Ndugu na msomaji wa blogu
ya jifunzeujasiriamali, hayo siyo maneno yangu bali ni maneno ya Rais Mteule wa
Marekani Bwana Donald Trump na wala hajaanza kuyatamka leo, ni maneno
anayopenda kuyataja karibu kipindi chote cha maisha yake.
Katika moja ya vitabu vyake Trump alieleza namna alivyokumbana na vikwazo vya kila aina katika maisha yake na jinsi alivyotumia ubunifu, na uking’ang’anizi wake kuvigeuza vikwazo hivyo kuwa ushindi. Leo hii tena Trump anatudhihirishia tabia yake hii baada ya kushinda uraisi wa Marekani.
SOMA: Maajabu ya kufikiria mambo makubwa na ni kwanini ujiwekee malengo makubwa maishani.
Ukimfuatilia Trump japo kwa kweli huwezi ukakubaliana naye kwa asilimia kubwa yale anayoyaamini(Hata mimi binafsi kwa kweli hanivutii kwa baadhi ya misimamo yake) lakini kuna kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwake kwamba “Lolote lile akili yako inaloweza kulifikiria basi na ujue jambo hilo unao uwezo wa kulitimiza licha ya vikwazo vingi unavyoweza kukutana navyo njiani”
Hata katika kipindi cha katikati cha kampeni akiwa ameelemewa kabisa na kambi ya mpinzani wake Hilary Clinton alikuwa haachi kutamka maneno ya kumtia nguvu yeye na wafuasi wake kama haya; “Tutashinda, tutaushitua Ulimwengu”. Sidhani kama kuna kitu Trump alicholenga kukipata maishani mwake akakikosa labda iwe ni kuishi milele pasipo kufa ndiko kutakakomshinda, kama ni pesa amezipata nyingi, na sasa ameweza kuishika nafasi ya kisiasa ya juu zaidi duniani.
SOMA: Kuna wakati mtangazania Donald Trump alizomewa kama chizi vile lakini katu hakukata tamaa.
Hakuna siri kubwa hapa zaidi ya ‘kuamini anaweza’ pamoja na ‘kutokukata tamaa’ Kama umesoma kitabu “Think & GrowRich” nadhani utafahamu vizuri sana mbinu aliyotumia Donald Trump kufika pale alipo sasa. Hata wewe na mimi tunaweza kufanya mambo makubwa hapa Duniani ikiwa tu tutajifunza mbinu hizi alizotumia Trump hata ikiwa hatukubaliani na mitazamo yake.
Mpendwa msomaji na mwanachama wa Blogu ya Jifunzeujasiriamali sasa utakua ukipokea mara kwa mara makala za kutia moyo ndani ya e-mail yako. Makala hizo ni maalumu tu kwa wanachama wala hazichapishwi katika blogu ya jifunzeujasiriamali.
Naomba pia kuchukua fursa hii kukujulisha kuwa tumeanzisha darasa maalumu la kujifunza Michanganuo ya Biashara kwa kina katika blogu nyingine iitwayo,’ MICHANGANUO YA BIASHARA’ Blogu hii au darasa ni kwa ajili tu ya wale wanaohitaji kujifunza namna ya kuandaa mpango wa biashara na kiingilio chake au ada ni shilingi elfu 10 ambazo mshiriki anapewa na kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali bure. Kufahamu zaidi juu ya darasa hili bonyeza maandishi yafuatayo. (Tanzania Online School Of Business Planning(TOSOBP))
0 Response to "KAMWE, KAMWE, USIKATE TAMAA(NEVER, NEVER GIVE UP)"
Post a Comment