Muda mchache uliopita leo hii nimepigiwa simu
na mkazi mmoja kutoka Mkoani Njombe Wilaya ya Wanging’ombe aitwaye Lameck Lupaya na kunijulisha kwamba yeye
amenipata kupitia mtandaoni, bila shaka namba aliiona kwemye blogu hii.
Mazao ya mahindi mabichi |
Lameck alinijulisha juu ya fursa kubwa na
nzuri iliyopo Mkoani Njombe hususan ya mazao ya kilimo kama matikiti maji,
mahindi, maharage, nyanya, na mboga za majani zikiwemo pilipili hoho. Alisema
lakini wakulima wa huko wana changamoto kubwa ya soko la mazao yao na akasema zao
kwa mfano la tikiti ni zao linalokua haraka sana hivyo kuwa na fursa kubwa mno.
Alinidokeza haja yake ya kutafuta washirika
hata ikiwezekana watakaoungana naye katika kutafuta masoko maeneo mengine kama
jiji la Dar es salaam na kisha kuwatafutia wakulima masoko ya mazao yao katika
maeneo yenye uhakika wa masoko ambapo wakulima hao watatoa kamisheni fulani, kama
sikosei bila shaka alikuwa akimaanisha yeye na hao washirika ‘kuact’ kama watu
wa kati.
Mimi binafsi nilimjibu kwamba hilo ni wazo
zuri sana na ninachoweza kufanya kama mhamasishaji wa maswala ya biashara na
ujasiriamali kwa sasa ni kuhakikisha ujumbe wake naufikisha kwa wadau wengine
kupitia blogu hii ya jifunze ujasiriamali kama tangazo. Vile vile mjasiriamali
huyu alinipa na namba zake za simu ambazo pia naziweka hapa ili kama kuna mtu
yeyote mwenye ‘interest’ na fursa hii basi wawasiliane, 0679325541 na 0756425541 .
…………………………………………………………………
Aidha
blogu hii haihusiki wala haiwajibiki kwa matangazo yanayowekwa humu, unapofanya
biashara na mtu yeyote aliyeweka tangazo humu hakikisha mnapitia taratibu zote
muhimu za kibiashara.
0 Response to "CHANGAMKIA FURSA HII MPYA YA MAZAO YA TIKITI MAHINDI, MAHARAGE NYANYA NA MBOGAMBOGA"
Post a Comment