Tanzania School of Business Planning ni
darasa la kwenye mtandao lililobuniwa rasmi kwa ajili ya wale wasomaji wote
wanaopenda kujua namna ya kuandaa michanganuo ya biashara zao(Business planning)
kwa njia rahisi isiyohitaji utaalamu mkubwa. Siyo mipango ya biashara tu peke
yake bali wanachama watapata fursa ya kushirikishana masuala mengine muhimu
mengi katika biashara na ujasiriamali kwa lengo la kusonga mbele zaidi ya pale walipo.
Hapa ndipo jukwaa mtu yeyote anayependa
kufahamu kila kitu kuhusiana na Mipango ya biashara anaweza kuja na kukutana na
watu wengine wenye maono na mitazamo inayofanana kuhusiana na biashara na
maendeleo binafsi kwa ujumla.
Utajifunza kwa kina jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara au kwa lugha nyingine mpango wa biashara, kusoma na
kupitia mifano au michanganuo ya biashara halisi mbalimbali, kufahamu kwa
undani jinsi ya kupanga hesabu za biashara na namna ya kukisia mapato,
matumizi, faida na mambo mengine yote yahusuyo makisio ya hesabu za biashara.
Faida kubwa mwanachama anayoipata tofauti na
msomaji wa kawaida wa blogu ya jifunzeujasiriamali, ni fursa ya kuuliza chochote
kile ambacho anadhani kinamtatiza kwa upande wa mpango wa biashara au hata katika nyanja
zingine na kupatiwa majibu aidha na wakufunzi katika mtandao huu ama na mtu
mwingine yeyote yule aliyeko katika kundi hili maalumu, “Mastermindgroup” spesho kwa ajili ya mipango
ya biashara.
Shule hii maalumu itakuwa na madarasa mawili,
“ORDINARY CLASS OF BUSINESS PLANNING”, NA “ADVANCED CLASS OF BUSINESS PLANNING”.
Katika darasa la Ordinary mshiriki atajifunza mambo yote ya msingi juu ya
mpango wa biashara pamoja na kusoma michanganuo mbalimbali. Advanced class, wanachama
watashiriki katika kuandaa michanganuo ya biashara ya kiwango cha hali ya juu
kabisa hasa ya zile biashara zilizokuwa za ubunifu mkubwa na ambazo zinaweza
zikawa chanzo cha mawazo bora ya biashara endelevu na zinazolipa. Mipango kama
hiyo unaweza ukamuuzia mtu au kampuni kiasi kikubwa cha fedha na akanunua bila
matatizo.
Ada ya kujiunga na shule hii ni sawa na bure
lakini haiwezekani ikawa bure kabisa kutokana na sababu kwamba siyo kila
mtu atapendezewa na bidhaa au huduma fulani,
vinginevyo darasa hili tungeli-liweka moja kwa moja kwenye blogu hii ya
jifunzeujasiriamali ili kila mtu anayetaka ashiriki.
Lakini baada ya kukumbuka hadithi moja ya
watu kugawiwa bure vyandarua kwa ajili ya kujikinga na malaria kisha wengi wao wakaenda kuzitumia
kama nyavu za kuvulia samaki ilinibidi wazo la kuanzisha darasa hili bure
kabisa tuliache na kuweka kiingilio kidogo.
Mtu yeyote anayependa kujiunga na Madarasa haya anatakiwa kulipa ada ya kiingilio shilingi 10,000/= ambazo atapata fursa ya kuwa mshiriki kwenye semina. Pia atapewa bila malipo kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NAUJASIRIAMALI” katika mfumo-pepe(softcopy) kwa njia ya E-mail. E-MAI hiyo inatakiwa kuwa ni ya GMAIL mfano "mimi@gmail.com".
Kwa wale wateja wanaonunua kitabu halisi (Hardcopy) cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali kwa shilingi elfu ishirini wataingia kwenye semina bure bila ya kulipa chochote, na hii ni kwa wateja wote hata wale waliokwishanunua kitabu hicho siku za nyuma. Kwa walionunua kitabu hicho zamani wawasiliane na sisi kwa ajili ya kupata e-mail zao ili tuwaunganishe na blogu maalumu ya semina.
Kwa wale wateja wanaonunua kitabu halisi (Hardcopy) cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali kwa shilingi elfu ishirini wataingia kwenye semina bure bila ya kulipa chochote, na hii ni kwa wateja wote hata wale waliokwishanunua kitabu hicho siku za nyuma. Kwa walionunua kitabu hicho zamani wawasiliane na sisi kwa ajili ya kupata e-mail zao ili tuwaunganishe na blogu maalumu ya semina.
Baada ya kulipia semina na kututumia E-mail yako kupitia namba za simu 0712 202244 au 0765 553030 tutakuunganisha kwenye blogu
maalumu iitwayo, “DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA”. ambayo huwezi kuifungua mpaka umejiunga na semina hii. Tukisha kuunganisha utatumiwa meseji kwenye e-mail yako na kisha
wewe utafungua e-mail hiyo na kukubali mualiko uliotumiwa kwa 'kuklick' kubofya maandishi ya link hiyo.
Tayari sasa utakuwa umeshakuwa mshiriki kamili wa semina ya Michanganuo ya biashara na utaweza muda wowote ule kusoma mambo mbalimbali yaliyomo katika blogu
hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa michango yako kama mshiriki. Vilevile kila somo litatumwa kwenye e-mail ya mshiriki katika mfumo wa PDF mbali na kuwekwa kwenye hiyo blogu ili hata ikitokea kuna matatizo ya mtandao basi aweze kudownload na kuyasoma katika flash au chombo kingine chochote.
Mara unapolipia moja kwa moja unakuwa
umejiunga na Darasa la ORDINARY Level, darasa hilo humalizika pale masomo yatakapomalizika na mshiriki kuelewa jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara bila wasiwasi. Cheti cha mshiriki ni mpango wa biashara ambao yeye ndiye atakayekuwa ametoa wazo na ataandika kwa uangalizi na usaidizi wa karibu kabisa wa mkufunzi kuhakikisha kama ameelewa vizuri na mchanganuo huo utabakia kuwa mali yake mwenyewe.
Habar ya kazi..,kwa sisi tuliochelewa kuona haya mafundisho maweza pata masomo haya kwa njia yoyote ile..??
ReplyDelete