Sera ya utoaji wa Elimu Tanzania inayoendeshwa chini ya
Wizara ya Elimu inazitaka shule zote kutoka mikoa yote ya Tanzania kutoa elimu
bora kwa watoto wote kuanzia shule za chekechea au kwa jina lingine shule za
awali, shule za msingi, shule za sekondari mpaka vyuo vikuu.
Kwa kuzingatia kwamba miaka ya awali ya mtoto yeyote yule
ni muhimu mno katika ukuaji wake kiakili na hata katika nyanja zingine zote,
Serikali ya Tanzania iliamua kuweka mfumo wa elimu ujulikanao kama, 2-7-4-2-3+
ambao unajumuisha, miaka 2 ya awali(Kindergarten) au maarufu kama chekechea. Mtoto
huanza chekechea akiwa na umri kati ya miaka 4-6.
Elimu ni ufunguo wa maisha, |
Miaka saba 7 ni kwa ajili ya shule ya msingi “Primary
School Education”. Miaka 4 ni Elimu ya Sekondari, kidato cha kwanza hadi cha
nne 4 “Ordinary Level”, ngazi hii mtoto hujiunga baada ya matokeo ya la saba
kutoka. Miaka 2 mtoto husoma elimu ya sekondari ya juu(Advanced Level ‘A Level”)
ambapo hujiunga na ngazi hiyo baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, ambapo
huangaliwa ufaulu katika matokeo ya Baraza la Mitihani Tanzania “NECTA”
Miaka 3 na kuendelea ya mwisho huwa ni kwa ajili ya
kusoma vyuo vikuu au vyuo vingine na taasisi za ufundi. Hapa ndipo utakutana na
vitu kama, Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu, Mikopo ya elimu ya juu na hata Bima
ya afya.
Lakini yote kwa yote kila kitu kinaanzia pale chekechea
ingawaje shule za chekechea, walimu wa chekeche na hata vyuo vya kufundisha
ualimu wa chekechea bado havijapewa uzito na umuhimu unaostahili. Mfumo wa
Elimu ya Tanzania una uhusiano mkubwa sana na mfumo wa ajira Tanzania. Ajira
Tanzania huwezi ukailinganisha na ile ya wenzetu kama Kenya, Uganda na hata
Zambia.
Sababu kubwa ni kwamba wenzetu hao majirani wameweka
msisitizo na umakini mkubwa zaidi katika elimu ya watoto wao ya nursery(chekechea)
hasahasa katika upande wa lugha, simaanishi kwamba kiingereza
ni bora kushinda kiswahili, la hasha, ila pointi yangu hapa ni “consistence”
au kwa maneno mengine msisitizo katika lugha moja kwanza kuepusha kuwachanganya
watoto katika hatua hizi muhimu za awali.
Mwanafunzi hujenga tabia ya kujiamini na kuwa na fursa
nzuri zaidi ya kuajiriwa endapo atakuwa mahiri katika ile lugha atakayokuwa
anakwenda kuitumia kwenye ajira. Sisi Watanzania tuliokuwa wengi ni “uvuguvugu”.
Kwenye kiingereza hatupo na wala kwenye kiswahili pia hatumo vizuri. Na hii
ndiyo sababu kubwa inayotufanya tukose kujiamini(lose confidence) mbele ya
majirani zetu Wakenya na wengineo, tunabakia kuwa “less competent” linapokuja
suala la ajira kimataifa. Yoote haya huanzia vidudu(chekechea).
Ndiyo maana siku hizi kuanzisha shule bora ya chekechea
Tanzania kunatafsiriwa na wengi kuwa ni lazima shule hiyo iwe ni “English
Medium”, yenye kufundisha `kwa lugha ya Kiingereza. Watu tunasahau kwamba ili
mtoto aweze kuwa na uelewa mzuri wa masomo yake kuna vitu vingi vya kuzingatia
mfano, nguo za watoto, chakula cha watoto, ratiba nzuri ya chakula, michezo ya
watoto nk.
Hata matokeo mazuri kidato cha nne 4, yale ya darasa la
saba 7, kidato cha sita 6(form six), vyuo na hata vyuo vikuu yanategemea sana
ni jinsi gani mtoto alivyowekewa msingi imara tangu alipokuwa darasa lake la
awali(nursery school).
SOMA: Maktaba ya vitabu inayotembea mashuleni.
SOMA: Maktaba ya vitabu inayotembea mashuleni.
Hapa chini kuna muhtasari wa Mchanganuo/mpango wa
biashara ya uanzishaji wa shule ya chekechea(Day Care Centre) au wengine
hupenda kuiita “Nursery”
Huo ni ufupisho wa mpango mzima, unaweza ukausoma wote kwenye kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI”. Ndani ya kitabu
hicho cha kurasa 410 kuna michanganuo mingine halisi ya biashara mbalimbali zinazolipa
unazoweza ukaanzisha hapa Tanzania. Michanganuo meandikwa kiubunifu kuchochea
mtu kuwa mbunifu na hata unaweza ukaitumia michanganuo hiyo kama ramani wakati
ukiandika mchanganuo wa biashara yako yeyote ile.
Hata kama hauna “interest” ya kuandika mpango wa biashara
, lakini kwa kuisoma michanganuo hiyo peke yake unapanuka kimawazo juu ya
biashara mbalimbali na kupata ‘triki’ nyingi ambazo pengine ulikuwa bado
haujazigundua.
SOMA: Kwanini uandike mchanganuo wa biashara yako kabla ya kuanza biashara yenyewe.
SOMA: Kwanini uandike mchanganuo wa biashara yako kabla ya kuanza biashara yenyewe.
Vitabu vya Michanganuo na Ujasiriamali vipo, na
unaweza ukapata nakala yako kwa kuwasiliana na mimi kupitia namba, 0712 202244
au 0765 553030 kisha utaletewa kitabu
chako mpaka pale ulipo kama wewe unaishi Dar es salaam . Malipo yanafanyika
ukishapokea kitabu na Bei ya kitabu kimoja ni TSH. 20,000/-, elfu ishirini tu.
Kama upo Mikoani pia wasiliana na sisi kwa namba hapo
juu, kisha baada ya kulipa fedha sh. 20,000/= pamoja na gharama ya
usafirishaji, tunakutumia kitabu kupitia mabasi yanayokwenda mikoani kutokea
Dar. Vitabu ni vya kawaida vya karatasi.
Ikiwa utataka kitabu kwa e-mail(Softcopy)PDF bei huwa
inapungua na ni shilingi 10,000/= elfu kumi tu kwa kitabu kimoja.
…………………………………………………………………….........
Mpango wa Biashara ya Shule ya Chekechea, shule ya awali.
(Jinsi ya Kuanzisha Shule ya Vidudu, Nasari)
SHULE
YA CHEKECHEA.
Cheichei Day Care
centre.
MUHTASARI.
Cheichei Day Care ni Kituo kitakachokuwa
kikijihusisha na uangalizi na ufundishaji wa watoto wenye umri
kuanzia mika 3 hadi mitano. Kutokana na
mfumo wa maisha siku hizi kubadilika tofauti na miaka iliyopita, familia nyingi hasa hasa maeneo ya
mijini baba na mama wote utakuta wanafanya kazi hivyo kuwa vigumu kukaa na
watoto wao wadogo wakiwaangalia kuanzia asubuhi mpaka jioni. Cheichei watalenga familia za namna hii.
Katika miaka
mitatu ya mwanzo Cheichei wamejiwekea
malengo yafuatayo-
(i) Kuhakikisha
wazazi wote wa watoto watakaowaangalia kituoni
wanafanya kazi zao mchana kutwa huku wakiwa hawana wasiwasi juu ya
usalama wa watoto wao.
(ii) Kupokea
watoto wapatao 20 katika mwaka wa
kwanza na kuongezeka kila mwaka kwa
asilimia 50%.
Kituo
kitamilikiwa kwa ubia kati ya Bibi Joys Komba na Mama Teresia Nduguru ambao wote
ni waalimu wastaafu wa shule za msingi wenye uzoefu wa kutosha katika shughuli za ufundishaji na uangalizizi wa watoto.
Jumla ya
mahitaji yote ya kuanzia biashara ni shilingi milioni 20, vifaa,
gharama mbalimbali pamoja na fedha za
akiba.
1.1 Dhamira kuu.
Dhamira kuu ya
Cheichei Day Care ni kutoa uangalizi wa
hali ya juu pamoja na mafuzo bora kwa watoto
ambao wazazi au mzazi huwa kazini nyakati
za mchana. Wazazi hao hufanya kazi zao kwa kujiamini huku wakijua
watoto wao wapo salama kwa
asilimia mia moja.
1.2 Malengo.
Katika miaka
mitatu ya mwanzo Cheichei kitakuwa na malengo yafutayo;
· Kutoa
uangalizi na mafunzo kwa watoto
yenye ubora wa hali ya juu, huku wazazi
wao wakifanya kazi zao pasipo kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa watoto wao.
· Kuhakikisha ndani ya mwaka wa kwanza wanapata watoto
wapatao 20.
·
Kuongeza
idadi ya watoto kila mwaka kwa asilimia 50%
· Kutoa
malipo mazuri kwa wafanyakazi wao wote pamoja na gawio zuri kwa wamiliki kila
mwaka.
Nawezaje kupata soft copy ya mchanganuo huu wa kuanzisha shule ya awali? WhatsApp 0754947671
ReplyDeleteUnaweza kupata tuwasiliane tu, 0765553030
DeleteNaomba soft copy ya mchanganuo was daycare
ReplyDeleteUnaweza kupata upo, tuwasiliane namba zangu ni 0712202244 au 0765553030
DeleteJe ntasajili vipi kituo
ReplyDeleteNaomb kupata soft copy y mchanganuo huo
ReplyDeleteKaribu, nitext watsap kwa 0765553030
DeleteNaomba soft copy ya mchanganuo wa day care
ReplyDeleteDuuu muda Muafaka Sana je naweza kupata soft copy ya mchanganuo wa kuanzisha day care na namna ya kusajili,? E-mail yangu ni moshiro getrude @gmail. Com
ReplyDeleteNitawasiliana nawewe asante
DeleteNashukuru Sana! Nahitaji mchanganuo pia napenda kufahamu jinsi ya kusajiri kituo. 0686 061 829
ReplyDeleteNawewe pia nashukuru
DeleteTafadhari naomba nakala ya mchanganuo huu wa Day Care Center email.fredkatulanda@gmail.com
ReplyDeleteMkuu naomba mchanganuo wa biashara ya shule 0865399321
ReplyDeleteTuwasiliane nikutumie karibu 0765553030
DeleteNaomba kupata Mchanganuo 0756323474
ReplyDelete