Vitabu vyako vya Self Help Books Limited vimerahisishwa ili kuweza kuwapa fursa watu wengi zaidi kuweza kuvisoma bila kikwazo chochote. Kitabu hasa cha "Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali" ambacho ilikuwa ni vigumu kumtumia mtu katika e-mail kutokana na ukubwa wa faili lake sasa wataalamu wetu wameweza kupunguza ukubwa wa faili la kielectronic(compression) mpaka likawa katika ukubwa unaokubalika.
Shughuli hiyo haijaathiri kwa namna yeyote ile ubora wa
kitabu chenyewe zaidi ya kukifanya kiwe ‘free’ zaidi unapokuwa ukishusha
ukurasa au kupandisha. Kadhalika pia kwenye email inachukua sekunde chache
zaidi kukidownloa(kupakua)
Vitabu vingine pia “Mifereji ya Pesa” na “Siri ya
biashara ya Rejareja”, navyo vimeboreshwa zaidi kuvifanya visomeke vyema zaidi
katika screen za simu za kisasa za Smartphone au Tablets.
Ndugu msomaji, ujuzi wa maswala ya biashara haupitwi na
wakati hata siku moa, hivyo nakutia moyo kama bado hukuwa umesoma vitabu hivi vizuri, basi
jitahidi kufanya hivyo kwani vimejaa mambo mengi yatakayokusaidia katika mapambano yako dhidi
ya umasikini na uboreshaji wa maisha kwa ujumla.
Siwezi kuchoka kuhubiri kitu
hiki;
“jifunze kupanga kwa weledi kila
jambo unalolifanya na hasahasa biashara
hata ikiwa kupanga huko utafanya kwa kichwa tu pasipo kuandika katika karatasi, kwani kupanga ndiyo msingi wa karibu kila jambo mwanadamu analolifanya hapa duniani.”
Nadhani Kabla ya kufanya jambo lolote huwa unafikiria
kwanza akilini, sasa kuwaza huko ndiko kupanga kwenyewe na unatakiwa
ujifunze namna bora zaidi ya kupanga
biashara yako iwe mpya au ulishaianzisha kitambo ikiwa utataka mabadiliko ya
kweli na ya haraka.
Achana na kudanganywa eti, “Mipango siyo matumizi”,
hiyo ni misemo ya jadi inayozidi kukufanya uamini kupanga hakuna maana wakati
kila siku unapanga. Unakuwa hauna tofauti na Ngamia anapojichimbia kichwa
mchangani akidhani kakwepa hatari kumbe kiwiliwili kingali bado nje na muda
wowote anaweza kutokea adui akamchoma mkuki.
Msomaji wangu ukihitaji kitabu chochote hapo, wasiliana
na mimi, unitumie E-mail yako na
kiasi cha fedha husika, nami nitakutumia kitabu chako mara moja pasipo
kuchelewa popote pale ulipo ndani na nje ya Tanzania. Namba zangu za simu ni 0712
202244 au 0765 553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo.
Ukitaka "Package" nzima yaani kifurushi cha vitabu vyote 3 ni shilingi elfu 18 tu, unapata maarifa ambayo kwingineko unaweza kulipa mpaka elfu 70, linganisha thamani na ubora. Asante sana kwa kusoma.
Napenda pia kukujulisha kuhusu DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA linaloendelea sasa katika blogu maalumu iliyoanzishwa iitwayo "Michanganuo ya biashara" Kwa taarifa zaidi na jinsi ya kujiunga na darasa hili bonyeza maandishi yafuatayo, Shule ya Michanganuo ya biashara Mtandaoni(TOSBP)
Ukitaka "Package" nzima yaani kifurushi cha vitabu vyote 3 ni shilingi elfu 18 tu, unapata maarifa ambayo kwingineko unaweza kulipa mpaka elfu 70, linganisha thamani na ubora. Asante sana kwa kusoma.
Napenda pia kukujulisha kuhusu DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA linaloendelea sasa katika blogu maalumu iliyoanzishwa iitwayo "Michanganuo ya biashara" Kwa taarifa zaidi na jinsi ya kujiunga na darasa hili bonyeza maandishi yafuatayo, Shule ya Michanganuo ya biashara Mtandaoni(TOSBP)
0 Response to "KUSOMA VITABU HIVI VYA MAENDELEO BINAFSI MTANDAONI SASA NI RAHISI MNO!"
Post a Comment