo kamili wa biashara hii ya ufugaji wa kuku wa
kisasa wa mayai ili uweze kuamini kama ni kweli kuku wa mayai wanaweza
kukuletea utajiri, tazama mpango wa biashara huu hapa, jinsi biashara yaufugaji wa kuku wa mayai inavyoweza kumtoa mtu haraka katika umasikini.
Mchanganuo huo unaelezea kila kitu kuanzia gharama za
kuanzia kwa mtu anayefuga kuku wa mayai 1000, mbinu na mikakati mbalimbali
inayotumika katika uendeshaji wa mradi huu, gharama za uendeshaji, mapato na faida pamoja na timu nzima ya watu
wanaohitajika kuhudumia mradi huo.
..................................................................................................
Usikose
kujiunga hapa darasa la Michanganuo ya Biashara, kupata mambo mengi usiyoyapata
mahali pengine popote pale. Pamoja na kuwa mwanakikundi cha kushauriana mambo
mbalimbali ya kiuchumi na ujasiriamali.
Tafadhali niwaombe wasomaji radhi, kuna watu
walinitumia ujumbe kutaka kujiunga na darasa lakini kwa bahati mbaya sikuwajibu
kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, sasa nimerudi na kila kitu
kitakwenda kama kilivyokuwa kimepangwa. Asanteni sana wadau wangu wapendwa.
Tembelea pia na SMART BOOKS TZ kujipatia vitabu vyako vya ujasiriamali kwa lugha ya kiswahili.
0 Response to "KUKU NI UTAJIRI: ANGALIA MCHANGANUO JINSI KUKU WA MAYAI WANAVYOWEZA KUKUTAJIRISHA HARAKA"
Post a Comment