VITU HIVI VITANO 5 VITAKUPA MAFANIKIO, FURAHA MOYONI NA AMANI YA NAFSI MAISHANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

VITU HIVI VITANO 5 VITAKUPA MAFANIKIO, FURAHA MOYONI NA AMANI YA NAFSI MAISHANI

Unaweza ukamiliki fedha, mali na utajiri mwingi lakini pasipokuwa na furaha, utulivu wa nafsi na amani moyoni mwako, hesabu hauna mafanikio katika maisha yako. Katika makala niliyoandika hivi karibuni isemayo, 2017 ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena au “Make Your Self Great Again”, nilitangaza kwamba tumeanza rasmi msimu ama kampeni mpya ya KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO ULIOPOTEZA.
Ulipokuwa chekechea
Na moja ya malengo ya kampeni hiyo ni pamoja na kuhakikisha kwamba watu hawafurahii tu maisha yenye neema kiuchumi, bali maisha yaliyojaa furaha na amani ya nafsi, vitu ambavyo huhesabiwa kama ndiyo utajiri wenyewe halisi.

SOMA NA HII: Malengo Dira na Dhamira yako kwa mwaka huu ni nini? jipange sasa hujachelewa bado.

Katika kukamilisha furaha ya mtu, hauwezi ukasema eti kitu kimoja tu kinao uwezo wa kuleta furaha. Furaha na utulivu wa nafsi  ya mtu huchangiwa na mambo mengi  mbalimbali yakiwamo, hali bora ya kiuchumi, afya njema ya kimwili na ya kiroho pamoja na hali bora ya kiakili. Kwa hiyo katika kampeni yetu hii tutakwenda sambamba na vitu(mambo) hayo yote manne tukichambua jinsi vinavyoweza vikachangia mtu kuwa na furaha na utajiri wa kweli maishani.
Ukiwa Shule ya msingi.
Leo hii tutakwenda kuviona vitu vitano (5) vinavyochangia kumpa mtu furaha na utulivu wa nafsi moyoni. Kujifunza vitu hivyo na kuvifanyia kazi havimgharimu mtu hata senti tano isipokuwa tu muda wako na jitihada binafsi.

NJIA TANO(5) UNAZOWEZA UKAZITUMIA KUJIONGEZEA FURAHA NA AMANI YA NAFSI MAISHANI KATIKA KUUFIKIA UTAJIRI WA KWELI.

1. KUCHEKA.
Wahenga hawakukosea waliponena “Kucheka huonngeza siku za mwanadamu za kuishi” ukweli huu unajidhihirisha wazi katika maisha ya kila siku ya mtu, hata wataalamu wamegundua kwamba mtu unapocheka unaongeza mzunguko wa damu mwilini  na kusababisha kuongezeka pia kwa kichocheo(enzyme) iitwayo “Endorphiny” inayohusika na kuongezeka kwa furaha ya mtu.

Na hata baada umeshahitimu shahada yako ya chuo kikuu.
Jitahidi kufanya shughuli zinazokufanya ujisikie kucheka kama vile kutazama michezo ya kuchekesha na kujumuika katika mazungumzo na watu wengine huku ukikwepa vitu vinavyokukasirisha.


2. KUTAFAKARI(MEDITATION)
Hii ni njia nyingine unayoweza ukaitumia kujiongezea furaha ya nafsi . Kutafakari humsaidia mtu kuzama ndani kabisa mwa hali ya akili, kitendo kinachoondoa msongo wa mawazo pamoja na mawazo hasi. Utulivu kupitia tafakari husaidia katika utoaji wa kemikali na vichocheo mwilini vinavyopambana na vichocheo vya msongo wa mawazo kama vile ‘Adrenaline’ na ‘Cortisol’ ambazo huweza kumfanya mtu  ajisikie mwenye aibu na asiyekuwa na furaha, hivyo kuziondoa na kuweka kemikali za kukufanya ujisikie vizuri kutakufanya uione dunia kuwa bora zaidi. Kutafakari kwa kina kila siku kutayafanya maisha yako kuwa mepesi na yaliyojaa furaha.

SOMA: Uwe ni mwaka wa kufanya mapinduzi makubwa katika maisha yako.

3. KUJISHUGHULISHA NA KAZI ZINAZOJENGA.
Kuwa ‘bize’ lakini siyo kupindukia kutakufanya ujisikie vizuri. Badala ya kutumia muda wako wote kwenye TV au vyombo vingine vya habari vya kisasa kama simu na kompyuta. Fanya vitu chanya kama vile kuimba muziki, kuchonga, kutarizi au hata shughuli zingine za kawaida zinazokuvutia kufanya.

4. KUJILAZIMISHA KUTOKUFIKIRIA MAMBO HASI AKILINI.
Duniani hamna mtu asiyekasirika, kuwa na wivu au kinyongo. Watu wote kwa nyakati tofauti hupatwa na hali hizi lakini kinachotakiwa, haraka unapopatwa na hali kama hizo basi mara moja jilazimishe kuzisitisha pasipo kusukumwa na mtu, na badala yake anza kufikiria akilini kitu kingine kizuri cha kupendeza, kwa mtindo huo utajizoeza taratibu kufikiri mambo yaliyokuwa chanya zaidi yatakayokufanya muda wote uwe ni mtu mwenye furaha na amani.

SOMA: Je wajua kitu binadamu anachokipenda kuliko vingine vyote duniani?

Kupata furaha na amani moyoni kupo ndani ya uwezo wa mtu mwenyewe ikiwa tu atachukua hatua stahiki. Asijekukudanganya mtu kuwa eti ili mtu uwe na furaha na utulivu moyoni mwako ni sharti uwe na fedha nyingi au uwe tajiri bilionea.

5. LENGA KUFANYA YALE YALIYOKUWA MUHIMU KWAKO TU
Watu wengi hujikuta wakielemewa na mzigo wa kufanya vitu vingi kutokana na kuzidiwa mno na taarifa nyingi kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari vilivyotapakaa kila kona ya nchi kama vile, Redio, TV, mabango, mtandao wa intaneti nk. Vyombo vyote hivi hupendekeza maelfu kwa maelfu ya njia mtu anazopaswa kufuata maishani ili aishi vizuri kama vile, ni nini mtu ununue, ni wapi mtu uende, ni nini mtu ule, ni nini mtu uvae, na hata ni kitu gani unachokihitaji maishani.

SOMA PIA NA HII: Kina mama chanzo kikuu cha furaha kwa watoto wao bila kujali wana umri gani.

Lakini kitu muhimu kushinda vyote hapa ni kwa wewe kujifunza jinsi ya kuzielekeza nguvu na mawazo yako katika vile vitu tu ambavyo kweli vina umuhimu mkubwa kwako kimaisha, jifunze mwenyewe pia kutambua ni nini hasa unachokihitaji maishani bila kupendekezewa na mtu au chombo chochote kile cha habari.

Mambo haya utaweza tu ukayatimiza kupitia nidhamu ya hali ya juu ya maisha. Unaweza kuanza kwa kupunguza matumizi ya intaneti, TV na vyombo vingine vyote vya habari kwa kufuatilia katika vyombo hivyo vile vitu muhimu tu kwako huku ukiachana na vile vitu ambavyo havina uwezo wa kuongeza chochote cha maana katika maisha yako. Pia tafakari(meditate) angalao kwa dakika 30 kila siku itakusaidia sana.

…………………………………………………………………………

Ndugu msomaji wa Blogu hii ya jifunzeujasiriamali, kuelekea kumaliza mwaka huu wa 2016 na kuingia mwaka mpya wa 2017, hebu tubadilishe fikra zetu kabisa na kuibua tena ule ukuu tuliokuwa nao nyakati fulani za maisha yetu, nyakati hizo zaweza kuwa ni kipindi ulichokuwa shule ya msingi, chekechea, sekondari, chuo, kipindi kabla hujaoa, kuolewa, kipindi ulipokuwa kijana, kipindi ulipopata kazi yako ya kwanza, kipindi ulipokuwa ukifanya biashara yako kwa mafanikio, kipindi ulipokuwa mcha Mungu sana nk.

Nakusihi katika kampeni hii tuwe pamoja mpaka mwisho, lakini nakushauri pia tukiwa njiani usiache jambo moja muhimu sana ambalo ni kama chachu au kichocheo cha kuweza kuufikia ukuu wako tena (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN). Chachu hiyo si nyingine bali ni kujikomboa kiuchumi. Kujikomboa kiuchumi peke yake hakutaweza kukurudishia tena ukuu wako, ni lazima kuwe na viungi vingine ambavyo utakuwa ukijifunza ndani ya kampeni hii. Lakini kiungi hiki cha hali ya kiuchumi huwa kama ndiyo hamira kwa viungo vingine vyote.


Kuhakikisha unakuwa na kiungo hiki muhimu cha hali bora ya kiuchumi basi nakushauri usikose kusoma angalau moja ya vitabu vyetu vya Self Help Books Tanzania. Kusoma vitabu mbalimbali ingia katika ukurasa huu hapa, SMARTBOOKSTZ uchague kitabu.   

0 Response to "VITU HIVI VITANO 5 VITAKUPA MAFANIKIO, FURAHA MOYONI NA AMANI YA NAFSI MAISHANI"

Post a Comment