Vifuatavyo ni baadhi tu ya vipande(siyo
hotuba kamili) vya hotuba ya Raisi wa 45 wa Marekani Donald J. Trump punde tu
baada ya kuapishwa kuingia ikulu ya white house ya Marekani.
"Hatukabidhi madaraka kutoka utawala mmoja
kwenda mwingine au chama kimoja kwenda chama kingine bali bali tunahamisha
madaraka kutoka Washington DC kwenda kwenu watu……..
Hii ni siku yenu
Hizi ni sherehe zenu…………
Kilichokuwa muhimu siyo chama gani kinachotawala
serikali yetu bali ni ikiwa serikali inatawaliwa na watu
Wanaume na wanawake wa Taifa letu
waliosahaulika, hawatasahaulika tena, kila mtu anawasikiliza sasa.
Kwa miongo mingi tumekuwa tukivitajirisha
viwanda vya nje kwa gharama za viwanda vya Marekani, kutoa ruzuku kwa majeshi
ya nchi nyingine wakati tukiruusu mdororo wa kuhuzunisha wa jeshi letu
Tumekuwa
tukilinda mipaka ya mataifa mengine wakati tukikataa kulinda ya kwetu wenyewe.
Na tumepoteza matrilioni kwa matrilioni ya dolla nje wakati miundombinu ya
Marekani ikiishia kuoza na kukatisha tamaa
Tumezifanya
nchi zingine kuwa matajiri wakati utajiri, nguvu na kujiamini kwa nchi yetu
kukipotelea kwenye upeo wa macho.
Viwanda
kimoja baada ya kingine vimefungwa na kuacha fukwe zetu zikiwa hazina hata wazo
moja kuhusiana na mamilioni kwa mamilioni ya Wafanyakazi wa Marekani walioachwa
nyuma.
Utajiri
wa watu wetu wa tabaka la kati umeporwa kutoka majumbani mwao na kisha
kugawanywa tena kote duniani. Lakini hiyo ilikuwa ni zamani na sasa tunatazama
mbele tu…………………
Marekani
itaanza kushinda tena, kushinda kuliko ilivyoshinda awali
Tutazirudisha
ajira zetu.
Tutairudisha
mipaka yetu
Tutaurudisha
utajiri wetu, na tutazirudisha ndoto zetu…………………..
Hatutafuti
kulazimisha njia yetu ya maisha kwa mtu yeyote, lakini badala yake kuiacha ing’are
kama mfano
Tutang’ara
kwa kila mmoja kuiga mfano.
Mwisho,
ni lazima tufikiri mambo makubwa na hata kuota mambo makubwa zaidi. Katika
Marekani tunatambua kwamba Taifa
linaishi tu ikiwa kama litafanya jitihada. Hatutaendelea tena kuwakubali
wanasiasa ambao wote huongea pasipo vitendo, wakilalamika mfululizo lakini bila
ya kufanya chochote.
Muda wa
mazungumzo matupu umemalizika. Sasa saa ya vitendo imewadia
Usimruhusu
mtu yeyote kukuambia kwamba haiwezekani kufanyika. Hamna changamoto inayoweza
ikafanana na moyo na mapambano na roho ya Marekani. Hatutashindwa. Nchi yetu
itanawiri na kuwa tajiri tena.
Kwa
pamoja tutaifanya Marekani kuwa na nguvu tena, tutaifanya Marekani kuwa tajiri
tena, tutaifanya Marekani kujivunia tena, tutaifanya Marekani kuwa salama tena
Na,
ndiyo, pamoja tutaifanya Marekani kuwa yenye nguvu tena
Asanteni
Mungu
awabariki
Na
Mungu Ibariki Marekani”
0 Response to "HOTUBA YA KWANZA KABISA YA RAIS DONALD J. TRUMP BAADA YA KUAPISHWA KUINGIA IKULU WHITE HOUSE"
Post a Comment