Biashara ya jumla hapa Tanzania ni biashara
yenye fursa kubwa ukizingatia kwamba maduka na biashara nyingi za
rejareja, hutegemea kununua bidhaa kutoka kwayo
kwa ajili ya kuuza. Maduka ya jumla yamegawanyika makundi mawili, yale
yanayouza bidhaa za aina moja tu na yale yanayouza bidhaa mchanganyiko.
Vinywaji baridi maana yake ni vinywaji visivyokuwa na
kileo. Maduka ya jumla mengi yanayouza vinywaji baridi utakuta ni maduka yenye
mchanganyiko wa bidhaa mbalimbali kama vile utakuta yakiuza soda mchanganyiko
na vinywaji vingine kama maji, juisi, maziwa ya paketi, vinywaji vya kuongeza
nguvu mwilini(energy drinks) nk.
Ukitaka kuanzisha duka la jumla hasa la vinywaji baridi
na uone mafanikio yake haraka itakubidi uwe na mtaji wa kutosha kuhakikisha
vinywaji vyote muhimu wateja wanapofika dukani hawavikosi. Kiasi cha mtaji
kitategemea ni skock ya bidhaa kiasi gani utakachoamua kuwa nacho dukani kwako.
Ikiwa hautapenda kuagiza vinywaji kiwandani mara kwa mara basi itakupasa uweke
stoku ya kutosha.
Uendeshaji wa duka la jumla ni kama zilivyokuwa biashara
zingine tu kwani utahitaji mtaji, mtu wa kuuza, mtu wa kutoa na kuweka mizigo
stoo, mtu wa kufungia wateja mizigo pamoja na mtu wa kufuatilia wateja mitaani.
Lakini kama bado mtaji wako ni kidogo unaweza ukawa na msaidizi mmoja tu halafu
shughuli zote mkafanya watu wawili tu na pengine mtu mmoja tena wa
muda(partime) kama vile mbebaji mizigo ambaye hulipwa na wateja wanaokuja
kununua bidhaa.
Katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI,
miongoni mwa michanganuo ya biashara iliyokuwepo, upo mchanganuo wa biashara ya
duka la jumla la vinywaji baridi, biashara iliyopo Malapa jijini Dar es salaam.
MCD Provision Store linamilikiwa na bwana Chacha Mwita na husambaza vinywaji
baridi maeneo mengi ya Buguruni Malapa na baadhi ya maeneo ya Temeke.
Ufuatao ni muhtasari wa mchanganuo huo ambao kwa yule
mwenye kitabu hicho anaweza akausoma mchanganuo huo mzima pamoja na michanganuo
mingine mbalimbali ya biashara za Kitanzania zinazolipa.
DUKA
LA JUMLA.
MCD Provision Store.
Duka la jumla la vinywaji baridi Malapa Cold Drinks Provision Store, MCD ni duka litakalouza vinywaji vya aina mbalimbali visivyo na
kileo. Litaanzishwa katika eneo la
Buguruni Malapa na kuhudumia maeneo yote ya jirani pamoja na wateja wanaotoka maeneo nje ya hapo. MCD
Provision mwaka 2013 imeweka lengo la kuingiza mapato yanayofikia shilingi milioni 450.
MCD imepanga kufikisha huduma zake za
usambazaji wa vinywaji visivyokuwa na kileo katika manispaa nzima ya Ilala pamoja
na baadhi ya maeneo ya Temeke. Mmiliki wa duka hili ni bwana Onesmo
Chacha ambaye baada ya kuuza sehemu ya shamba kubwa alilorithi kutoka kwa babu
yake kijijini kiasi cha shilingi milioni 70 aliamua kuja kuanzisha duka hilo.
MDC litauza bidhaa zifuatazo.
·
Soda aina zote.
·
Maji
aina zote.
·
Juice
aina zote.
·
Malta.
·
Redbull
na
·
Bavaria
Maeneo ya Buguruni, kuna maduka mengi
ya reja reja pamoja na Bar/Groceries, vyote hivi huhitaji vinywaji kwa ajili ya
kuwauzia wateja rejareja.Makadirio ya mauzo katika miaka mitatu yamekisiwa
kutokana na utafiti uliofanyika kuhusiana na soko la vinywaji baridi lililopo
katika eneo la Buguruni sokoni, Malapa pamoja na yale maeneo MDC inayopanga kufikisha huduma
zake.
1.1. Dhamira kuu.
MCD
Provision Store imedhamiria kutoa
huduma bora za usambazaji wa vinywaji
visivyokuwa na kileo katika
maduka, mabaa na sehemu yeyote
yenye shughuli kwa bei nzuri
pamoja na usafiri wa uhakika.
1.2. Malengo.
·
Kusambaza
vinywaji katika kata zote za Ilala na
baadhi ya maeneeo ya Temeke ifikapo
mwaka 2014.
·
Kuongeza
pikipiki za matairi matatu kutoka 1
mpaka kufikia 3 ifikapo mwaka wa 2015.
·
Kufikisha mauzo yapatayo milioni 560 ifikapo mwaka 2015.
2.0 Maelezo
kuhusu biashara
MCD
Provision chini ya mmiliki wake bwana Onesmo Chacha Mwita itajijengea umaarufu
wa kipekee kwa wateja wake kutokana na kuwafikishia vinywaji mpaka mlangoni mwa
biashara zao. Mtaji wa kuanzishia biashara hii aliupata baada ya kuuza sehemu
ya shamba kubwa alilorithi kutoka kwa marehemu babu yake huko kijijini Migori.
2.2 Historia
ya Biashara.
Miaka kabla
ya 2012 katika eneo zima la Buguruni Malapa kulikuwa na maduka machache sana yaliyokuwa yakiuza vinywaji vya jumla visivyokuwa na
kilevi, hata maduka machache yaliyokuwepo
mteja ilimbidi aende na usafiri wake au
mtu maalumu wa kumbebea mzigo. Onesmo
kwa kuliona hilo mwaka huo huo mwezi
Septemba aliamua kuanzisha mipango ya kufungua
duka katika eneo hilo baada ya kuacha kazi katika kiwanda cha soda.
Mwanzoni MCD
itatoa huduma katika maeneo machache tu lakini baadaye itafika hata maeneo mengine ya mbali kama vile; Buguruni kwa Mnyamani,
Buguruni Madenge na Ilala Shariff Shamba.
Itaanza na mfanyakazi mmoja na baada ya miezi michache itaongeza kufikia watatu.
2.3 Kianzio.
Gharama
mbalimbali zitahitajika wakati wa kuanza, nazo zimekisiwa kama ifutavyo; usajili,
uwekaji wa bango pamoja na ukarabati wa chumba cha biashara jumla Sh. 500,000/=.Vile
vile kutahitajika rasilimali mbalimbali zikiwemo, fedha taslimu, bidhaa za
kuanzia, mali nyinginezo na mali za kudumu kama vile pikipiki ya bajaji na
makreti ya soda jumla shilingi 52,000,000/= Chati na majedwali yafuatayo
vinaelezea kwa ufupi makisio hayo. Jumla ya fedha zote za mahitaji ni Sh.52,500,000/=. Na zitatokana na mauzo ya shamba la urithi
Shilingi milioni 70.
0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA DUKA LA KUUZA VINYWAJI BARIDI MCHANGANYIKO NA MAJI"
Post a Comment